Monday, January 27, 2020

BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA ISHILINI NA SITA







ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TANO : “kumbe mama yule kijana ulie nisimulia ni huyu Edgar” aliuliza Malaika kwa mshangao mkubwa, “tena jina lake nimelijuwa jana ulipo litaja kwenye simu jana usiku, unajuwa ilifikia kipindi niliomba kuwa ndio angekuwa mchumba wako” Waliongea huku wakinywa chai, chai ambayo mama Malaika aliita ni chai nzito, tena akuitaji kabisa chai yenyewe yeye alikula na kushushia maji kutokana na pombe alizokunywa jana, walifanya yote kwa shangwe, pasipo kujuwa kuwa nje kuna mtu na wachungulia na kuwasikiliza wanacho ongea, endelea.......
Pale nje ya nyumba ya Edgar, baada ya kulizika, naliyo yasikia, yule mtu pale dirishani akatoka na kurudi kwa wenzake, yani Para na vijana wake wawili na mwanamke mmoja wakiwa ndani ya gari, mbari kidogo toka kwanye nyumba ya Edgar, ni mita mia mbili toka kwa kina Edgar, wakiwa wameshuhudia kila kitu, kunzia mama Malaika alipo kutana na Edgar ambae walikuwa wanamtilia mashaka, liicha ya kumkumbuka vyema kuwa kuna siku aliwai kuwashushia kipigo, walipo jaribu kukaba mzee Haule, Malaika mwenyewe alipo toka nje na kupokea begi kwenye gari, waliwaona walipoingia ndani, na huyu mwenzao, aliwasimulia alicho kisikia mle ndani, Para na vijana wake wakaondoka zao, wakipanga kurudi jioni kwa ajili ya kuwakamata wakina Edgar, waliamini kazi yao imekuwa lahisi sana, “lakini mna mkumbuka yule kijana,?” aliuliza mmoja wa, “leo tutakuwa na bastora, wala msiogope” aliwaondoa wasi wasi bwana Para “tena kamwambie mzee Komba, kuwa huyu mama anahusika na mpango mzima wa kumtorosha mwanae kanisani” aliongea yule mwanamke kwa msisitizo, maana waliamini hivyo, kutokana na walicho kishuhudia, Para na watu wake haooo, walishika njia kuelekea nyumbani kwa mzee Komba **** Wakati huo mzee Haule baada ya kuamka, aliona nivyema akienda nyumbani kwa mzee komba akamjulie hali, na kutafuta mwafaka juu ya mambo ya liyotokea, maana aliona kukaakimya ni sawa na kwamba amelidhika na kitendo cha mwanae, japo aliamini n akufahamu kuwa Martin siyo kijana mzuri wa tabia, wakufaha kukishi na mwanae, kweli mzee Haule alifika nyumbani kwa rafiki yake na kumkuta mzee Komba na mwanae wakiwa wamekaa na wageni wachache wakinywa pombe, maana wengine walisha anza kuwasafilisha kurudi makwao, kabla haja kaa mzee Haule alijikuta akikaribisha na matusi mazito toka kwa Martin, licha ya kuwa ni mtoto wa rafiki yake, alie ishinao kiiurafiki toka kijana huyu akiwa mtoto mdogo, pia ilikuwa awe mkwe wake, kiukweli yalikuwa ni matusi ambayo siwezi kuya andika, Martin alishusha matusi mazito, huku mzee Komba akishuhudia, na wala akuongea chochote cha kumzuwia mwanae, zaidi ya kutabasamu akishangilia anachokifanya mwanae Martin, kiukweri alimtukana sana, kiasi ambacho ilikuwa ni kashfa kubwa kwa mzee Haule, ata wale wageni walipo jaribu kumzuwia, walisikia amri toka kwa mzee Komba “kama kuna anaye ungana na huyu mzee, naomba atoke kwangu haraka“ hapo wageni waka nywea, na kuwa pole, akuna alie taka kukosa bia za bure, mzee Haule akiwa anakumbuka maneno ya mke wake, aligeuka na kuondoka zake kwa unyonge wa hali ya juu, machozi yakimlenga, alipishana na kijana mmoja mwenye kipara na ndevu nyingi, alie shuka toka kwenye taxi, lililosimama hapo nyumbani kwa rafiki yake Komba mabasi, kisha akamshuhudia yule kijana akiingia ndani kwa mzee komba,  mwonekano wa kijana yule ulimpa mashaka lakini akumjari sana akaingia ndani ya gari lake na kuondoka zake, wakati anaondoka akatazama kwenye lile taxi, akaona kuna watu ndani ya lile gari huku kwaharaka sana akiitambua sura ya kijana mmoja ambae aliwai kumkaba siku moja jioni nje ya ofisi ya Malaika, akaokolewa na kijana amba akuwa anamfahamu, hapo mzee Haule akahisi kuna mchezo mchafu Rafiki yake anataka kuucheza ****** Mama Malaika akiwa na wanae aliongea nao mengi sana, kiasi kwamba alijikuta akiona kama vile, Malaika na Edgar, wapo kwenye mausiano alali, waliongea mengi sana kwa muda mrefu, mpaka ilipo timia saa saba mchana aka waacha wakina Malaika, akiwakabidhi shilingi laki mbili za matumizi, na kupanda gari lake na kuondoka zake, akiwahacha wakina Malaika wakaelekea mtoni kuogelea, nayeye akarudi nyumbani, akitambua kuwa mwanae hakuwa tena bikila, maana siyo kwa kunogewa kukaa na mwanaume kiasi kile, nyumbani nako alimkuta mme wake akiwa anafakamia pombe vibaya sana, huku machozi ya kimtoka, muda wote mzee huyu, alilalamika kuwa toka azaliwe ajawai kutukanwa, matusi mazito kama yale, “leo hii natukanwa na mtoto mdogo kama Martin” alizidi kulalamika mzee Haule, Mama Malaika alipata kazi ya alimtuliza mume wake, na kumwambia asiwe na wasi wasi, Malaika yupo salama, tena mama Malaika akamdanganya mume wake kuwa, Malaika alikuja ofisini, amemwambia kuwa muda wowote atakuja nyumbani, wasiwe na wasiwasi wowote, Hapo mzee Haule akatulia kidogo, uso wake ukikunjuka kwa tabasamu la matumaini, akagugumia pombe iliyokuwa kwenye grasi “ebu mpatie dada pesa millioni mbili yao, ampelee mshenga awarudishie pesa zao, na ukimwona tena mwanangu mwambie arudi nyumbani” mzee Haule alimwagiza mke wake, ambae alikuwa anakaa na kukamata chupa ya bia, mda wote shangazi Sonia alikuwa amejibanza jikoni akiwasikiliza,  alipo waona wame maliza akarudi zakee kwenye chumba cha nje na kujifungia, nitaujuwa tu ukweli” ***** Mzee Komba mabasi alipewa riport kama wale vijana walivyo shuhudia kule seed farm, Martin akiwa pembeni akisikia yote “nilijuwa kuwa yule mama atakuwa anausika, maana alitokea kumchukia Martin bila sababu” aliongea mzee komba kwasauti yakilevi, wote kwa pamoja na Para walipanga mida ya kuvamia nyumbani kwa Edgar, kisha wale vijana waka ondoka zao, ****** Jastin akiwa anaendelea na biashara, akaja mwenzie ambae anauza nguo wakawa wanapiga story,  ni baada ya wateja kuwa wamepungua, waliongea kidogo ndipo jamaa akakumbuka jambo “hoya! hivi yule demu aliekuja hapa asubuhi kumwulizia Edgar una mfahamu?” japo Jastin alisha sahau, lakini akakumbuka mala moja “yule aliesema ana fwata viatu vya mtoto?, Simjuwi” alisema Jastin “alisema ana fwata vitu vya mtoto kivipi?” aliuliza yule mwenzie kwa mshangao “alisema ni vya shule si unajuwa kesho j’tatu, hivyo akasema nimwelekeze nyumbani kwa Edgar akamwone” alijibu Jastin “mh! Jastin ebu sububiri kwanza, unamjuwa vizuri yule dada?” aliuliza yule yule jamaa, akionyesha kutilia mashaka ujio wa yule dada wa asubuhi “Hapana, kwani vipi” hapo Jastin alielezewa ukweli kuhusu yule mschana, kuwa ni mtu hatari sana, ujiusisha na mipango ya ujambazi na wizi, ata makundi yake ni mabaya sana, yule jamaa akaendelea kumweleza Jastin kuwa yule dada akuwa na mtoto, wala mdogo wa kumnunulia viatu vya kuvaa shuleni, hivyo pengine kuna mchongo unapangwa juu ya Edgar, au kwenda kumwibia rafiki yao, hapo Jastin akapata picha kamili, kuna nini kinaendelea, ilikuwa saa tisa jioni akaamua kufunga biashara, ili awai akamjulishe Edgar lile jambo,**** naam mida hiyo hiyo Sophia Mapunda ndio alikuwa anashuka kwenye basi, katika stend ya magengeni, iliyopo karibu kabisa na mtaa wa seed farm, akitokea namabengo kijijini  kwao, alikokwenda kumtengeneza Edgar, ii amrudie mala moja, Sophia akiwa ame pewa dawa na marti ilitakiwa aende akaweke dawa nyumbani kwa edgar, mida ya usiku, kwakuwa ilikuwa ni mapema sana, Sophia aka tafuta sehemu yenye kimvuri akakaa, ilikusubiri giza liingie aende kwa Edgar akafanye alichoagizwa na mganga, ilikumrudisha mpenzi wake, muda wote huo akujuwa kilichotokea wakati hayupo, Sophia akiwa amekaa hapo kwa muda mrefu kidogo, alimwona Jastin akipita mbio kuelekea mtaa wakina Edgar, **** Jastin alienda moja kwa moja mpaka kwa Edgar, akawakuta ndio kwanza wanatoka mtoni kuvua samaki na kuogelea, waka washa moto na kuwaweka samaki juu yake, kisha wakamwacha jastin pale nje na wao wakaenda kuoga, baada ya nusu saa walitoka, wakajiunga na Jastin kuchoma na kubanika samaki, hapo Jastin akamsimulia Edgar, juu ya mwanamke anayedai alimwagiza viatu vya mtoto vya shule, ukweli Edgar akuwa na maagizo kama hayo, hivyo alijuwa kuwa kuna hatari inamjia, je? ninani alie mtuma, labda kama wazazi w malaika wanaweka mgeto, isinge wezekana wamtume mtu sababu mama yake Malaika, anapajuwa pale nyumbani, na mzee Haule amesha tulia, kama alivyo waambia mama yake malaika, zaidi ya hapo ni upande wa mzee komba mabasi ndio watakuwa, walio suka mchezo?, vijana wale watatu waliongea sana, wakijadiriana juu ya swala lile, kuna muda mama Malaika alipiga simu na kuwasimulia kilichomtokea baba yake Malaika, pia akawaambia kuwa mshenga amekabidhiwa fedha amerudisha kwa kina Martin, walipo maliza kuongea na mama malaika, baadae kidogo, mzee Mbogo alifika akiwa na mke wake yani mama Edgar na Prosper, nao walikaa kwa muda kidogo, huku baba yake Edgar akisoggea pembeni na Edgar wakiongea atima ya Edgar kuishi na Malaika kwa kujificha, Edgar akamweleza baba yake kuwa mausiano yake na Malaika ata mama yake Malaika anayajuwa, hivyo anauwakika haya mambo yakipoa itakuwa lahisi kwake kufanya taratibu za kwenda kupeleka barua ya posa, nimaneno ambayo mzee Mbogo aliyakubari, lakini akatoa ushauri kwa mwanae, “kumbuka hakuna mwanaume anae kubari kunyang’anywa tonge mdomoni kilahisi, kwa hiyo tambua kuwa hupo vitani” baada ya story nyingi sana mwisho wakaaga, kisha wakaondoka zao, Jastin alisema bado anapiga story  kwamba ataondoka baadae **** Mshenga mzee Mbawala alifika kwakina Martin, akawakuta wakiendelea na pombe akawakabidhi fedha zao kisha akaondoka, maana alishawachukia kwa tabia waliyo ionyesha ya kumtukana mzee Haule, mzee Komba alizishika zile fedha, huku akiwa ameachia tabasamu la kilevi kisha akamwambia mwanae kwa sauti ya chini “hii fedha ndo itawalipa wale vijana, baada ya kuwafundisha adabu awa wajinga wanao chezea hakili za watu” kisha wakacheka kidogo, lakini “baba, akikisha awamfanyi chochote Malaika mpaka ni mfanyie kile anacho jivunia, ndipo mambo mengine yaendelee” aliongea Martin kwa msisitizo***** baada ya kuongea kwa muda mrefu, pale nyumbani kwa kina Edgar, atimae saa mbili usiku Jastin aliaga tayari kuondoka, Edgar na Malaika wakamsindikiza, lengo likiwa na wao wakatembee kidogo baada ya kukaa sana nyumbani siku nzima, kumbe maeneo hayo, Sophia alikuwa amejibanza sehemu, ndani ya kichaka komoja, karibu na nyumba ya kina Edgar, akitafuta namna ya kwenda kufukia dawa yake mlangoni kwa kina Edgar, ili Edgar atakapo pita juu yake, aanze kumpenda zaidi ya alivyo kuwa akimpenda mwanzo, Baada ya kukaa kwa muda pale mafichoni akijadiri namna ya kukamailisha maagizo ya mganga wake, Sophia akawaona Edgar na Jastin wakitoka pamoja na Malaika wakija upande alipo yeye, aka jificha zaidi, huku wivu ukazidi kumtafuana “ina maana huyu mwanamke ameshaona kamchezo, mpaka ananogewa namna hii, tena amevaa nguo za Edgar, inamaana analala hapa hapa” aliwaza Sophia akijibaza akuwasubili wapiti, ili aende kufanya yake, walipo pita akawangoja waende mbari kidogo, kisha akatoka pale mafichoni na kuifwata nyumba ya kina Edgar, “siunajifanya bingwa la kuchukuwa wanaume wawatu, sasa ngoja uone anavyo kutimua” alijiseme Sophia huku akitembea kwa tahadhari kubwa akiufwata mlango wauingilia ndani kwa kina Edgar, ***** mida hiyo hiyo, Para na wenzake walikuwa wamesha paki gari lao, mbari kidogo toka ilipo nyumba ya Edgar, walikua wakitembe kwa mwendo wa haraka kuelekea kwa kina Edgar wakipitia kwenye chochoro na vichaka, isiwe lahisi wao kuonekana, Wale vijana watatu wakiongozwa na Para, walipo ikaribia nyumba ya kina Edgar, walimwona mschana mmoja akielekea mlangoni, wakizani anainia ndani, pasipo kuiona sura yake, kutokana na taa afifu zilizotumika kipindi kile, wakaona haina sababu ya kuchelewa, bola wamuwai kabla ajaingia ndani, kitendo bila kuchelewa, wakijuwa kuwa ndie Malaika, para na wenzake moja kwamoja waka mvamia na kumkamata, huku mala moja wakamchomeka kitambaa mdomoni ili asipige kelele, kisha waka mchoma sindano ya usingizi, maeneo ya shingoni, iliyo anza kumlegeza mda hule hule alafu wakambeba na kutokomea nae gizani, ndani ya vichaka, ni  baada ya kuona kuwa mle ndani ya nyumba, akukuwa na dalili ya kuwepo mtu mwingine, itaendelea ...... kwa story kari zaidi like page yetu ya Hadithi ZA MBOGO EDGAR





from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2GuRvbS

No comments:

Post a Comment