Thursday, January 30, 2020
Nawashwa Chini 15
SIMULIZI Nawashwa UKU
SEHEMU - 15
TULIPOISHIA.
tuliishia pale ambapo boss antony akitoka nje anakimbia huku akituacha vichwani tukiwa na maswali kibao kuhusu zile damu zilizotapakaa kifuani mwake haikupita muda tuliona kwa chini nje ya mlango wa chumba cha boss lady ikijivuta mikono iliokuwa imelowa damu,
#SONGA___NAYO
Mioyo ililipuka mtetemo ulitukumba kwa pamoja tukashindwa kuzikanyaga hatua za haraka kuusogelea mlango, jackrine na maria wao walikuwa wamefumba midomo kwa mikono yao huku macho yao yote wakiwa wameikodolea ile mikono jackrine alishindwa kuvumilia taratibu alianza kuangua kilio huku maria nae akimsapoti jackrine wote walianza kulia, kidume niliukaza moyo kisha nikaanza kujisogeza taratibu huku nayo mikono ile ikizidi kujitoa ndani na umbo kichwa kikaanza kujitokeza kwa nje, tulifika kwa pamoja na kumkuta boss susan akiwa katika hari mahututi huku damu nyingi zikimvuja tumboni na hapo ndio tafsiri ya kile kitu kilichokuwa kimefungwa kwenye kitambaa na boss antony ndio ilikuja kwani alipofika ndani alimkita na kisu kile mara mbili kisha mara ya pili alikiacha tumboni kikiendelea kumpa maumivu boss lady susan nae antony kukimbia, nilikinyanyua kichwa cha boss lady susan na kukilaza miguuni mwangu huku kichwa changu kikiwa kimechanganyikiwa "JACKRINE MUITE MORINE HARAKA FANYA HARAKA JACKRINE MAMA ANAKUFA" niliongea kwa kutetemeka huku nisiamini kile ninachokiona pale "MARIA MUITE MLINZI HARAKA AJE TUSAIDIZANE KUMBEBA TUMWAHISHE HOSPITAL" nilimtuma maria aende nje akamuite mlinzi aje atupe msaada wa kumbeba boss lady susan tumuwahishe hospital..
nko!! nkooo!! NKOOOO!!!! upande wa pili mlango wa morine ulipigwa kwa nguvu kumshtua lakini mda huo morine alikuwa ameweka earphone masikioni akisikiliza mziki kwa sauti kubwa wala hakuwa na habari kabisa ndio kwanza alizidi kutingisha kichwa kwa utamu wa song.. lakini jackrine nae hakufa moyo ndio alizidi kuupiga kwa nguvu huku akiitaa "morineeeeee morineeee mama anakufa morine pleaaase amkaaaaa!!!" jackrine alipiga sana mlango huku akilia, kwa mbari sauti zilianza kupenya na morine alihisi kunashida kwani gafla tu alijikuta moyo wake ukipata waswasi na mapigo ya moyo yakimuenda kasi alichomoa headphone haraka nakuzitupa hapo kitandani huku akitamka neno "mama" alifungua mlango haraka anataka kutoka anamkuta jackrine akiwa amekaa chini pembezoni mwa mlango kwani alipiga mlango mpaka akachoka akahisi huenda morine hakuwemo ndani "we jackrine kuna shida gani??" morine aliuliza huku akimnyanyua jackrine, jackrine alizidi kulia tu alishindwa hata aanzie wapi kumwambia morine akibaki kusema "mama morine msaidie mama" jackrine alitia huruma maskini "sa jackrine nimsaidie mama siuseme mama amekuwaje??" morine bado aliendelea kuuliza "WE JACKRINE ONGEA BASI" bado morine alizidi kufoka, Bila neno lolote jackrine alimshika mkono morine nakumpeleka sehemu ambayo mama yao yupo lakini hawakumkuta jeff wala maria zaidi walichoambulia kuona ni zile alama za dumu za viganja vya boss susan na zike zilizokuwa zikivuja wakati jeff amembeba, morine baada ya kuona tu damu alianza kuangua mwano, lakini kidogo maria aliingia ndani nakuwakuta wakiwa wamesimama pale mlangoni "Jamani mnasubiliwa nyie tumuwahishe hospitali" maria alisema mara moja jackrine aliingia chumbani mwa mama yao nakuichukua simu ya mama ake kisha wakapanda wote na safari nikuelekea hospitari ndogo ya mawenzi hospital ili apewe huduma ya kwanza,
nilijitahidi kuiweka mikono yangu kwenye sehemu ya mwanzo ambayo inaonekana ndio ilioanza kuchomwa kisu ili kuidhibiti damu isiendelee kuvuja kwa wingi na isitoshe kisu kile kilikitw sehemu mbaya sana, ni mwendo wa nusu saa mpaka kufika mawenzi tulibahatika kufika na kumkuta nesi mmoja aliekuwa zamu usiku ule alitupokea bila maswali ya pf3 alimuingiza kwenye chumba cha oparation kisha haraka aliitisha usaadizi kutoka kwa daktari mwingine aliekua nae zamu siku hiyo tuliona daktari akiingia chumba kile haraka na ilionekana taa nyekundu kisha kazi ikanza, tulibaki kwenye viti vya koridoni tukisali na kumuombea mungu boss susan apone licha ya kuwa tulijua kwa ile hari tuliomfikisha nayo boss susan sio wakupona viti vilikuwa havikaliki kila mtu alikuwa juu juu kama tai hakuna aliefurahia kukaa "nesi vipi hali ya mgonjwa" nilimdaka nesi mmoja alieonekana kuwa spidi akitoka chumbani mule nesi hakunijibu zaidi aliingia haraka nakuyarudishia mapazia ya mlangoni ili asiweze mtu kuchungulia ndani kwa usalama wake,
simu za kuwataarifu ndugu na jamaa wa karibu na boss susan zilitawala tulomtaarifu kila mtu aliekuwa karibu na boss susan na kweli zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani jopo kubwa la watu wengine wafanyakazi wake na hata majirani zake baadhi walifika kwa kuwa boss susan alikuwa ni kipenzi cha watu na alikuwa na moyo wa kujitolea sana, tulijazana koridoni tukiendelea kusubiri majibu ya waganga walikuwa ndani ya chumba kile, tulikaa sana sana, lakini kidogo mlango ulifunguka wa chumba cha oparation kila mtu alikuwa antation kujua nini kilichojiri, niliamka haraka kwenye benchi na kumuwahi doctor "doctor vip mgonjwa wetu anaendeleaje??" kila mtu aliuliza swali lile lile, doctor alitikisa kichwa kisha akasema "tumejitahidi sana kuyaokoa maisha yake lakini mlichelewa kumleta damu nyingi zimepotea...!!" doctor alisita kwanza kusema alikaa kimya kiasi kisha akafungua kinywa chake nakusema "nasikitika kuwaambia kuwa amefariki, hatupo nae tena duniani" "whaaaaaaat????!!!" niling'aka kisha nikashuka chini nakuangulia kilio,
msiba mkubwa masikini kwenye familia ya boss susan, kwa uthibitisho wa daktari boss lady susan hatupo nae tena, ameshatangulia mbele ya haki
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2u5G9Zp
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment