Monday, January 27, 2020
BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA THELASINI NA MOJA (MWISHO)
ILIPOISHIA SEHEMU YA SELASINI : “lakini shemeji hukupaswa kumwambia mama martin” aliongea mzee Komba akimsogelea mama Malaika, akakutana na kofi nzito la usoni lililo mfanya aone nyota, akapepesuka na kutaka kumdondokea, Malaika akakutana na kofi jingine lililo m’badilishia uelekeo na kwenda kujigonga kwenye meza ambayo ilimchana paji la uso, Martin alishuhudia yote hasiweze kumteta baba yake, wakati huo wakina Para wakiwa wame lala kwenye sakafu awajiwezi, dada jambazi alipiga mahesabu ya haraka ya kukimbilia nje maana mlango ulikuwa wazi, akahesabu kimoyo moyo, “ moja...mbili.... tatu...”, endelea..........
Hapo dada jamabazi Quen akachomoka mbio za maana kuufata mlango, lakini alichelewa, sababu muda huo huo, magari ya polisi yalisimama nje, yakiongozana na gari la baba yake Malaika ambalo alipanda Jastin rafik yake Edgar, “yule dada ni jambazi” alipiga kelele Jastin maana almtambua mala moja dada jambazi, hapo kitendo bila kuchelewa akachooka polisi mmoja na kumdhibitimwanamke huyu, kwa kumzowa mtama mmoja mkali sana, akiangukia mkono wake hule hule alio vunjwa na Edgar mda mfupi uliopita, na bado maumivu makali ya mkoni alikuwa ya membana, dada jambazi akatulia pale pale chini, sekunde chache baadae polisi waliizunguka nyumba na wengine wakiingia ndani, nakuwakuta wakina Para wakiwa ndio wana lejewa na fahamu, pia yule mwenzao bado anavuja damu, sehemu aliyo chomwa kisu na mwenzie, huku maumivu makali yakiwa yame mshika, Martin na baba yake, nao walikuwa wakiugulia maumivu, baba Malaika naye aliingia ndani akifwatana na Jastin kuja kuwatambua waalifu, kwanza alikumbatiana na familia yake yani mke wake, kisha mwanae, ambae alikuwa ajamwona kwa siku tatu, alipo maliza akaanza mgeukia kijana ambae sasa alikuwa amesimama karibu na Jastin, akamtambua ndie alie ondoka na Malaika, kanisani, lakini leo ilimjia kumbukumbu ya kukutana mala ya kwanza na kijana huyu, ni siku ambayo aliokolewa kutoka kwenye mikono ya majambazi, akachomoka mzee Haule na kumkumbatia Edgar “kijana leo ndiyo nime kukumbuka vizuri, kumbe ndiyo wewe, haaa! siamini macho yangu, kumbe ulikuwa mkwe wangu bwana” aliongea kwa sauti mzee Haule, kihasi cha watu wote kushangaa mlendani, mzee haule aliwasimulia kilicho waikumtokea siku ile jioni alipo vamiwa na majambazi, na kusaidiwa na Edgar, pia mzee Haule aliwa tambua wale vijana wa para kuwa ndiowalio mshambulia sikuile jioni, wakitaka kumpola fedha, akasaidiwa na Edgar, wakati wote mzee Komba alimtazama mzee Haule kwa macho ya huruma, usoni akichuruzika damu, alipoona mzee Haule, aonyeshi dalili ya kumuonea huruma, akaona bora, ajarubu kuongea nae, “mzee mwenzangu naomba tuyaongee kabla hayaja fika mbali” kauri iliyo mtia hasira sana mama Malaika “tulisha kuomba tuongee matokeo yake ulimwacha mwanao amtukane mume wangu, huku ukishangalia, na kumuunga mkono” alisema mama yake Malaika, “shemeji ilikuwa ni hasira tu, naomba tuyaongee tumetoka mbali jamani” alizidi kubebembeleza mzee Komba, “kaka sina namna, nakuomba kubari kubari matokeo,” alisema mzee Haule akimshika mkono mke wake na kutoka naye nje akifwatiwa na Edgar na Malaika nao wameshikana mikono pia, huku sura zao ziki tawaliwa na tabasamu , wakiamini mpaka hapo penzi lao limesha pata Baraka za wazazi wao, Dakika kumi mbele, polisi walikuwa wamesha wa chukuwa waharifu wote sita yani mzee Komba na Martin, Para na vijana wake wawili na dada jambazi, wali wajaza nyuma ya gari la Police Toyota pick up, safari ya kituoni ikaanza, ***** Mzee Komba, Martin na wakina Para walifunguliwa mashtaka, ya kujaribu kuteka nyala, walikaa mahabusu kwa miezi sita na hukumu yao ikatoka, Martn na baba yake, walifungwa miaka kumi na tano jela, Para na wenzake waliunganishwa na makosa ya siku za nyuma, waka fungwa miaka ishirini jela, Kwaupande wa Sofia alirudi kijijini kwao ambako anaishi mpaka sasa, sawa na shangazi yake Malaika yani Sonia, ambae licha ya kuomba radhi, kwa kaka yake na wifi yake na Malaika, lakini alifukuzwa na kurudi kijijini, na sasa ni mrevi mbwa wa pombe za kienyeji, huku walevi wenzake wakijibebea kila alipo lewa na kuangusha gari, mama Martin, alipooza baadhi ya viungo vyake vya mwili, baada ya kupatwa na mstuko siku ya hukumu, ya mumewake na mwanae Martin, pia ameshindwa kusimamia kampuni yao ya mabasi, na kupelekea kampuni kufa kabisa, Edgar na Malaika walifunga ndoa kanisani, na sasa wanamiliki biashara zao kubwa za maduka ya viatu vya mitumba na vya kawaida pia wanauza nguo za kila aina, na mwaka mmoja baadae walipata mtoto mmoja wakiume, wanaishi maisha mazuri yenye furaha na amani katika nyumba yao, ni ileile ya seed farm waliyo kabidhiwa lasmi na mzee Mbogo, ambayo sasa wameikalabati na kufanana na uzunguni,
HUO NDIYO MWISHO WA STORY YETU, YA MALAIKA SASA KAA MKAO WAKULA UISOMA STORY NYINGINE YA MREMBO KIPOFU, KWA MAONI NA USHAURI KARIBU IN BOX AU COMMENT KUTOA MAONI YAKO ASANTENI KWA KUIFUATILA MWANZO MPAKA MWISHO, KWA STORY NYIGINE, LIKE PAGE YETU YA Hadithi ZA MBOGO EDGAR
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2RWOC94
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment