Monday, January 27, 2020
BIBI HARUSI MTARAJIWA MALAIKA SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU : “ni mimi mwanangu tutaongea mengi siku nyingine, tumekuja kuwaletea mchele, mala moja” aliongea mama Edgar akizidi kumshangaza Malaika, ambae alianza kupatwa na hofu ya kufumaniwa na wazazi wake, akiamini huy mama amekuja watu wengine pale, “Asante kwa mchele mama, sasa umejuwaje kama nipo huku” aliuliza Malaika akipepesa macho huku na huku, kuona kama kuna watu wengine wanakuja, ENDELEA.......
“Mwanangu mimi ni mama yake Edgar” liongea mama Edgar, akijitaidi kujizuwiahali yake ya ulevi hisionekane mbele ya Malaika, “Kweli mama, inamaana hii suit aliyoivaa ndo ile uliyo sema ya mwanao?” aliuliza Malaika kwa mshangao, “aswaaaa na mwanangu mwenyewe ni huyu Edgar na huyu ndio mzee Mbogo baba yake” alijibu mama Edgar na Malaika aliruka ruka kwa shangwe, utazani amepata majibu mazuri ya mtihani, akiwahacha wanafamilia wakimshangaa, “Kweli mungu mkubwa, yani mama uwezi amini, siku tuliyo kutana, ndiyo siku niliyo kutana na Eddy” alisema Malaika kwa sauti iliyojaa furaha na shangwe, za hali ya juu, basi waliongea mengi sana, huku mzee Mbogo na Prosper wakiwa kimya kabisa, wakisikiliza mtu na mkwe wake, Malaika akawakaribisha ndani, lakini wakakataa wakidai wao sio wakaaji sana, hapo Prosper akaingiza mchele ndani, kisha akarudi tena nje, baba aka aga, akiahidi kuwatembelea kesho,“na wewe shemeji kesho uje na baba” Malaika alimwambia Prosper, “aya shemeji nitakuja kesho, tena akuna shule” alijibu Prosper “Msalimie huyo bwana akija” aliongea mzee Mbogo, akimaanisha kuwa Edgarv akirud asalimiwe, “sawa baba nita mwambia, lakini mnge msubiri kidogo, maana ameenda dukani mala moja” alisema Malaika “Hapana tutamwona kesho” Familia yamzee Mbogo iliingia kwenye gari na kuondoka zao, na kamailivyo kuwa mwanzo, walipishana kidogo na Edgar, ambae alimkuta Malaika akiwa amechangamka mala dufu, “Edgar, nikikuambia kitu uwezi amini” aliongea Malaika, akimrukia Edgar na kumkumbatia, huku akiwa amening’inia kwenye mwili wa mpenzi wake huo, “kitu gani?” aliuliza Edgar kwa shahuku, “mama, baba na Prosper, wameondoka sasa hivi” aliongea malaika na kumfanya Edgar shangae, “mh” Edgar aliguna kidogo akishangaa ujio wa watu hao aliotajiwa, “Hahaaa! hilo siyo jibu bwana, sema ndiyo au siyo kweli, ni juwe kama unaamini au hauamini” aliisema Malaika, akiwa anajishusha toka kwenye mwili wa Edgar, “Ndiyo kweli na amini” alijibu Edgar, kwa sauti iliyo ambatana na kiunyonge flani, maana alihisi kuwa, kufahamika kwa hii inshu mbele ya wazazi wake, ndio mwanzo wa kufichuka kwa siri ya uwepo qa Malaika maali pale, “kumbe mama yako namfahamu tokea zamani” aliongea Malaika akipokea vitu vyake toka kwa Edgar, “Malaika tafadhari, nisaidie kitu kimoja, ebu niambie kwa kunyooka, kimetokea nini” aliongea Edgar, ambae alionyesha wazi kuwa na wasi wasi, ukizingatia msimango ya kuiba bibi harusi toka kwa baba yake yalikuwa yana mngoja, hapo Malaika alimsimulia jinsi walivyo mtokea ghafla, pia akamwelezea jinsi alivyokutana na mama yake, siku ya kwanza pale dukani kwake, na mambo yaliyo tokea, pia maneno aliyo kuwa anapenda kumwambia, ata walipo kutana siku ya pili, “wamesema watakuja kesho tena” alimaliza Malaika akiwa amemsimulia Edgar, jinsi anavyo fahamiana na mama yake, “sasa wamejuwaje kama wewe hupo hapa na mimi?” aliuliza Edgar, akiwa na nia ya kuondoa wasi wasi, “Si nimekuambia kuwa nilimpa kadi ya mwaliko, maana yake walikuona pale kanisani, wakati unanitorosha” Malaika alimaliza simulizi yake, huku akianza kuchambua chupi tano alizo nunuliwa, za rangi tofauti tofauti, pia ndani ya mfuko kulikuwa na mfuko mwingine mdogo, Malaika akaufungua na kuchungulia ndani yake, kulikuw na bagia za kunde, “umejuwa je kama nazipenda san hizi bagia?” aliongea Malaika kwa sauti yenye furaha na shangwe, akaaziacha bagia pale nje chini ya mwembe, ambapo Edgar alikuwa amekaa akitafakari, yeye akaenda kuziweka ndani chupi zake, wakati anapita sebuleni , akitokea chumbani kuweka zile chupi, Jackline akakiona kikaratasi chini ya simu, kikiwa kime gandamizwa na simu yenyewe, Jackline akashikwa na wivu, maana alijuwa lazima itakuwa ni namba ya simu, ndizo zilizo andikwa kwenye kile kikaratasi, akakichukua na kukiangalia kile kikaratasi, Malaika akapigwa na butwaa, zilikuwa ni namba za simu za nyumbani kwao, na vikaratasi kama vile, uwa anavyo baba yake peke yake, na uwa anawagawia marafiki zake, au watu muimu tu kwenye biashara zake, “huyu ame kipataje?” aliwaza Malaika huku ana kibeba kile kikaratasi, kisha akatoka nacho nje “tafadhari Edgar unaweza kuniambia hiki kikaratasi umekitoa wapi?” aliongea Malaika akionyesha mshangao wa wasi wasi wenye tahadhari, “hacha wivu mke wangu, hicho kikaratasi alinipatia mzee mmoja hivi” alisema Edgar bila wasi wasi, “unamjuwa kwa jina huyo mzee”aliuliza Malaika akikikagua vizuri kile kikaratasi “mh kiukweli, jinaaaaa!” Edgar alijaribu kukumbuka, lakini akuweza “kwa kweli sikumbuki, lakini si lime andikwa hapo?” aliuiza Edgar, ambae kiukweli akuwa amesoma sana kile kikaratasi, maana akuzani kama ata mwitaji yule mzee, “jina hili, hapa Willson Haule , inamaana ukulisoma ili karatasi, toka huyo mzee alipo kupatia?” aliuliza Malaika, huku moyoni mwake akijiuliza baba yake na Edgar walikuwa wanafahamiana kivip, “kwakweli siku tazama sana, kwani sidhani kama nitampigia,” aliongea Edgar ambae alikuwa anaendelea kugeuza kuku na mahindi, “kwanini usi mpigie, kwani mligombana, na mna fahamiana toka lini na huyu mzee?” aliuliza Malaika kwa sauti, Edgar alimtazama Malaika, ambae alikuwa ameonyesha kupoa kidogo, kwa kunyongea, “ labda ni kusimulie kidogo ilivyo kuwa, ni kwamba, juzi jioni wakati nakutafuta, ni lipitia mitaa ya ofisini kwako ………..” Edgar alimsimulia Malaika kilichotokea siku ile aliyo msaidia mzee Haule pale mjini, “hoo! Kumbe ni wewe Edgar, ulimsaidia baba yangu” aliongea Malaika kwa sauti kubwa ya mshangao, “kumbe yule mzee ni baba yako” waliongeamengi sana, huku wakaendelea na shuguli zao, za mapishi, pia wakicheza michezo yao, ya kimapenzi, wakiwa wamesha sahau yaliyo tokea mchana, ****** Mida ya jioni, maeneo ya sokp kuu, Jastin alikuwa kijiweni akijiandaa kufunga bi hashara, leo akumwona kabisa rafiki yake Edgar na pia amesikia habari kuwa Malaika amekimbia kanisani, na kwamba, kuna kijana alimsaidia kutoroka kwa pikipiki kubwa, aliamua afunge biashara, ili ajaribu kwenda kwa Edgar akajuwe kinachoendelea, maana akilini mwake alijuwa fika kuwa Edgar atakuwa na Malaika seed farm, hivyo akafunga haraka sana, ili awai, maana giza lilianza kuingia, Jastin alipo maliza kufunga alienda kituo cha daladala, akapanda yale yanayoenda mahenge **** Ilisha timia saa mbili usiku nyumbani kwakina Malaika, watu walikuwa wakiendelea na vinywaji na chakula, wakiamini Malaika atarudi muda wowote, kasolo mama yake Malaika pekee, ndie alijuwa Malaika leo lazima atalala kwa Yule kijana, maana aliasha anza kupata uakika kuwa lazima Malaika alikuwa na mausiano na kijana huyu, toka siku zile ambazo Malaika alikuwa amenza kubadirika kitabia, mama Malaika akazidi kuumiza kichwa, akiwaza afanyeje, iliaweze kujuwa mwanae yupo wapi,
naam baada ya kuwaza kwa muda mrefu mama Malaika, akapatajibu, alitabasamu kidogo huku anainuka toka kweny kochi ***** Wakati huo huo nyumbani kwa mzee Komba, ilikuwa kama simanzi kwa mama yao, ambae muda wote alikuwa amejifungia chumbani akilia, huku akimlazimisha mume wake kuakikisha anafanya jambo litakalo wafanya familia yamzee Haule ijutie kitendo kile, mzee Komba alimwakikishia mke wake kuwa, kila kitu kimesha pangwa, wakati huo Martin na baba yake walikuwa wakiendelea kunywa pombe, wakisubiri matokeo ya kazi waliyompatia jamaa mmoja anayeitwa Para, ni jambazi maarufu sana mjini Songea kipindi hicho, alikuwa anawatumia vijana wake alio waamini kwenye kazi hii ya ujambazi, wa kutumia nguvu na silaha, mida hiyo Martine na baba yake walikuwa amelewa sana **** Sasa Mama Malaika alikuwa ameingia, chumbani kwa Malaika, akijaribu kuikagua simu, kwa bahati akakuta kikaratasi chenye namba za simu chini ya simu , akajaribu kupiga zile namba **** Wakati huo Edgar na Malaika walisha maliza kula chakula cha jioni, akuna aliewaza juu ya kilicho tokea leo hii, wao walikuwa wamekaa kwenye kochi, Malaika amelala juu ya Edgar, wakitazama filamu ya tarzan ya kihindi, ndipo simu ilipoanza kuita, mawazo ya wote wawili yalihisi simu inatoka kwa kina Edgar, hivyo moja kwamoja Malaika akainuka na kwenda kuipokea, kwani alijuwa wamesha fahamu uwepo wake pale nyumbani kwa Edgar, “hallow” alipokea Malaika kwa sauti ya uchangamfu, akijuwa kuwa mpigaji lazima atakuwa ni mama Edgar, sauti ya upande wa pili ilijibu kwa sauti ya chini na utulivu “hallow mwanangu hupo salama huko” hapo Malaika akaiisi tumbo likiunguruma kwa mstuko, “mh! mama umejuwaje hii namba, au amekupa …….” Malaika alistuka kusikia sauti ya mama yake akahisi pengine mama yake Edgar ameenda kutoa taharifa, kuwa yeye yupo na mwanae, Edgar alikuwa makini kufwatilia maongezi ya Malaika kwenye simu, akijuwa mambo yamesha aribika, maana macho ya Malaika yalikuwa yakimtazama Edgar, ya lionyesha mstuko wawazi kabisa “usiwe na wasiwasi mwanangu, na juwa kila kitu, ata huyo kijana ulie nae, nina mfahamu vizuri sana, naamani hupo sehemu salama, mimi na jinywea bia, najuwa hupo kwenye mikono salama kabisa, na hii namba nimeipata chumbani kwako chini ya simu” hapo Malaika akagundua kuwa mama yake alisha gundua mambo yake, kabla ata ya harusi, akageuka kumtazama Edgar hukuakitafakari, mama yake anamfahamu vipi mbona hakuwai kumwambia “mbona huku niambia kama unafahamu kuhusu mimi na Edgar, na vipi kuhusu baba anajuwa lolote?, kumbe Edgar anafahamiana na baba pia, ndiye alie msaidia siku alipo kutana na majambazi” hapo mama Malaika alipata kulijuwa jina la yule kijana kuwa anaitwa Edgar “Hapana baba yako ajuwi lolote, ila nime mtoa wasiwasi nime mwambia utarudi mda wowote, kwa sasa yupo sebuleni anakunywa pombe,” aliongea mama Malaika akionyesha kuwa kweli amekunywa bia nyingi sana, “Sawa naomba msije mkaenda polisi, mtatuweka kwenye matatizo” aliongea Malaika kwa sauti ya kubembeleza, “sawa, tutaongea kesho mwanangu, na kutakia usiku mwema msalimie Edgar, ila muwe makini maana umesha tengeneza uadui kwa mzee Komba” alitahadhalisha mama Malaika, “Sawa mama tena ata nyumbani hatutoki” Walimaliza maongezi yao kisha Malaika akarudi kwenye kochi “naomba ufafanuzi mama amekujuwaje” aliongea Malaika kwa sauti iliyo jaa utani, “hapa unapo niona nimejaribu kukumbuka toka nikiwa na miaka mitano, mapaka saa hizi tupo hapa, sikumbuki kumfahamu mama yako, atakama tuliwai kukutana kwa dakika moja, ninge kumbuka” alijibu Edgar akiwa na uakika kuwa, amjuwi mama yake Malaika “au mama ananichezea akili, ila kama anakufahamu lazima atajuwa namna yakututafuta” aliongea Malaika huku anajilaza kifuani kwa Edgar, “hivi anaweza kuja na polisi?”aliuliza Edgar “Hapana, kwa jinsi alivyo kusifia, pia alikuwa apendi niolewe na Martin, sema baba na shangazi ndio walio kuwa wanashupalia” wakati wakiendelea na maongezi mala mlango ukagongwa mioyo yao iklipuka waka tazamana Edgar akamwonyesha hishara Malaika akimbilie chumbani wakati Malaika akiinuka mlango ukagongwa mala ya pili safari hii, iliambatana na sauti, itendelea ......... kwa story kari zaidi like page yetu ya Hadithi ZA MBOGO EDGAR
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2RYqbs5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment