KITUMBUA CHA BUKU
SEHEMU YA KWANZA
SEHEMU YA KWANZA
Kijana Prosper alikuwa amejilaza kwenye mkeka, akipunga upepo wa na kufaidi kimvuri cha mti wa mwembe dodo mkubwa sana, uliopo pembeni ya kibanda kidogo cha bati,( full suit), ambao kwa kipindi hiki cha mwezi wa kumi na mbili, uwa unadosha sana maembe, hivyo kumfanya awe na tahadhari nyingi sana pale chini ya mwembe dodo, huku ana waza mambo mengi sana juu ya maisha yake ya sasa na ya baadae, “ukweli ujinga siyo kipaji, ujinga nitaaluma ambayo mtu ujivunza kwa juhudi kubwa sana” aliwaza Prosper au Pross kama wenzake walivyo penda kumwita, asa wakati yupo shule, “hakika usiyo yafanya utotoni utakuja kuya fanya ukubwani” aliendelea kuwaza Prosper, huku akitazama juu kwenye mti huu uliostawi na kuzaa maembe mengi sana, ukiwa ni mmoja kati ya miembe kadhaa iliyopo kwenye eneo ili la shamba kubwa sana, lenye mazao mengi sana, ikiwepo minazi ambayo ilikuwa nusu ya shamba, ndizi michungwa mipapai na matunda mengine, pamoja na viazi vitamu na mihogo ambayo Pross aliipanda mwenyewe nje na maataba wa mwenye shamba, yeye akiwa kama mlinzi na mfanyakazi wa shamba ili, ambae nikama aliuzwa au alikabidhiwa kwa mmiliki mpya wa shamba ili ambae ni bwana Shinyangwe, toka kwa mmiliki wa zamani wa shamba ili, alie linunua mwezi mmoja uliopita.
Huyu mmili mpya alikuwa ni bwana Vitus Kipanta, mzee wa miaka hamsini na nane, askari mstaafu wa Jeshi la ulinzi, alie staafu akiwa na cheo cha nyota tatu, ukweli bwana Vitus Kipanta alimkumbusha machungu makubwa sana Prosper, mwenye miaka 22, machungu ambayo yalisababishwa na aba yake ambae alikuwa ni askari mstaafu wa jeshi la polisi, ambae mala baada ya kustaafu, na kulipwa mafao yake akaondoka na kuwaacha wakina Pross, kwenye nyumba ya serikali, (quarters) za polisi maeneo ya Mivinjeni, kipindi Pross akiwa amebakiza miezi mtatu kumaliza kidato cha sita, na bahati mbaya au nzuri, Pross alikuwa anaishi na mama wa kambo, yani wa kufikia, kwahiyo mke alie telekezwa na bwana Feruz, siyo mama mzazi wa Pross,
Huyu mmili mpya alikuwa ni bwana Vitus Kipanta, mzee wa miaka hamsini na nane, askari mstaafu wa Jeshi la ulinzi, alie staafu akiwa na cheo cha nyota tatu, ukweli bwana Vitus Kipanta alimkumbusha machungu makubwa sana Prosper, mwenye miaka 22, machungu ambayo yalisababishwa na aba yake ambae alikuwa ni askari mstaafu wa jeshi la polisi, ambae mala baada ya kustaafu, na kulipwa mafao yake akaondoka na kuwaacha wakina Pross, kwenye nyumba ya serikali, (quarters) za polisi maeneo ya Mivinjeni, kipindi Pross akiwa amebakiza miezi mtatu kumaliza kidato cha sita, na bahati mbaya au nzuri, Pross alikuwa anaishi na mama wa kambo, yani wa kufikia, kwahiyo mke alie telekezwa na bwana Feruz, siyo mama mzazi wa Pross,
Na ukweli toka baba yao bwana wana Vitus Feruz aiache familia yake ya mke ambae na watoto watatu yani Pross ambae ndie mkubwa, na wadogo zake wawili aliochangia baba, yani watoto wa wili, wa mama huyu, alie mlea Pross, toka Pross akiwa na miaka kumi na tano, yani kidato cha pili, ambo ni wawili tu! mmoja akiwa wakike ambae alikuwa mdogo kabisa, na kwa sasa alikuwa darasa la sita, na kaka yake ambae sasa alikuwa kidato cha tatu, ukiachia watoto wa bwana Feruzi walio telekezwa, pia kulikuwa na mdogo wa mke wa bwana Feruzi, ambae wakina Pross umwita mama mdogo, huyu nae alikuwa na miezi michache hapa nyumbani kwa Feruzi, akitokea kijijini kwao Iringa.
Pross akiwa katika kumbukumbu ya machungu, anakumbuka kuwa baba yake ambae alimtoa kijijini kwa mama yake, alie wai kuwa mpenzi wake, na kumpatia ujauzito ambao alizaliwa yeye, kwa ahadi ya ndoa, iliyo potea, baada ya kukutana na mama huyu mwingine, Pross alikumbuka siku ambayo alikuwa likizo yake ya mwisho kabla ya kwenda kwenye mitihani, ambapo baba yao aliondoka nyumbani akisema anaenda kuangalia kama fedha zake zamafao zimeingia kwenye account yake, na kurudi siku ya pili mida ya saa sita mchana, akionekana wazi kuwa alikuwa amechoka kwa pombe na starehe, lakini Pross na wadogo zake, walifurahi sana, kumwona baba yao, wakijuwa kuwa, ata kuwa amekuja na mambo mazuri, lakini aikuwa hivyo maana baba na mama yao wakajifungia chumbani na kuanza kulumbana, hapo ndipo Pross ambae alikuwa ana umri wa miaka kumi na tisa, ambayo ilitosha kuelewa kinacho endelea, aka ng’amua mapema sana kuwa kulikuwa na ugomvi mkubwa sana, kati ya baba yake na mama yake wakambo, na akaja kuli thibitisha ilo, jioni ambapo baba yake aliondoka kama vile anaenda kutembea, na akurudi tena, ata wiki ilikatika, huku maisha yao yakianza kuwa magumu, maana awakuwa na kipato kingine zaidi ya kumtegemea baba yao, na walikuwa awakopesheki , sababu kila mwenye duka aliamini kuwa aadda ya kulipwa mafao yake bwana Feruzi, angeondoka muda wowote toka pale kwenye nyumba za Polisi, za Mivinjeni, na kupisha askari wengine katika nyumba ile, ya serikali, lakini mwokozi wao akawa mama mdogo, ambae alikuwa ana pewa ela na mwanaume mmoja ambae alikuwa ni askari pale line polisi, lakini pia alikuwa mume wa mtu.
Maisha yakazidi kuwa magumu kwa upande wa familia hii, huku wakimsikia mama yao akilalamika kuwa, kuna habari nyingi mtaani, kuwa baba yao anaonekana mitaa ya Kigamomboni huko Tuamoyo, akishinda na kura raha na mschana mmoja, ambae mwanzo mama yake akuwa anamjuwa, lakini japo akuwa na wasi wasi juu ya mama huyu wakambo ambae alimwonyesha upendo kama vile mwanae, ila Pross akaamua kwenda kigamboni kumtafuta baba yake, alitoka asubuhi na mapema, na kuanza kumsaka baba yake.
Kwa hakiri za kitoto, Pross alisaka kwenye mitaa akizunguka Tuamoyo nzima, mpaka uwanja wa swala kiiukia PCOL, na kufwata barabara ya mikadi, na alipoona ame kosea akarudi tena uwanja wa maputok akinyoosha mpaka karibu na kambi ya Jeshi, kisha akarudi tena Tuamoyo kwa kutumia chochoro za mitaa, huku akinunu amaji, na vitafunwa kama karanga, na vinginevyo, kiasi kwamba mpaka saa kumi jioni, Prosper alikuwa amejikuta maeneo ya CCM, ajuwi la kufanya na akuwa ata na nauri ya kurudia kwao Mivinjeni, “nitafanya nini” alijiuliza Pross, huku akitazama maduka na bar ndogo ndogo, zilizopo pembezoni mwa ukumbi wa CCM, ungesema anatazama kama ange mwona mtu ambae anaweza kuwa anamfahamu akamwombe nauri.
Kwahakika kama unge mwona Prosper kwa wakati huo, unge gundua mala moja kuwa kijana huyu alikuwa amechoka sana, kwa mwendo wa kutwa nzima, tena kwenye juwa kali, maana uso ulimpauka huyu kijana ambae urefu wake wa wastani, na mpata kidogo, alionekana kubonyea mgongo, kama vile anakibiongo, kwa jinsi alivyochoka, na miguu yake ambayo alikuwa amevaa viatu vya chini, vya mikanda, yani sendo, ilikuwa imechafuka vumi, kama ingekuwa kule kusini kwa wamwela, tungesema ametoka kucheza ngoma za wakati wa unyago.
Kijana akuwa na lakufanya, akaamua kuanza kutembea taratibu, kuelekea kivukoni, huku akiwaza atatoa wapi shilingi mia ya kuvukia, kwenye pantone, maana aliamini kitu ambacho akiwezi ni kuogelea tena kwa umbali mrefu kama ule wa kutoka kigamboni mpaka magogoni, lakini kama atafanikiwa kuvuka, anauwezo wa kutembea kwa mguu mpaka Mivinjeni, ata kama akifika kesho hiyo isinge sumbua, cha msingi ni kwamba avuke kwanza.
Bahati ilikuwa upande wa Prosper, nasema Bahati sababu alifanikisha lengo la safari yake, maana wakati Pross ana maliza kulivuka jengo la ukimbi wa CCM, akaiona bar moja ndogo, ambayo ilikuwa na watu wachache sana, na watu hao kwa mtazamo wa haraka walikuwa katika meza mbili, kama wateja, na ukiondoa wahudumu na mchoma chips, kulikuwa na mwanaume mmoja na wanawake sita, waliokaa kwenye meza mbili zilizo ungwa pamoja, na kuonekana kama meza moja ndefu, wakiwa wamevalia vinguo ambazo ziliwatamulisha kuwa ni wanawake wa aina gani, maana kama siyo fupi, basin i nyepesi na iliyo ana, na kuchora maungo yao.
Meza zile zilikuwa zime tapakaa vinywaji, navyo vikiwa ni pombe tupu, ambazo kwa haraka Pross akujuwa gharama ya pombe zile, lakini kwa mimi kama mwandishi na kwa maelezo ya Pross kichwa cha bei ya chini ilikuwa ni win flani ya box, iliyo kuwa inauzwa shilingi elfu saba kwa mwaka ule wa 2009, vingine vilionekana kuwa vya gharama ya juu zaidi, pamoja na sahani zilizo nona kwa vyakula tena akukuwa na nyama ya ng’ombe, ni ndizi choma kwa nyama ya kuku.
Mwanzo Prosper akumwona kwa sura yule mwanaume, sababu alikuwa amemgeuzia mgongo, kwa ukaaji wake, lakini aliweza kuziona sura za wanawake walio mzunguka, ambao walikuwa wana kunywa na kula, wakicheka kwa furaha, huku mmoja wa wachana wale, muda wote akimfanyia michezo ya kimahaba, bila kujari kuwa ilikuwa saa kumi jioni, na ile sehemu ni barabarani, ukweli Prosper alihisi kengere ya tahadhari ikigonga kichwani mwake asa baada ya kugundua kuwa wale waschana anao waona mbele yake anawafahamu, tena walikuwa wanatoka maeneo ya karibu na makazi ya askari wa jeshi la polisi, ni wadada flani ambao sifa zao siyo nzuri sana, pale mtaani, ni wadada ambao mala nyingi akiwa anarudi toka shule uwa anawaona kwenye vibar vya mtaani kwao wakiwa wanakunywa pombe na wanaume tofauti tofauti, sijuwi kwanini aliingiwa na wasi wasi mkuwa kwa kuwaona wale wanawake, lakini akapata wazo la kwenda kuwaomba wamsaidie nauri ya kufikia Mivinjeni, maana akuwa na njia nyingine, na aliamini kuwa uwepo wa wanawake wale ambao kwamwonekano siyo wanawake wa mchezo mchezo, ambao wakikutia mkononi, lazima uuze mpaka nguo ya ndani.
Prosper alipiga moyo konde na kusogea pale kwenye bar, “shikamo” alisalimia Prosper, mala baada ya kuifikia sehemu lengwa, wote saba wakamtazama Prosper ambae alikuwa amemkazia macho mmoja wa wanawake wale, lakini alishangaa kuona sura za wana wake awa zikibadirika toka kwenye vicheko na kukunja midomo kama vile wamemwona hasidi, au fisadi, “we! Pross, ume fwata nini huku?” alikuwa ni sauti ya kiume iliyo jaa mshangao wa kilevi, Prosper alie itambua ile sauti mala moja kuwa, akamtazama yule mzee, na alipo hakikisha kuwa ni baba yake kweli, kama alivyo isikia ile sauti yake, Pross akatabasamu,………
_________ITAENDELEA___________
NAFASI ZA KAZI ZILIZOTANGAZWA LEO ZISOME HAPA
WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2MNk7ka
No comments:
Post a Comment