Thursday, January 2, 2020

Mambo Tunayotakiwa kuwa nayo makini ktk uhusiano



UTULIVU katika mahusiano yako hautokei kama ajali. Ni suala la umakini, udhibiti na maarifa. Inabidi uwe makini katika kauli na matendo yako kama unataka mahusiano yako yawe katika mstari mnyoofu.
Inakupasa uwe na uwezo wa kujidhibiti dhidi ya tamaa na hasira zako ili kuyajengea mahusiano yako uzio madhubuti wa amani na furaha.

Ila pia unahitajika kuwa na maarifa ili kufanya mahusiano yako yawe ya amani na uchangamfu siko zote.
Watu wengi wameingia katika mahusiano kwa sababu ya kuwaona wakina fulani wana furaha katika maisha yao ya kimahusiano bila kuangalia chanzo cha hiyo furaha na amani yao.
Matokeo yake baada ya kuwa ndani ya kwa muda mfupi wamejikuta wakikinahi kuwa katika mahusiano na kuamua kutoka haraka huku wakilaumu kila kitu.
Kumbe kitu cha msingi ambacho walipaswa kukiangalia kwa umakini kabla hawajababaishwa na furaha ya wahusika, ni chanzo cha furaha yao. Kwanini watu hawa walikuwa na furaha?
 Je, ni kwa sababu ya sura na maumbile yao tu? kupendana pekee kunatosha kuwafanya watu kuwa na furaha katika mahusiano yao?
Majibu yanayotokana na maswali ya namna hii yangewajenga zaidi kabla ya kuingia katika mahusianao.Unayafahamu mambo ya kuwa makini nayo katika mahusiano yako na mwenzako?
Je, unafahamu kuwa mahusiano yanajengwa kutokana na mambo wanayofanyiana wahusika na yanabomoka pia kutokana na mambo wanayofanyiana?
Unafahamu ni mambo gani unayotakiwa kuwa nayo macho zaidi katika mahusiano yako? Kiujumla mambo unayotakiwa kuwa nayo makini yako mengi ila kutokana na ufinyu wa nafasi leo nataka tujadili mambo matatu tu.
1.  NAMNA UNAVYOONGEA NA MWENZAKO
HILI ni suala muhimu sana. Suala hili ndio linalompa tafsiri ya haraka juu ya namna unavyomchukulia na namna alivyo juu yako.
Katika kuongea na mwenzako ndipo unapotengeneza mtazamo wako juu yake. Kauli na sauti yako wakati unazungumza naye inaenda kutoa mirindimo katika masikio yake utakaotoa tafsiri juu ya thamani na umuhimu wake katika maisha yako.
Kupitia kauli na sauti yako ndipo mwenzako atapata hamasa ama ya kuwa karibu na wewe ama kuwa mbali na wewe.
      Wapo baadhi ya watu wanaolalamika kuwa waume  zao hawana muda wa kukaa na kuongea nao bila kujua kuwa kauli na sauti zao wakati wakizungumza zimekuwa miiba inayowakera na kuwaumiza wenzao.
 Kauli yako ni kitu cha msingi sana. Namna unavyoongea na mwenzako ni kitu kinachoweza kusababisha apende kuzungumza ama kujadili na wewe au aamue kukaa mbali na wewe.
2.  UNAVYOMTENDEA
MATENDO yako kwa mwenzako yako vipi? Matendo yako yanamfanya akujengee picha gani katika akili yake?
Matendo yako ni nguvu inayozima hisia hasi na fikra potofu zote juu yako. Mfano, mwenzako ameambiwa huna mapenzi naye, kwamba wewe unamtumia tu katika maisha yake.
Maneno ya namna hiyo huenda yakamchoma na kumuumiza sana ila nguvu ya hayo maneno kuzidi kuteka akili yake inategemea na matendo yako kwake.
Mfano kama anaambiwa humpendi ila kila siku anaona unavyohangaika kwa ajili ya kumfanya si tu awe na amani na furaha ila pia awe wa thamani na bora katika jamii.
Maneno yale ya wanafki hapo yatakuwa na nguvu?Matendo yako ni kama maji ya kuzima nguvu ya maneno ya wanafiki pamoja na hisia hasi juu yako.
 Hakikisha mbali na kuzungumza na mwenzako katika namna nzuri ya kufurahisha ila unamtendea mambo yatayomfanya hata akiwa peke yake akikufikiria abaki na tabasamu na amani katika nafsi yake.
3. USIKIVU WAKO JUU YAKE
MWENZAKO akiwa anaongea huwa unampa usikivu wako wote? Au akiwa anaongea nawe unakuwa ‘busy’ tu na simu ama na mambo mengine?
Nakuibia siri. Chanzo cha hisia nyingi hasi zinazozuka katika mahusiano ni pale mhusika anapohisi asikilizwi inavyopaswa wala kupewa heshima katika makatazo, maagizo ama mawazo yake.
Akiwa anaongea mpe heshima na thamani ya kumsikiliza ila pia kama kuna jambo linalomkera alikwambia uliache na ukaahidi kuliacha basi fanya hivyo maana ukiacha kufanya hivyo huenda akadhani humpi heshima na thamani anayostahili kitu kinachoweza kuleta shida kubwa baadaye katika mahusiano yenu.


  WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/35i7bJD

No comments:

Post a Comment