Thursday, January 2, 2020

Kuna Bahati ya kupendana ikitokea usiipoteze



KUNA Mara nyingi huwa ni vigumu sana kukutana na mtu ambaye utampenda sana, naye akupende kupitiliza. Ni nadra sana kukutana na mtu huyo duniani.
Mara nyingi hutokea mara moja, ni ngumu sana kutokea mara ya pili na ya tatu. Ukijaribu kuzungumza na watu wengi walioko kwenye ndoa, watakupa visa tofauti.
Kuna ambaye atakuambia, mpenzi wake wa mwanzo alimpenda sana, lakini kutokana na sababu mbalimbali, alijikuta ameoa au kuolewa na mtu mwingine kwa sababu ya uhitaji wa ndoa kwa wakati huo.
Yawezekana akawa anapata presha kutoka kwa ndugu, jamaa au marafiki. Anajikuta ameanzisha uhusiano na mtu mwingine na baadaye kufunga naye ndoa. Bahati mbaya sana, watu wa aina hii kwa namna moja au nyingine huwa wanapitia kipindi cha mat-eso kwe-nye mahu-siano yao mapya.
Yule aliyem-penda awali huwa anamku-mbuka, ana sababu zake za kumpenda. Ndugu zangu tukubali, tukatae, mara nyingi mwana-damu hukutana na mtu mmoja ambaye humpenda sana. Inapotokea mtu huyo amepishana naye na kushindwa kuoana naye ndiyo basi tena.
Ataingia kwenye uhusiano na mtu mwingine kama tu kutimiza wajibu kwamba naye awe na mtu, lakini kiwango cha kumpenda hakiwezi kuwa kama kile kilichokuwa awali. Ataishi naye, atazaa naye watoto, lakini upendo siyo ule wa asilimia mia moja.
Ndiyo maana leo mada yangu imejikita kwenye eneo hilo. Lazima tutambue thamani ya kupendana mara moja. Inapotokea umekutana na mtu mkapendana, hii ni bahati. Unatakiwa kuithamini mno na kuitunza maana wapo wengi ambao wanahangaika miaka nenda rudi hawaipati.
Wengi wamekuwa wepesi wa kutoijali hii bahati. Wanaichukulia poa kwa sababu ipo na matokeo yake baadaye ikipotea wanakuja kujuta. Wanajuta maana tayari mazingira yanakuwa hayaruhusu tena kurudi kwa yule aliyempenda.
Vuta picha kama unaishi na mtu ambaye unampenda halafu na yeye anakupenda kwa dhati ni nini kitakuwa kinaendelea kati yenu? Ni zaidi ya furaha maishani, mtastarehe vizuri kwa sababu kila mmoja atakuwa na amani na mwenzake. Asikudanganye mtu kwamba eti wanaopendana kwa dhati hawaoani au hawadumu, hizo ni imani tu!
Nikuambie wewe ndugu yangu unayesoma hapa leo, yawezekana upo kwenye wakati wa kuwa na mtu ambaye mnapenda, itumieni hiyo fursa na msiiache ipotee maana huko muendako kila mmoja akichukua njia yake, mtaikumbuka.
Kwa nini utengeneza mazingira ya kuja kujuta baadaye, wakati nafasi unayo ambayo ni sasa? Madhara ya kuingia kwenye ndoa na mtu ambaye hauna upendo naye kwa asimilia mia moja ni makubwa sana. Usipokuwa makini, matatizo ya usaliti ndipo yanaibuka.
Mnapokutana wawili ambao kweli mkijitathmini mnapendana kwa dhati, msifanye mzaha hata kidogo. Msiringiane. Mpeane! Tengenezeni maisha yenu vizuri na muweke mikakati haraka ya kwenda kwenye ndoa. Ishini mkijua kwamba, thamani ya kupendana kwenu mmeibeba ninyi wawili.
Shirikishaneni kwenye kufanya uamuzi sahihi na kwa wakati. Asiwepo mmoja wenu wa kumkatisha tamaa mwenzake maana akitokea tu ni hatari. Maisha ya mahusiano yana siri kubwa, kila mmoja ana historia na mapito yake hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa.
Tengenezeni mapito yenu, ishini kwa malengo ili muweze kufika mahali mjivunie mikakati yenu.
Kwa leo inatosha, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine. Instagram &Facebook: Erick Evarist, Twitter: ENangale.


  WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2Qn91Vr

No comments:

Post a Comment