Na Amiri kilagalila
Serikali wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe imekabidhi gari namba SM 12714 kwa ajili ya kubebea wagonjwa (ambulance) Zahanati ya Imalinyi iliyopo katika kijiji cha imalinyi kata ya imalinyi wilayani humo mkoani Njombe.
Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Antony Mahwata amesema kuwa gari hilo lililetwa kwenye kituo cha afya cha Imalinyi wakati kata hiyo haina kituo cha afya hivyo amemtaka mganga mkuu kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo kuhakikisha zahanati ya Imalinyi inapandishwa hadhi kuwa kituo cha afya kwa kukamilisha baadhi ya mahitaji.
“Sasa gari hiyo ilivyo kuja wakasema Imalinyi sio kituo cha afya nikawaambia kwa kuwa imeandikwa ipelekwe kwenye kituo cha afya na magari yanapelekwa kwenye vituo vya afya anzeni kabisa hiyo gari kuiandika ni kituo cha afya cha Imalinyi hata kama hakijawa ni kituo cha afya," amesema.
Aidha Mwenyekiti huyo amemuagiza Mkurugenzi,afisa utumishi na afisa usafirishaji wa halmashauri hiyo kufanya utaratibu wa kumuajiri dereva wa mda na atakayelipwa na serikali huku akitoka katika maeneo ya kata hiyo kwa kufuata mchakato wa kuanzia kwenye kamati
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2GSvS51
No comments:
Post a Comment