Wednesday, May 29, 2019

SIMPLE RULES OF LOVE



1.sio mahusiano yote yataishia kwenye ndoa,,baadhi ya mahusiano yao kwasababu fulani,mengine ni ya msimu na mengine hudumu mpaka ndoa,,hivyo kama mahusiano yako yamefeli usisikitike,,kulikuwa na sababu,tambua hilo na usonge mbele.
2.usipende kwa moyo wako wote,unavyopenda ondoka na akili yako pia,mpende mtu uliye nae lakini jipende na wewe pia,ujue mustakabali wako na muelekeo wa maisha yako,usiwekeze kila kitu kwa mtu mliyejuana nae ukubwani,kuwa muangalifu.
3.usivutiwe na mtu kisa pesa au uzuri wake;kama mtu huyo hakupendi na anazo sababu zake binafsi basi,,Uzuri wake au pesa zake haziwezi zikafanya mahusiano yadumu.
4.mapenzi pekee hayatoshi ila maelewano,heshima,kuendana,uvumilivu na ustahimilivu ndivyo vitakavyofanya kuwe na mahusiano au ndoa imara.
5.usijidanganye kuwa,inakubidi uwe na hisia za kumpenda mtu ndiyo umkubalie au uwe nae kwenye mahusiano,watu hufikiria wapo kwenye mahusiano yasiyofaa au ndoa isiyofaa kwasababu tu hawawapendi walio nao,wasichojua ni kwamba, mahusiano na ndoa ni maamuzi zaidi kuliko hisia.
Unapoamua kuwa na mtu hisia za mapenzi hufuata baadae,na hata unapomchukia mtu,hisia zako zitakufanya kila siku uyaone makosa ya mtu uliyempenda awali,
Kupenda ni maamuzi sio hisia pekee,,choose to love and the right feelings will follow.

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2XdsxV7

No comments:

Post a Comment