Tuesday, May 28, 2019

INASIKITISHA ATEKWA NA KUBAKWA NA WANAUME WANNE



DAR ES SALAAM: Unyama gani huu? Tukio baya limejiri jijini Dar likimhusisha mrembo mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Masenze.
Mrembo huyo ambaye jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili, anadaiwa kufanyiwa ukatili wa kutisha na watu wasiojulikana.
Mrembo huyo anadaiwa kutekwa kisha kubakwa kwa zamu na wanaume wanne kabla ya kuchomwa kisu sehemu za siri na kumsababishia majeraha na maumivu mazito.
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa juu ya tukio hilo la kutisha, baba wa mrembo huyo ambaye naye jina linahifadhiwa alisema kuwa alishangazwa na kusikitishwa mno na vijana waliofanya unyama huo kwa mtoto wake.
Alisema kuwa siku ya tukio hilo alirejea kutoka kazini majira ya saa 2:00 usiku ndipo akasikia watu wakisema kwa nje kuwa binti yake anatokwa na damu nyingi na hawezi kutembea.
“Niliposikia hivyo, kwa kweli nilijiuliza atakuwa amevamiwa na wahuni au kuna kitu gani kimempata? Nilichanganyikiwa sana, wakati ninatafakari niliona baadhi ya jirani zangu wamembeba wanamleta ndani nguo zote zikiwa zimeloa damu,” alisema baba huyo.
Akiendelea kuzungumza, baba huyo alisema kuwa baada ya kumuingiza ndani mwili wake wote ulisisimka baada ya kumuona mwanaye huyo akiwa analia kwa uchungu kutokana na maumivu makali huku damu zikimchuruzika.
Alisema kuwa mama ake alimpokea binti yake huyo na baada ya kumchunguza alizimia baada ya kuona mwanaye ameumizwa vibaya mno kwa kuchomwa kisu sehemu za siri.
“Jamani inauma sana… Baada ya kumuangalia mwanangu, kwa kweli niligundua huku duniani kuna watu wanyama sana maana walichomfanya mwanangu hakiwezi kuelezeka kabisa na huwezi kukubali kama ni binadamu wenzake wamefanya hivyo,” alisema baba huyo.
Baba huyo aliendelea kusimulia kuwa baada ya mtoto wake kuletwa katika hali hiyo, alimpeleka moja kwa moja mpaka katika Hospitali ya Mwananyamala ambapo walianza kumpatia matibabu na angalau sasa hivi anaweza hata kutembea mwenyewe.
“Namshukuru sana Mungu. Baada ya kumpeleka Mwananyamala wakaanza kumpa matibabu ya haraka na kulazwa ambapo sasa hivi angalau kidogo anaweza kutembea,” alisema baba huyo.
Juzi Jumatano, Gazeti la Ijumaa lilifika hospitalini hapo na kumuona mrembo huyo akiwa wodini akiendelea na matibabu.


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/30Oag33

No comments:

Post a Comment