Friday, May 3, 2019

Serikali yatoa tamko kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa



Naibu Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara ameliambia bunge kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika mwenzi wa kumi mwaka huu. 

Waitara ameyasema hayo wakati kijibu swali la Alfred Kahigi mbunge wa viti maalum amabaye alitaka kujua ni lini serikali itaongeza posho za viongozi wa serikali za mitaa. 

Naibu waziri akasema kuwa posho za wenyeviti wa serikali za mitaa zinalipwa kulinga na makusanyo ya mapato ya ndani yanayofanywa na  halmashauri huska ambayo mwenyekiti huyo wa mtaa anatoka. 

Akasema kuwa hata moja ya sifa ya viongozi wa serikali wa mitaa anatakiwa awe anashughuli halali inayomwingizia kipato ili isiwe anabaki kutegemea kuendesha gharama za maisha yake kupitia posho hiyo. 

Akaongeza kuwa hata uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyikia mwezi wa kumi moja ya kigezo cha wagombea lazima awe na sifa hiyo ya kuwa na kipato kingine badala ya kutegemea posho zinazotolewa na halmashauri.



from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2V9LJpQ

No comments:

Post a Comment