Habari wakuu....
Jamani mimi huku nyumba imewaka moto, Moja haikai mbili haisogei mama watoto hanielewi.
Iko hivi
This weekend nilitoka kwenda somewhere kwenye mizunguko yangu hapa mjini. Ilivyofika muda was lunch nikapita somewhere kupata chakula maana njaa ilikukua kali na isingekuwa rahisi kurudi nyumbani kwa wakati huo.
Kimbembe.
Kumbe muda ule napata chakula kwa bahati mbaya something like mchuzi ulidondoka kwenye shati na kuacha alama ambayo ilikuwa spherical like a shape, sasa mimi sikujua na kwa namna nilivyokua busy hata sikupata muda wa kujiangalia.
Mama watoto nyumbani.
Mara tu baada ya kurudi nyumbani yeye ndiye alikua mtu wa kwanza kubaini alama ile kwenye shati. Hapo ndipo akauwasha moto huku akidai kuwa ile ni alama ya lipstick ambayo anaamini nimeachiwa alama hiyo na mchepuko.
Nimejieleza sana kama mwanaume nimejitahidi kumuelewesha kwamba ile ni alama ya mabaki ya chakula ambayo ilinidondokea wakati nakula lakini bado hakuamini.
Msimamo wake.
Shati ile ameifungia kabatini kabisa hata hajaifua na masharti aliyoyatoa ni kuwa ili ndoa yetu inisurike basi twende kwa mkemia mkuu wa serikali akapime sample ile ili tujue kama ni lipstick au la.
Shati ile ameifungia kabatini kabisa hata hajaifua na masharti aliyoyatoa ni kuwa ili ndoa yetu inisurike basi twende kwa mkemia mkuu wa serikali akapime sample ile ili tujue kama ni lipstick au la.
Jamani amegoma, ndani hakukaliki... Wadau msaada tutani napata wapi huduma hii ya mkemia mkuu wa serikali au mnisaidie nini nifanye nijinasue maana mziki huku si wakitoto.
Nawasilisha......
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2vCpfyG
No comments:
Post a Comment