Rais John Magufuli ametoa Tsh. Bilioni 5 ili ijengwe mabweni ya Chuo Kikuu cha Teknolojia Mbeya (MUST), huku akisisitiza Wataalamu kutoka chuoni hapo ndio wajenge kwa lengo la kuanze mapema.
Ameeeleza hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Maktaba ya Chuo hicho ambapo amesema sio lazima kuanza kutafuta Mkandarasi wa ujenzi huu sehemu nyingi kwa sababu umechelewa.
"Kama kuna fedha zozote zimebaki Wizara ya Elimu, hata kama ni Bilioni 20, tuzitumie kuletea Chuo hiki cha MUST vifaa vya kisasa, vilivyopo ni vya zamani sana, hivi ndivyo tutamuenzi Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wake," amesema.
Ameeendelea kwa kusema, "Kwa niaba ya Serikali tunaomba radhi kwa kuchelewa kujenga barabara ya kiwango cha lami kuelekea Chuo Kikuu cha MUST, ilihali ni chuo kikongwe na chenye heshima kubwa".
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2GRAjx4
No comments:
Post a Comment