Friday, May 3, 2019

Mradi ujenzi wa Makao ya Watoto Dodoma mbioni kuanza, Tsh Bilioni 10 kutumika



Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Makao ya Watoto Dodoma wenye thamani ya dola za Kimarekani million 5.5 sawa na takriban Bilioni 10 za Kitanzania  unatarajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Kikombo nje kidogo ya Jiji la Dodoma katika eneo lenye ukubwa wa ekari 40. 

Mradi huo ni wa kwanza  na wa aina yake kwa kuwa tofauti na miradi mengine utakapokamilika utatoa huduma za utenganifu wa saikolojioa lakini pia utatoa elimu ya ufundi kuwawezesha watoto waishio katika mazingira magumu kupata stadi za kujitegemea na kuwezesha kaya maskini ambazo watoto hao wanatokea ili kukabiliana na umasikini wa familia. 

Mradi huo Mkubwa unajengwa kwa Msaada wa Shirika la Kimataifa la Abbott lenye Makao yake Makuu Nchini Marekani na unajengwa Jijini Dodoma kufuatia Serikali kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Jijini Dodoma hivyo kulazimika kuhamisha Makao ya Taifa ya Watoto ya Kurasini. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wafadhili wakubwa wa Mradi huo kutoka Shirika la Abbott kuharakisha kuanza kwa Mradi huo mapema iwezekanavyo na  kuhaidi kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha zoezi la kuanza kwa Mradi huo. 

 ‘’Anzeni Mradi huu kwa sasa kwa kuwa viongozi wote wako hapa Dodoma wakishiriki katika Bunge la Bajeti hivyo kuwa rahisi kutatua mambo kwa haraka maana mkichelewa baada ya Bunge la Bajeti watasambaa kila mahali kutekeleza shughuli nyingine za Serikali. 

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Mradi huu unajengwa katika Jiji ambalo limepimwa tofauti na Makao ya Taifa ya Watoto  Kurasini ambayo kwa sasa yako katika msongamano wa makazi ambayo hayakupimwa jambo linalofanya Mradi huu kuwa wa aina yake hapa Nchini.



from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2GTz5kZ

No comments:

Post a Comment