Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge limekataa kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na si ofisi ya CAG.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo bungeni leo mchana Alhamisi Aprili 4,2019 wakati Mkutano wa 15 wa Bunge ukiendelea.
"Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Prof. Mussa Juma Assad. Halijakataa kufanya kazi na Ofisi ya CAG. Na sisi kama bunge hatujawahi kukataa kufanya kazi na taasisi yoyote," amesema Spika.
Bunge lilishapitisha azimio la Kamati ya Haki, Maadili & Madaraka la kutoshirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad baada ya kukiri kuwa Bunge ni dhaifu na kusema hajutii na ataendelea kutumia neno hilo kwani kiuhasibu linamaanisha upungufu.
Utakumbuka CAG, Prof. Assad alipokuwa akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na alisema,'Kama tunatoa ripoti zinaonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, kwangu ni udhaifu wa Bunge,'
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2Vd6QYB
No comments:
Post a Comment