Msanii na mwanasiasa wa upinzani Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bob Wine ameachiwa kwa dhamana na mahakama mjini Kampala japo kwa masharti makali.
Mchakato wa kulisikiliza ombi lake la dhamana uliendeshwa kwa njia ya video akiwa gerezani Luzira.
Aliweza kuwasiliana na hakimu kupitia mawasiliano hayo ya video, hatua ilioepusha kutokea kwa vurugu kama ilivyotarajiwa iwapo angasafirishwa hadi mahakamani.
Ameshtakiwa kwa kushiriki katika maandamano ya 'haramu' mnamo mwaka jana ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii maarufu Uganda kama OTT.
Bob Wine amepewa masharti magumu ya dhamana kulingana na umarufu wake anapopita mjini anakuwa na wafasi wakubwa wakimufatilia, na katika masahriti hayo amekatazwa kuhusika katika mkusanyiko au Maandamano kama anavyosema wakiri wake Asumani Basalilwa.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2VeNVfW
No comments:
Post a Comment