Mamia kwa maelfu ya watu wamehamishwa kwenye pwani ya mashariki mwa India wakati kimbunga kikali kikivuma kuelekea Ghuba ya Bengal kabla ya kupiga leo.
Idara ya Hali ya Hewa ya India imesema Kimbunga Fani ambacho ni kikali mno kinatarajiwa kupiga karibu na mji wa Odisha, wenye hekalu la Kihindi la Puri, kikiandamana na upepo mkali unaovuma hadi kilometa 200 kwa saa.
Majimbo ya Andhra Pradesh, Odisha na Bengal Magharibi yanatarajiwa kukumbwa na mvua kubwa na mafuriko. Karibu watu milioni moja wanatarajiwa kuhamishwa kutoka maeneo ya nyanda za chini hadi kwenye vituo vya muda, shule na majengo mengine yaliyo salama.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2GU9VTq
No comments:
Post a Comment