Friday, May 3, 2019

TEAM YA KMC YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI




Katika kuendeleza harakati za Rais John Magufuli, Timu ya manispaa ya Kinondoni KMC imeingia makubaliano ya kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika kuendeleza uzalendo wa kuhamasisha katika makusanyo na kulipa kodi.

Akizungumza na vyombo vya habari Mstahiki Meya wa Manispaa ya Benjamin Sitta amesema wameamua kutumia mchezo wa leo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Azam FC kwa timu yao kuvaa jezi zenye ujumbe wa kuhamasisha ulipaji wa kodi 'Kodi yetu Maendeleo yetu'.

"Tumekataa ofa nyingi za watu kuweka matangazo kwenye fulana za timu yetu, tukaamua kumuunga mkono Rais ktk suala la kukusanya kodi kuna maneno tumeyaweka kwenye fulana zetu 'Kodi yetu Maendeleo yetu' ktk hili TRA hawajatoa fedha kwani KMC ni timu ya Serikali' - Benjamin Sitta

Meya huyo ameongeza kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kama ishara ya kuonesha uzalendo kwa taifa ukizingatia kuwa timu hiyo inamilikiwa na serikali, huku akisisitiza kuwa wazo hilo wameshirikiana na mamlaka ya ya ukusashaji kodi (TRA) ambao hawajatoa fedha yoyote kwenye zoezi hilo.


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2JdGxds

No comments:

Post a Comment