Friday, May 3, 2019

MBUNGE WA CHADEMA AIPONGEZA SERIKALI KWA MAENDELEO JIMBONI KWAKE





Mbunge Rombo, Joseph Selasini ameishukuru serikali kwa kuridhia kuboresha huduma ya maji kwa vijiji 41 vyenye shida kubwa ya maji wilayani Rombo.

Mbunge huyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameeleza kuwa miundombinu ya maji katika Wilaya hiyo imekaa miaka 20 bila maboresho.

“Changamoto ya maji Rombo inatokana na sababu kwamba hakujawahi kuwa na uwekezaji mkubwa wa maji kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita hivyo miundombinu na vyanzo vya maji havijaboreshwa kwa miaka 20 iliyopita," ameeleza.

Ameendelea kwa kusema, "Hata hivyo kwa sasa ninayo furaha Serikali imerdihia kuboresha huduma hiyo ya maji kwa vijiji 41 vya ukanda wa chini ambavyo ndio vina shida kubwa ya maji” Joseph Selasini-Mbunge Rombo


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2GRAt7E

No comments:

Post a Comment