?
Katika uzoefu wangu wa kusafiri hasa katika routes za DOM, DAR, ARUSHA, KILIMANJARO, MBEYA.
Lakini pia hata routes ndefu ndefu za ndani ya mji! Mfano;
SIMU2000 -MNAZI MOJA
MBEZI - BUGURUNI
SIMU2000- MBAGALA, G. MBOTO
MBEZI - BUGURUNI
SIMU2000- MBAGALA, G. MBOTO
Ikitokea mwanaume umekaa na mdada seat moja? Ni mara chache mdada kutoa salam au kuanzisha maongezi hata safari ikiwa ni ndefu sana.
Sasa kina dada napenda kujua kama mkikaa siti moja na mwanaume either wa umri wako au mkubwa kwako (makamo), nini hasa inakua fikra ya kwanza kichwani kwako! Na kwanini wengi mnasubiri hadi msalimiwe ndo mjibu salam na sio nyie kuanza kusalimia?
USHUHUDA:-
Miaka michache nyuma, nilikua natoka Dar naenda mkoa fulani, nilikaa na mdada kwa kua aliamua kupiga kimya na mimi sikua na mood siku hiyo nikapiga kimya hadi tunafika Morogoro hata salam hatujapeana! Wakati tunaondoka sasa Morogoro baada ta kupata chakula, yule dada aliingia na box la juice ya Azam kwenye bus, bahati mbaya bus linavoondoka box likaniangukia na juice ikanimwagikia mapajani! Alitaka anifute na kitambaa chake nikakataa nikajifuta mwenyewe.

Ila safari nzima kuanzia hapo yule dada akawa kama MC, yani kumbe ni muongeaji vibaya mno! Mimi nipo cool yeye anaongea sana. Kujitambulisha sana kuniambia dhumuni la safari yake, a bit of her family issues.
Kina dada naomba kujua kwanini mna hii tabia, au ni kiburi au maringo au dharau?
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2J9xrhN
No comments:
Post a Comment