Thursday, May 2, 2019

JE KUNA URAFIKI KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE BILA CHOCHOTE?




Nimekuwa najiuliza sana hili, katika jamii zetu za kiafrika hasa Tanzania hivi kweli kuna uwezekano wa msichana na mvulana kuwa marafiki bila ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi?

Katika kufanya uchunguzi wa jambo hili nikagundua kuwa wale wanaojifanya kuwa na Urafiki kati ya msichana na mvulana urafiki wao umejengwa katika hali zifuatazo,

1. Mmoja kati yao (mwanaume au mwanamke) anamtaka mwenzie kimapenzi hivyo anaanza na gia ya kuwa marafiki na mwishowe huishia kuwa wapenzi.

2. Mmoja kati yao (mwanamke au mwanaume) ametongoza na kukataliwa kisha kaambiwa tuwe marafiki, hii huwatokea wanaume wengi hivyo huwalazimu kuwa marafiki kwa kutumaini kuwa ipo siku watakubaliwa.

3. Walikuwa wapenzi kisha wakaachana kwa amani na kuamua kuwa marafiki hivyo wakati wowote wanaweza kurudiana na mara nyingi hutokea kwa watu hawa kurudiana.
Hivyo basi kama urafiki wa mwanamke na mwanaume hujengwa kwa hali hizi je, kuna urafiki wa kweli hapo?

Je, wewe unadhani kuwa upo urafiki wa mwanamke na mwanaume?

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2DJk6Jo

No comments:

Post a Comment