Friday, May 3, 2019

CHUNGA MOYO NA UBONGO WAKO KATIKA SUALA LA MAHUSIANO



Usimlaumu mtu kabla ya kuchunguza,,fikiri kwanza halafu utoe lawama,,Sikiliza kabla ya kujibu,,mwanamke/mwanaume anapochoka mapenzi ya kitoto na kupewa ahadi hewa mwisho wa siku anaamua kutafuta pumziko lenye tija katika mustakabali wa maisha yake na future yake.
Ubunifu wa mapenzi daima hutokea sehemu yenye mapenzi ya dhati na sehemu ya kuaminiana,,baadhi ya vijana linapokuja suala la mapenz,,utoto umechukua nafasi kubwa sana na ndio maana mabinti wengi wenye ufahamu wameingia mwenye mahusiano na wanaume wenye kujitambua na nidhamu ya kila kitu na sio kutizama umri au kazi.
Mke muaminufu ni furaha ya mumewe,,mumewe ataishi kwa amani miaka yote,,ndoa zote tamu zina misingi bora ya uchumba,,chunga moyo wako na ubongo wako katika swala zima la mahusiano,,huwezi kutengeneza future nzuri au kuwajibikia mahusiano yako ukiwa heartbroken.
Baadhi ya wanawake pesa ndo imekuwa kigezo cha kuanzisha mahusiano,,tumia akili kutafakari kuhusu ndoa na usitumie moyo kufikikilia ndoa,,pesa haiwezi kukupa furaha ya ndoa.
Chagua mwanaume mwenye upendo wa dhati akutreat kama princess na usichague mwanaume mwenye pesa akutreat kama housegirl.
Dear brothers mwanamke bora na mjenzi wa familia hatizamwi shape,sura wala rangi,,ubora wa mwanamke upo mwenye ubongo wake,moyo wake na tabia yake.
Wanawake bora hutengeneza mwanaume bora ila usiwekeze kwenye English figure utegemee ndoa/mahusiano bora,muombe Mungu akupe mke/mume bora.


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2Y3CBQB

No comments:

Post a Comment