Sunday, March 22, 2020

Mada 5 Za Kuua Upendo Wa Mwanamke Kwako Na Ambazo Unafaa Kuziacha Sasa Hivi




Kuapproach mwanamke si jambo gumu. Jambo gumu ni kudhibiti mazungumzo yako na mwanamke.
Ok acha tuanze na maswali.
Je, ushawahi kuongea na mwanamke halafu ukagundua ameboeka hataki stori zako tena? Ushawahi kuanza gumzo na mwanamke halafu ikafikia pahali flani ukaanza kuzungumza mada ambazo unazihisi si sawa? Je unajua sheria na masharti ya kufanya wakati unapozungumza na mwanamke? Je unashindwa kudhibiti maongezi na mwanamke?
Well, maswali haya ndio yalimfanya msomaji mmoja wa NESIMAPENZI.com kuwasiliana nasi kupitia inbox ya ukurasa wetu wa Facebook na alikuwa na hili swala zito. (Aliniomba nimstiri jina lake)
Hello Nesi Mapenzi.
Nimekuwa nikimakinika na kufuata hatua kwa hatua machapisho yako ya NESIMAPENZI.com. Kitambo nilikuwa na woga wa kuapproach wanawake lakini sahizi nashukuru muda wa mwezi mmoja sasa nimeweza kufanikiwa kutangamanana wanawake aina tofauti tofauti. Nashukuru. 
Ila sasa nimekumbwa na tatizo jipya. Nashindwa kudhibiti maongezi marefu na mwanamke. Sijui tatizo liko wapi. Naomba msaada wa dharura. Nifanye nini?
Well. Hili tatizo la msomaji huyu wetu (acha tumuite Papito) halimkumbi yeye pekeake, wanaume wengi bila kujua wanaingia katika kategoria hii ya kukosea hadi kumfanya mwanamke kuchoshwa na maongezi yake. Kuna maPapito wengi ambao wanashindwa kudhibiti maongezi wakati wanapoongea na mwanamke.

Katika kumjibu Papito kwa uharaka nilimkumbusha mambo mawili makuu:
1. Tabia ya kuwa mchoyo na kutaka kuongea yeye pekeake na kujipa sifa za kijinga- Tabia hii wanaume wengi hupenda kuifanya bila wao kufikiria. Tabia hii ni kuanzia kutaka kuongea pekeako ili umpendeze mwanamke hadi kujisifu kumiliki elektoniki ghali, kuishi kifahari nk.
2. Tabia ya kutaka kuongea ili uonekane wewe una akili kuliko wote, kuonyesha wewe ni bingwa wa ujuzi katika nyanja tofauti tofauti- Hii kwa mara nyingi baadhi ya wanaume wanaitumia ili kuonyesha madoido yao kwa mwanamke lakini maskini inafika mahali wanabaki na maswali ya kwa nini wameshindwa kumaliza mchezo.
Kwa kuwa mada hizi mbili tayari nilikuwa nimezizungumzia kwa kina hapa, Papito aliweza kuridhika kimtindo flani.
Lakini leo nimeamua nihakikishe hatorudi tena kuulizwa swali kama hilo kwa kumuandalia mada hii:

Maongezi ambayo yataua maongezi yako na mwanamke ghafla.

Hii inaenda kwa maPapito wote kule nyanjani hivyo pia wewe unaweza kujinoa makali ili usithubutu kuongea maongezi aina kama hii.
1. Siasa
Ok. Tunajua ya kuwa  kila kitu kinahitaji marekebisho hapa ulimwenguni, na kila mtu ana maoni tofauti tofauti jinsi ya kusuluhisha matatizo hayo. Na haitakuwa rahisi kwa mwanamke kama huyu kukubaliana na wewe kwa hata asilimia 50. Hivyo jambo zuri ni kuepuka swala hili kadri inavyowezekana....wenyewe wanasema siasa ni mchezo mchafu, hivyo usitake kumchafua kipenzi chako ambaye bado uko safarini unajenga vizingiti kwako.
2. Dini
Kwanza ni kuwa mwanamke unayeongea naye lazima ufahamu ya kuwa katika familia yake ama jamii yake kuna mmoja au mwengine ambao wana dini tofauti tofauti. Mwanamke mwenyewe labda ana imani tofauti tofauti kuhusu dini tofauti tofauti hivyo lazima umakinike kabla hujatoa maneno ya kuudhi ambayo yanaweza kumkwaza.
Pia fahamu kuwa katika dunia hii vita vingi chanzo chake kimekuwa ni dini hivyo usitamani kuanza vita na mwanamke ambaye bado unamtongoza.
3. Usawa
Usiwahi kujaribu kuongea kuhusu ufeministiki, maswala ya jinsia, usawa katika makabila nk. na mwanamke ambaye unajaribu kujenga urafiki ndani yake.
Kila mtu anajua kuwa kuna sheria hizo zote ambazo zimetungwa lakini bado zinakiukwa. Hakuna siku itafikia ya kila mtu kuwa na usawa na mwingine.
Hivyo ukiwa na mwanamke unaongea naye hakikisha ya kuwa unaepuka swala hili kadri uwezavyo.
4. Kazi
Kumwinjoy mwajiri wako inaweza kuwa jambo la kufurahisha....lakini sivyo. Unaweza kuongea jinsi kampuni unayofanya kazi inakuboesha, kuchosha ama kukuudhi. Lakini wadhani nani atashughulika na miguno yako?
Kuongea uchafu na matope kwa mtu ambaye anakupatia mshahara kila mwisho wa mwezi kwa mwanamke kunaua azma ya kuendelea maongezi na wewe.
Pia fahamu ya kuwa kuongea mabaya kila wakati kuhusu mtu kutaanza kuibua maswali iwapo ni wewe ndie mwenye tatizo na unafaa kuondolewa au ndio vipi. Hivyo epusha hili swala kadri iwekanavyo.
5. Ishu zako binafsi
Dalili kuu ya kuwa unaishi ndani ya kichwa chako ni wakati ambapo unaongea maswala yako binafsi na mtu usiyemjua.
Na hii ina maanisha ya kuwa unahitaji mtu akusikilize, jambo ambalo mwanamke hayuko radhi kushabikia kamwe. Mwanzo utakuwa unajenga picha ya kuwa kama unashindwa kumudu matatizo yako binafsi utaweza ya mwingine!
Unless umebahatika umepata mwanamke ambaye ni mshauri nasaha, wanawake wengi watakutenga kama pamba na moto. Jitahadhari na tabia hii.
Upo!?
Ok siwezi kuwa kando yako nikikukochi wakati unapokuwa na mwanamke unaongea naye wala sijui wanawake unaopenda, kuzidisha siwezi kujua ladha ya wanawake unaowapenda. Hivyo kama Papito alivyofanya aliweza kunitumia jumbe moja kwa moja kuwasiliana nami kupitia fb. Hivyo maswali, tashwishi waweza kunirushia huko.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2UtcOBm

No comments:

Post a Comment