Wednesday, July 3, 2019

MAMBO 4 YA KUMFANYIA MWANAUME UNAEMPENDA AKUWAZE MUDA WOTE










Kuwa original.
Ndio ni kweli, usipitishe tu macho yako haraka haraka kusoma hii sentensi kwa sababu ni sentensi uliyoizoea kuisikia mara nyingi. Lakini ulishawahi kujiuliza kwanini ni kitu ambacho maranyingi hupendekezwa wakati unaanza uhusiano mpya?
Kwa sababu ni kweli! Ukiwa original ni kitu kikubwa sana kinachoweza kumfanya mwanaume wako akupende zaidi. Inatakiwa umuoneshe haswa wewe ni nani kutoka kwenye kiini cha ndani ya tabia yako, ukijifanya muigizaji baadae utaumbuka! Kuwa original kutamfanya mwanaume unayempenda akupende wewe kwa jinsi ulivyo.
 Jiamini.
Najua hii umeshazoea kuisikia pia. Kujiamini kunavutia. Inamaanisha unajitambua wewe ni nani na unataka dunia nzima ijue wewe ni nani – na wanaume hupenda hili. Achana na madhaifu yako yote na jiamini ulivyo lazima atakupenda tu.
Jiheshimu.
Hakuna kitu kisichovutia kwa wanaume kama mwanamke asiye jiheshimu. Wanaume hujua- kama unaweza ukaonesha tabia za kutokujiheshimu mwenyewe – unawezaje kumshawishi kwamba unaweza kuwaheshimu wengine? Kwa wewe kujiheshimu kutamfanya macho yake na mawazo yake yakuwaze wewe tu!
 Usitabirike.
Kwa suprise unaweza kwenda nyumbani kwake na pizza, au wyne, au bia, au keki. Siyo tu atavikubali, lakini utamfanya awe kichaa zaidi juu yako. Kuwa unatabirika mara nyingi kuna udhi, na atakuchoka mapema. Kwa kuendelea kum-suprise kutamfanya awe hana ujanja kwako na atakuwa anatamani ajue utafanya nini wakati ujao!]




from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2YvMqHV

No comments:

Post a Comment