Kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba kuwa na mahusiano baina ya watu hawa wawili hukusudia kuwa na upendo ,kujaliana , kuthaminiana , kuvumiliana na kuwa na urafiki wa hali ya juu . Lakini kutokana na hali kuwa mbaya kwa sasa mahusiano ya walio wengi huenda tofauti na m,akusudio ya kuanzisha uhusiano huo,Watu wengi wameumizwa na wapenzi wao kwasababu ya kutokuwepo kwa uaminifu katika mahusiano yao .
Ninaposema kutokuwa mwaminifu hapa namaanisha hali ya mpenzi mmoja kuwa na mahusiano yasio rasmi ya nnje na mpenzi au wapenzi wengine pembeni kwa lugha ya kizazi cha sasa “michepuko”.
Jambo hili mara nyingi hufanywa kwa siri sana na mwenza huyo tena kwa kuogopa sana ili asije akaharibu mahusiano aliyonayo kwa kipindi hicho n wapo baadhi ya wapenzi ambao waliachana na penzi kufa kabisa baada ya siri hiyo kugundulika na wengine kuamua kujiua kabisa ili asishuhudie akiendelea kuumia nafsi.
Pia wapo ambao wameweza kuhimili machungu baada ya kugundua wapenzi wao kutokuwa waaaminifu lakini wapo ambao uvumilivu uliwashinda na kuamua kubaki binafsi au”single” pia wapo ambao hali hii imewaletea shida kabisa na kupelekea kupata shida za kisaikolojia ,kihisia na hata kiafya .
Na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuzijui hata dalili zozote zinazoonyesha mabadilikowalionayo wapenzi wetu ili basi wanapokuwa na tofauti basi tuanze kuzichunguza kabla mambo hayajafika pabaya.
Kutokana na uchunguzi nilioufanya kwa njia ya majadiliano na marafiki zangu ambao wapo kwenye mahusiano na pengine wamepitia baadhi ya dalili hizo au zote na pia kwa kusoma vitabu mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii , asilimia 80 ya watu walio kwenye mahusiano si waaminifu na wenza wao wamekuwa hawayajui mabadiliko yanayoonyesha mtu au mpenzi anayechepuka .
Hivyo hizi ni baadhi ya dalili zinazoonyesha mtu anayechepuka
Kwa kawaida mtu unapomzoea mara kwa marakuwa anawahi kurudi Hapa ningependa uelewe sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini bas anachepukaa au sio mwaminifu , lakini zaidi ya asilimia 80 ya ambao wamekuwa na mahusiano ya nnje , kunakuwepo na hali ya kuwa na visingizio vya mara kwa mara vinavyohusiana na kazi ,mikutano , na safari za kikazi yamkini ww ni mmoja wa shuhuda la hili.
Unaweza kukuta mtu alikuwa anafanya kazi hiyo muda mrefu au tangia muanze mahusiano lakini ghafula hali inabadilika , siku hizi anakuwa mtu wa kuchelewa sana kurudi nyumbani na anaporudi unaweza kutegemea akirudi utamwona amechoka kimwili na hata kiakili kwa majukumu ya kikazi kuhusiana na kazi anayoifanya lakini utakuta mtu wala haonyeshi haaali ya kuchoka na ana furaha kama kawaida, Hali hii inapojitokeza mara kwa mara usichelewe kuwa macho na kudadis I mazingira maana yamkiniipo kazi ya ziada anayoifanya ila sio ile ya ajira unayojua wewe .
Kuwa mkali sana unapoishika simu yake
Yamkini katika mapenzi yenu mwanzoni ulizoea kuwa huru kuishika simu yake kwa wakati unaopenda na yeye anashika simu yako kwa wakati wowote lakini inafika kipindi ghafla unapotaka kuishika tu simu yake utasikia sitaki uishike simu yangu mana kila mtu anasimu yake pengine anadiliki kukuambia hata ukiona mtu anapiga sipo uiache hivyohivyo hata usiipokee , wakati mwengine anaweka neno siri “password” ili usiweze kuifungua na kuitumia, wakati hapo mwanzo alikuwa anakupa namba za siri kila anapobadilisha
Utakuta mda mwengine anadiliki hata kuingia nayo bafuni wakati wa kuoga na utashangaa mda mwengine hata ikiita mbele yako baadhi ya namba hapokei akiwa na wewe au anaenda kuongelea pembeni. tena akiwa katika hali ya wasiwasi utamuelewatu mana atakuwa katika haliya wasiwasi , ukiona dalili kama hizi basi anza kuwa macho na kufanya uchunguzi kwa nini mazaingira yamebadilika gafla , unaweza ukagundua nini kinachoendelea.
Kuwa na hali ya kujipenda kwa kupita kiasi
Inawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa mavazi ya kwaida, hapa simaanishi kutopendeza laa, na wewe ulikuwa umemzoea katika hali Fulani ya mavazi na mitindo lakini ghafla anabadilika nakuwa mtanashati Zaidi anabadilisha mavazi , anapenda mavazi ya gharama na nap engine alikuwa hatumii manukato yoyopte au ya kawaida sana mara anakuwa anapenda manukato tena ya gharama .
Na pia anakuwa mtu anayejijali Zaidi kuliko kawaida yake na ulivyomzoea , katika hali kama hii hembu jaribu kuchunguza kwa ukaribu ili ugundue nini kinachosababisha mabadiliko ya ghafla kiasi hicho
Kupenda kutembea na mipira ya kinga “condoms”
Huwa inashamgaza sana mara nyengine mpenzi mmoja kati yenu kuwa na tabia ya kupenda kutembea na mipira ya kinga au kondomu kwa pochi au mfuko wake kwa kusingizia kuwa anatimiza wajibu wa kujali afya zenu cha kushangaza zaid unakuta yuko kwenye mahusiano ya ndoa nikimaanisha mke na mume yamkinni kuwa anakujali hilo sio jambo la kustua wakati mwengine imahitajika kutumia kinga ili kulinda afya zenu au kwa sabamu nyengine Zaidi
Lakini inakuwaje pale unapogundua kuwa ile kondomu uliyokuwa unaiona au uliiona ghafla haipo tena na yamkini wewe haukuhusika katika kuitumia . ukiona hali kama hii chukua hatua ya kuchunguza kwanini kunakuwa na jambo kama hilo kati yenu.
Kutokuwa na hamu ya kuona uwepo wako
Katika jambo kama hili mara nyingi watu wanapo anza mahusiano kunakuwa na hali ya kujaliana na kutamani kuwa karibu muda wote lakini kutokana na majukumu ya kujenga taifa katika shughuli mbalmbali kuna kuwa na nafasi chache za wapendanao kuwa karibu lakini ukaribu wao wanaweza wakafanya hata kwa njia ya mawasiliano ya simu ya mara kwa mara na kujitahidi kutafuta nafasi ya kuwa karibu japo mara moja kwa wiki hasa kwa wale ambao sio wanandoa yani ambao hawaishi pamoja na kwa wale wanaoshi pamoja unakuta wanaporudi kutoka kazini wakati wote wanafurahiana na kupenda kushirikiana mambo yao kwa pamoja yanayohusu mapenzi yao likiwemo tendo la ndoa ,.
Uliizoea kuwa mnaonana mara kwa mara saa nyengine mara tatu hadi nne kwa wiki kama akiwa hayupo na wewe utakuta anakutafuta kwenye simu mara kwa mara hata kwa message lakini gafla kila unapohitaji ukaribu wake atakwambia yuko bize sana na kazi hivyo hatapata nafasi hadi siku za wikiendi au kukosa kabisa kwa wiki nzima mara anapunguza mawasiliano ya simu na wewe mara kwa mara au akupigii kabisa hata siku tatu na utakuta kama ni wanandoa mnaishi pamoja akirudi hafurahi kama zamani anakuwa kama ni mtu mwenye stress au mawazo mda wote na anapunguza kukushirikisha mambo mengi wakati mwengine kama humuonyeshi hali ya kumuhitaji kimwili inaweza kupita hata mwezi au miezi miwili hajisikii kabisa kukutana kimwili na wewe na ni mzima kabisa ukiona hali hii anza kuchukua hatua .
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2YwyegI
No comments:
Post a Comment