Friday, May 3, 2019
Ni ndoto ya kila binadamu kuishi maisha marefu na yenye afya, kimsingi hakuna binadamu angependa kuishi maisha mafupi na yenye afya mbovu lakini kulingana na asili ya dunia yetu kuna changamoto nyingi sana za magonjwa na ajali ambazo zimepunguza urefu wa maisha wa binadamu wengi. Vipo vyanzo vichache vifo ambavyo kimsingi haviepukiki lakini vyanzo vingi vinaweza kuepukika na kuongeza urefu wa maisha yako hapa duniani.
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuishi maisha marefu;
Acha ulevi
Unywaji wa pombe kupita kiasi una madhara makubwa kwa binadamu. Madhara ya kifedha yaani kufilisika na na madhara ya kiafya. Pombe ina haribu maini kwa kiasi kikubwa sana na baadae heleta kansa ya ini ambayo imeua vijana wengi wadogo.kama unapenda pombe basi kunywa kiasi kidogo na nyakati maalumu na haitakudhuru. Lakini pia wasichana wengi wamejikuta wakifanya ngono mpaka na watu ambao hawakuwategemea sababu ya ulevi.
Acha ngono zembe
Tabia ya kufanya ngono na wanawake tofauti bila kinga haitakufikisha mbali, ukimwi umeua vijana wengi sana na sio rahisi kujua kwani hua ni siri ya familia siku ya mazishi na kama huwezi kutumia kondom basi tafuta mpenzi mmoja muaminifu na utulie naye. Utafiti unaonyesha wanawake wmeathirika sana na ukimwi, pamoja na sababu zingine za kitaalamu lakini hofu yao ya mimba ni kubwa sana kuliko ukimwi.
Kula vizuri
kabla hujala chakula chochote unatafakari kama kina faida yeyote kwenye mwili wako, ulaji wa vyakula ambavyo havina faida mwilini kama pipi, biscuit, soda, na jamii zake vitakuua na kansa siku za usoni lakini pia unene ambao kimsingi huletwa na kula sana utakuletea magonjwa hatari kama kisukari na magonjwa mengine ya moyo.
Tumia vyombo vya moto kwa uangalifu
Matumizi ya vitu kama gari na pikipiki yanahitaji umakini mkubwa sana hasa ukiwepo barabarani, vijana wengi wadogo wameuawa na vyombo hivi. Epuka kuendesha gari umelewa, epuka mwendo mkali, vaa helmet wakati wa kuendesha pikipiki, Funga mkanda wewe dereva au abiria na usikubali kubebwa kwenye gari au pikipiki na mtu ambaye hathamini maisha yake. Usione aibu kumwambia dereva apunguze mwendo kwani umemlipa na ameshika maisha yako. Na wewe usiyejua kuvitumia vyombo vya moto kajifunze kwanza chuoni ndio uanze kuvitumia.
Shiriki mazoezi
Magonjwa ambayo sio ya kuambukizwa kama kisukari, ugonjwa wa moyo, na presha husababishwa sana na maisha ya uvivu. Binadamu anatakiwa afanye mazoezi angalau nusu saa kwa siku. Visingizio kwamba uko bize sana ni dalili ya kukosa vipaumbele na nidhamu kwenye maisha yako. Hizo hela unazotafuta usiku na mchana usipokua na afya bora utakufa uziache.
Epuka ugomvi usio na maana
Mimi nafahamu watu waliopigwa ngumi moja tu wakafa hapohapo. Mwili wa binadamu ni mlaini sana kuna sehemu ambazo zikipigwa unakufa hapohapo. Jitahidi kua mtu wa kusuluhisha zaidi kuliko kukunja ngumi. Watu wote waliouawa kwa kuchoma visu au kupigwa mawe walikufa kwenye mazingira haya. Kama umejifunza kupigana basi pigana pale unapokua umeshambuliwa ili kujilinda sio kuanzisha ugomvi makusudi.
Usivute sigara
Sigara ni moja ya starehe ambayo haina faida yeyote kwenye mwili wa binadamu, huharibu seli za kwenye mapafu na baadae huleta kansa ya mapafu. Unaeza ukasema mbona fulani kavuta mpaka leo hajafa. kila mtu ana kinga yake ya mwili amabyo ni tofauti na mwingine lakini pia hakuna anayechoka kuishi...huyo unayemuona anatamba, siku akiambiwa sigara ndio iko inamuua hata kama ana miaka 90 atasikitika sana.
Usijihusishe na madawa ya kulevya.
Madawa ya kulevya hayatakuua hapohapo lakini yatakuondoa kwenye mkondo wa maisha ya mafanikio. Utadharaulika na kila mtu, utakua huwezi kufanya kazi, muda mwingi utawaza kuiba ili upate madawa mengine ya kutumia. Rafiki yangu mmoja mwaka 2004 alivuta bangi kama miezi sita tu akawa kichaa na hajapona mpaka leo pamoja na kupelekwa hospitali nyingi za vichaa. Unaweza ukaona jinsi amegeuka mzigo kwa ndugu zake.
Jiepushe na uvunjaji wa sheria za nchi makusudi.
Tabia za wizi, dili za kihalifu, uuzaji wa magendo au kumuibia muajiri wako ii ufanikiwe haraka hua hazina muda mrefu sana maishanI, yaani huwezi ukawa mjanja maisha yako yote kwani ipo siku utakamatwa tu. LeO hii kijana au mtu mzima ukihukumiwa miaka 30 basi maisha yako yameishia hapo na huenda ukafia gerezani. Matajiri wote duniani walianza miaka mingi iliyopita. jifunze kua mvumilivu.
Waheshimu wazazi wako
Ukisoma biblia kitabu cha kutoka 20;12 biblia inasema 'waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kua nyingi katika nchi upewayo na bwana mungu wako' sio kuwaheshimu kwa kuwapa shikamoo kila asubuhi bali kwa kufuata maelekezo na ushauri wao kwani wao wameishi miaka mingi sana duniani na wameona mengi kuliko wewe.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2GVKYHb
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment