Kila siku yule Mama alikuwa akienda kugonga mlango katika ile nyumba, beseni lake kichwani akiuza mboga za majani na kila siku alikuwa akiambiwa hawahitaji mboga zamajani. Mama mwenye nyumba alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kila kitu walikuwa wakinunulia supper Market na sehemu safi safi na si mitaani.
Alishamuambia mfanyakazi wake wa ndani kutokununua mboga au kitu chochote kwa wapita njia kwani vinaweza kuwa na magonjwa. Lakini yule Mama hakukoma alienda tu kugonga akisema kuwa anauza mbogamboga, ilifikia hatua wakataka kumpa pesa tu wakidhani ni ombaomba lakini alikataa, yeye alitaka kuuza mboga.
Baada ya kuona hivyo Mama mwenye nyumba alimuambia mfanyakazi wake awe ananunua fungu moja la mchicha kila siku lakini hawakuupika kila siku walinunua na kuuutupa. Hali ile iliendelea kwa zaidi ya miaka miwili. Siku moja mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa mpya alimfuata Mama mwenye nyumba na kumuuliza.
“Mbona yule Mama kila siku akishaleta mchicha pale hutembea mbele kidogo na kukaa pembeni ya Barabara na kulia, kwani ana tatizo gani?” Mama mwenye nyumba alistuka kwani hakuwa akimfuatilia awali,. aliamua kumsubiri siku nyingine na kukuta kweli anafanya hivyo, alimuangalia kwa wiki nzima na kukuta anafanya hivyo hivyo.
Lakini pia aligundua kuwa ingawa mtaa ule ulikua na nyumba nyingine lakini alikuwa akigonga pale tu, hakuenda kuuza mboga katika nyumba nyingine, jambo lile lilimstua na siku moja alipoleta mboga alimuambia aingie ndani na hapo akaanza kumhoji. Mwanzoni yule Mama alikuwa mzito kuongea lakini baada ya kubanwa sana huku akitoa machozi alianza kuongea.
“Mimi siji hapa kuuza mboga, nakuja kumkumbuka mume wangu. Miaka kumi na tano iliyopita mimi ndiyo nilikuwa mmiliki wa nyumba hii, tuliijenga na mume wangu kuanzia msingi mpaka hapo ilipo. Mume wangu alikuwa kiongozi mkubwa serikalini na alikuwa na pesa nyingi, mimi nilikuwa Mama tu wa nyumbani na kutokana na pesa za mume wangu sikuona umuhimu wa kufanya kazi.
Lakini baada ya mume wangu kufariki dunia mamoi yalibdilika. Niliachiwa kulea watoto watano mimi peke yangu bila kazi yoyote, ndugu wa mume wangu walinitelekeza ingawa mume wangu aliwasaidia sana, kweli waliniachia mali zote za marehemu lakini sikujua hata nizifanyie nini. Ndipo nilianza kufanya biashara lakini kwakuwa nilikuwa sijui chochote kuhusu biashara nilipoteza kila kitu.
Mafao ya mume yaliisha yote na nikawa sina hata hela ya chakula, nyumba hii ndiyo kitega uchumi pekee ambacho kilibaki, nikachukua mkopo benki kwa dhamana yake na niliposhindwa kulipa nikanyanganywa ikauzwa. nyie ni watu wa pili kuinunua hii nyumba na kila siku nimekuwa nikija hapa kujikumbusha tu maisha niliyokuwa nikiishi.
Hii nyumba niliijenga kwa jasho langu na ndiyo mali pekee ya mume wangu ambayo naiona na kila mara nikija hapa naangalia na kumkumbuka mume wangu.” Yule Mama alimaliza kuongea huku akitokwa na machozi, Mama mwenye nyumba alimuonea huruma pesa kidogo ili amuongezee mtaji wake. Yule Mama aliaga na kutaka kuondoka lakini kabla ya kufika mbali aligeuka na kumuuliza.
“Samahani Dada kwani wewe unafanya kazi?” Alimuuliza yule mwenye nyumba. Yule mwenye nyumba alitingisha kichwa kushiria kuwa hafanyi chochote. Huku akimnyooshe mkono alimrudishia kile kiasi cha pesa alichokua amempa na kumuambia “Chukua hizi zitakusaidia ufungue biashara yoyote, uwe na kitu cha kufanya, unauhitaji msaada huu zaidi yangu.
Mimi tayari nina biashara ya mchicha naweza kuwalisha wanangu lakini wewe huna biashara yoyote unasubiri mume wako awalishe, haipaswi kuwa hivyo, siku akiondoka watakufa njaa, chukua hizi pesa kafungue biashara ukifanikiwa kutengeneza pesa za kwako basi utanipa msaada na si hizi za mumeo. Mimi pesa za mume wangu hazikunisaidia hivyo sidhani kama za mume wako zitanisaidia hata wewe hazitakusaidia.”
Yule Mama aliziacha zile pesa na kuondoka. Alimuacha Mama mwenye nyumba akiwa ameduwaa tu, hakurudi tena kwenye ile nyumba. Mama mwenye nyumba alizinduka usingizini na kweli alichukua zile fedha na kununua vitenge akaanza kuuza kwa mashoga zake sasa hivi anaduka kubwa la vitenge ambazo huchukulia Congo pia ana duka la nguo ambazo hununua China, hamtegemei tena mume wake kwa kila kitu.
*****MWISHO
#SHARE huu ujumbe labda utaweza kumuamsha mwanamke mmoja aliyelala akimtegemea mume wake kwa kila kitu. Inawa siwezi sema labda ipo siku mume wako anaweza kukuacha na kukutelekeza na watoto lakini nina uhakika kwa silimia 100 kuwa hawezi kuishi milele, hivyo jiandae sasa kama akitangulia yeye na si wewe.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2LRfzJo
No comments:
Post a Comment