Tuesday, October 15, 2019

HILI NI FUNZO KUBWA KATIKA MAPENZI JIFUNZE!!!



Nimekaa sehemu leo napata lunch, mara dada mmoja mrembo aliyekuwa karibu yangu "kareact", "mameseji kibao halafu marefu, hayaeleweki.
Unanijazia tu inbox, utakuwa masikini tu wewe halafu hujiamini".Dah, nilishtuka sana. Baada ya dakika kama 2 hivi..
nikamuuliza dada yangu mbona hasira sana, kwa nini.
Akanijibu "kuna jianaume linanijazia tu inbox, linatuma messages nyingi, ndefu halafu halieleweki, wiki ya pili sasa, mie ananiudhi!"


Nikamwuuliza "mbona unasema atakuwa masikini,akajibu "mtu mwenye hela zake na anayejiamini atahangaika kutuma mameseji kibao, marefu ambayo hata hayaeleweki."


Kwani huyo hawezi kuwa tajiri, lakini kumbe anafanya ufafanuzi kwa kuandika kwa kina,"ingawa simjui, atakuwa hana lolote, anafikiri akijieleza au kuandika sana nitamhurumia au nitamwelewa, akafie mbele huko, tena namblock, hii ni kawaida ya wanaume kapuku."








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/32ksJog

Sunday, October 13, 2019

NJIA ZA KUNOGESHA PENZI LAKO KWAKE DAIMA




KUPITIA safu hii uipendayo, leo ninakupa njia nne zitakazolifanya penzi lako liendelee kunoga, hata kama litakuwa limeanza kufubaa utaliamsha upya.


Wengi wamekuwa hawaelewi mambo mengi kuhusu uhusiano ndiyo maana huishia kulalamika kwamba wanapenda sana lakini mwisho wa siku huishia kutendwa.


Hakuna mtu ambaye hahitaji faraja, kila aliyekuwa na mpenzi wake anahitaji kuwa na furaha. Hakuna mtu ambaye anaingia kwenye mapenzi ili apate msongo wa mawazo, kila mtu anayediriki kuutoa moyo wake, kitu cha kwanza anachokitarajia ni faraja kisha furaha.


Ipo hivyo! Watu wengi wanakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wakiwa na matumaini kwamba hao waliokuwanao inawezekana watakuwa wapenzi wa maisha yao yote. Pasipo kujua, wakati mwingine kuna makosa hufanyika, mtu hajui afanye nini ili penzi alilonalo kwa mpenzi wake linoge, hajui ni njia zipi zitamfanya kupendwa kila siku.


Leo nitakutajia njia chache ambazo kama utazifanya, nakuhakikishia penzi lenu litashamiri zaidi ya lilivyo hivi sasa.


MPE UHURU KWANZA


Kila mtu anapenda kuwa huru, kuachwa afanye mambo yake anayoyapenda. Hakuna mtu anayependa kuingiliwa, hasa kwenye masuala ya kutumia simu yake. Kama kweli unahitaji penzi linoge, usitake kuingilia mambo yake hasa katika matumizi ya simu, unachotakiwa ni kumwambia muda ambao hupendi kuona akizungumza na simu na si kwamba kila unapoona simu yake inaita, unaichukua kwa nguvu.


Mapenzi hayapo hivyo, mpe uhuru mwenza wako. Haimaanishi mtu kama hajatulia basi kuchukua simu muda wote inapoita ndiyo kutamfanya kutulia, hapana, bali kwa kufanya hivyo utampa mbinu nyingine ya kuweza kupambana nawe. Unachotakiwa ni kumfanya kuwa huru, usimuingilie.


CHUKUA MUDA WAKO KUMTOA ‘OUT’


Wengi hukosea hapa, huwa hawapendi kwenda matembezi na wapenzi wao. Wengine hujifanya wapo bize, hata ukimwambia Jumamosi nataka tutoke out atakwambia anataka kufanya hili na lile.


Rafiki yangu, kila mtu anahitaji kuwa karibu na mpenzi wake, hakuna anayependa kuwa na mpenzi ambaye muda wote yupo bize tu. Mchukue, nenda naye sehemu. Kutoka mitoko ya mara kwa mara itawafanya muwe karibu zaidi, itawafanya muda wote mzidi kupendana, ila kama utajifanya upo bize, jua kuna mtu ataitumia nafasi hiyo kutoka na umpendaye.


PENDELEA KUFANYA UTANI


Hakuna mtu anayempenda mpenzi ambaye yupo siriazi saa ishirini na nne. Pata muda wa kukaa na kutaniana naye. Mchombeze kwa vineno vya utani, mpetipeti, mlaze kitandani na uanze kupiganapigana naye vibao vya kimahaba hata kwa kutumia mito ya kulalia.


Unapokuwa siriazi kila wakati inakuwa ni vigumu mwenzako kulifaidi penzi, pendelea kutabasamu inapobidi kila unapokuwa na mpenzi wako, siyo kila atakachokwambia wewe uso wako umekunja ndita kiasi kwamba ataonekana kukuogopa na kumtafuta mtu mwingine ambaye atahitaji kuliona tabasamu lake, atahitaji kuona akifanyiwa utani wa mahaba nk.


HEBU MSIFIESIFIE BASI


Wengi wanaogopa kuwasifia wapenzi wao, hawajui kama kila mtu duniani anapenda kusifiwa. Mpenzi wako anapovaa nguo nzuri zilizomtoa, usikae kimya, mwambie amependeza kwani hilo litamfanya kufurahi sana. Kama utakuwa na mpenzi halafu kila siku humsifii hata akifanya kitu gani, jua kwamba atajisikia vibaya, wakati mwingine atahisi hayupo sawa kwa kuwa tu hujawahi kumsifia.


Unapomsifia mpenzi wako kunamfanya kuongeza umakini katika kuvaa kwake, kununua manukato na hata jinsi atakavyosuka au kunyoa atafanya kwa ubora wa hali ya juu kwa kuwa anajua utamsifia







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2MC2vqJ

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AWE NA FURAHA




Kila mwanaume anapenda kujua jinsi ya kumchangamsha mwanamke ili ampende. Lakini wengi hushindwa njiani pale wanapojaribu kufanya hivyo kwa sababu hawajui vitu vitano vya kumchangamsha mwanamke.


Yafahamu hayo mambo matano, na namna kuyatumia.


Nadhani utakuwa ushashuhudia baadhi ya wanaume wakichati na wanawake(zao),wakati mwingi unakuta mwanamke anacheka na kumsifia kuwa anamfurahisha(“hahahaha!…. unanifurahisha”).


Kuambiwa na msichana kuwa unamfurahisha ni mojawapo ya kitu kikubwa sana ambacho wanaume wengi hawakisikii kutoka kwa mwanamke. Haihusiani na muonekano wako, ila namna unavyopangilia hoja zako na mada zako kwake na jinsi unavyoziwasilisha kwa kuangalia mazingira.


Jinsi ya kumfurahisha na kumchangamsha mwanamke
Ni kitu gani hasa kinamfurahisha mwanamke? Hauwezi kumfurahisha mwanamke kwa kumkejeli au kumshika baadhi ya maeneo ya mwili wake(utaishia kumchukiza na kujiondolea point).


Utajua unamfurahisha mwanamke pale tu unapomfanya ajisikie furaha, na wakati mwingine hushindwa kujizuia na hujikuta anakukiss!.


Ntakupa mambo matano ya kufanya ambayo yakuufurahisha moyo wa msichana unayemtaka(kumpenda).


Unaweza kubadilisha muonekano wako kimavazi, wakati mwingine unaweza kumkazia macho lakini hiyo haitamfurahisha bali itamtisha.


Kumchangamsha/kumfurahisha mwanamke kunahitaji kutengeneza mvuto(impression) zaidi ya muonekano na swaga.


Kama unataka kujua jinsi ya kumfurahisha mwanamke , mwanzo wa yote, huanza na maongezi. Na mwisho wa yote ni hapo pia.


Mawasiliano mazuri kimaongezi ndiyo njia pekee ya kumfurahisha na kumchangamsha msichana.


Yatumie haya mambo matano, na utafanikiwa hata kabla ya kufikia mwihso:


1. Mshawishi kupitia kitu anachokipenda
Unaweza kudahani hii haina umuhimu. Wanaume wengi hufikiri hivyo na hushangaa kwanini tu niongee kuhusu kitu ambacho msichana anakipenda. Kwanini wasichana nao wasiongee kuhusu vitu wanavyovipenda wanaume?


Wanawake huweza kufanya hivyo, japo hatujui. Wanawake wengi hujitahidi sana kujua wavulana hupenda kuongelea nini. Lakini, wakati unataka kumvutia msichana, ni muhimu ukajua ni kitu gani kinachoendelea kwenye mawazo yake. Sasa tambua kwamba, kujua kitu msichana anachokipenda haimaanishi, dhahabu, mitindo au vipodozi. Tofauti kati ya msichana na mvulana kwa namna ya kuishi imepungua sana kwa sasa(wanawake hufanya vingi ambavyo wanaume hufanya). Kwa maana hiyo ni rahisi kuwa na maongezi yenye kuvutia bila kuboa. Achana na mambo ya mahesabu, michezo, teknolojia, amini yatakua poa tu maongezi yenu.


2. Mtanie
Unapoongea na msichana, ni rahisi sana kumfanya na yeye aongee na wewe hatakama hakupenda mwanzo. Lakini hiyo haitoshi. Kama unataka kujua ni jisi gani ya kuongea na msichana/mwanamke, utapaswa kumfanya yeye ajisikie huru na mwenye kujiamini(confortable), lakini pia mfanye ajue kuwa unampenda hatakama haujamwambia.


Kumbuka, kama utaongea nae kama rafiki, lazima awaze na ajue kuwa wewe ni mwanaume noma sana(great guy), lakini hatahisi kwamba wewe ni mwanaume unaeweza kumchangamsha au kumfurahisha. Ili kuonekana kama mwanaume anayefurahisha kwa mwanamke yeyote, inatakiwa akuone kama mtu muhimu wa kukutana nae, na ili kufanya hivyo, msukume sukume hata bega katikati ya maongezi. Lakini usizidishe sana utaishia kumboa, fanya hivyo pale tu anapoongea jambo linalochekesha au lenye utani ndani yake.


Ila usiende na kumwambia maneno ya kawaida kama “unamuonekano mzuri”, “wewe ni mzuri sana”, au maneno yenye kufanana na hayo. Inawakera sana na haioneshi utofauti na watu wengine wa mtaani. Badala yake, jaribu kuwa specific wakati unamuambia jambo fulani mnapokutana. Mwambie maneno kama “umependeza sana leo. Huo ni mtindo mpya wa nywele?”, Hayo ni maneno mazuri sana kwa mwanamke kwa sababu ni wanaume wachache sana huyatumia kwao. Kwa hiyo unavyosema “leo umekua mrembo zaidi” inamfanya ajue ni jinsi gani unamaanisha mpaka umevunja ukimya.


Kwa kumtania huko – unaweza kufanya mambo matatu. Unaweza kumshtua na kumfanya atabasamu. Unaweza kumfanya ajue kwamba wewe unamuona mtu wa tofauti sana. Au tatu, unaweza kumfanya atambue kwamba umemwona wa kuvutia sana. Kumbuka hayo yote unamfanya yeye aone ni mtu mzuri ambaye anaweza kudate na wewe.


3. Kuwa mcheshi(be funny).
Baada ya kumfanya atabasamu na kuyafurahia maongezi yako na yeye, ni muda wa kumuingia ndani zaidi kidogo. Kila mmoja wetu anamambo yake ya siri ambayo hatupendi watu wote wajue labda mtu ambaye tunamwamini sana. Ili kumfanya ajiamini kwako, unatakiwa kumfanya awe na good time sana na wewe. Sasa hatuwezi kukuambia kabisa jinsi ya kumfanya mwanamke acheke. Lakini tunaweza kukupa mambo mawili ya kutumia. Usimwambie utani wowote wakati unaongea nae. Kuwa mwenye furaha muda wote unaoongea nae.


Hii inaweza kukutatiza kidogo. Kwanza kuongea utani wa moja kwa moja kama mtu aliyekariri ni ujinga. Badala yake, ongea nae maongezi yatakayomfanya aone unamtania, na hapo naye ataanza utani.


Jitahidi kuonesha unafurahia maongezi wakati unaongea nae kama unataka kumchangamsha. Ukiwa na furaha, dunia nzima inatabasamu pamoja nawe!. Kama unatabasamu na kujisikia furaha, naye atatabasamu pia na kuwa na furaha. Lakini kama unauoga, utamfanya naye awe
mwoga(unconfortable).


4. Unaweza kumsukuma kidogo kati kati ya maongezi
Najua unaelewa ninaposema kusukumana, hii utokea mara nyingi pale mvulana na msichana wanapukua wamezoeana, kwa hiyo kuifanya na mwanamke kwa mara ya kwanza inatakiwa uwe mwangalifu na makini ili usije kuharibu. Unapofanikiwa kufanya hivyo, jitahidi isiwe kila saa maana utamkera kama nilivyosema hapo awali.


Ili uweze kufanya hivyo inatakiwa uwe wa kawaida – chukulia kama ni mtu wa kawaida japo wewe unajua ni special. Muulize alifanya nini weekend au baada ya kutoka kazini, muulize anapenda kwenda wapi akitoka out au ni mgahawa gani anaupenda au anatamani kwenda au kitu kingine chochote ambacho ni binafsi(very personal). Lazima atajua wewe unamtania mana hakuna mtu ambaye anaweza kuulizwa maswali yote hayo na hajazoea kuulizwa, hivyo lazima afunguke.
Na bila kusitaa, usisahau kuuliza hili swali.


“Hey, samahani hii ni very personal – hivi una boyfriend? Kama unaye basi jua moyo wangu utavunjika vipisivipisi zaidi ya millioni hamsini sasa hivi!”, umeona ilivyo ya kichokozi eeh?. Lakini hii hufanya maajabu!.


Lazima acheke, lakini hiyo sentensi itaweka lengo lako kwake moja kwa moja, na lazima atajua kuwa unamtaka–hahahah!. Lakini angalia usiharibu kwa kuwa kituko baada ya kukupa jibu – maana unaweza kuta anaye, na kama atakwambia anaye tabasamu. Na ongelea mada nyingine tofauti kama vile swali lililopita halikumaanisha kitu kwako. Lengo lake lazima atakuwa ashalijua, na pia utafanikiwa kumfanya awe confortable kwako.


5. Mshike.
Huu ni uwanja hatari sana, lakini ni kitu unachopaswa kujifunza kwa sababu unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, si ndiyo? Hivyo kumshika katika muda muafaka inakamilisha point ya 5 ya mambo ambayo unapaswa kuyajua wakati unataka kumfurahisha mwanamke. Kama utafanikiwa kulifanya hili kwa usahihi, utakua umejichukulia point kubwa sana.


Sasa kumshika msichana ni kama kucheza na moto. Ukiushika fasta hauwezi kusikia joto, lakini ukiushika muda mrefu utaungua! Unaona ilivyo hatari?
Unaweza kumshika bega au mikono kama tayari ushamfurahisha vya kutosha. Lakini kumbuka hili, mshike tu pale unapokua na sababu ya kumshika, mfano mshike masikio kama unayasifia masikio yake au nywele kama unazisifia nywele zake, au mfute koti lake kama kuna kauchafu hatakama hana hako kauchafu, au mshike begani kama unatembea nae barabarani/ mtaani. Kumbuka kumshika mtu ni very personal, hivyo inabidi uwe makini sana na uangalie anamuitikio gani wakati unamshika kabla haujamshika tena.


Kama unataka kujua jinsi ya kumchangamsha msichana, yatumie haya mambo matano wakati utakapokutana na mwanamke next time. Na baada ya hapo utaona ni jinsi gani unavyoweza kumfurahisha mwanamke na kumfanya ayapende maongezi yako kwa mara ya kwanza!.







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/32iOGEk

WANAUME KULALA USINGIZI BAADA YA TENDO LA NDOA




Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.


Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.


Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.


Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.


Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.


"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.


“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.


Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….


Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/35xmI9O

Kwa WANAWAKE TU! Hizi Hapa Njia 14 Za Kujiweka Ili Wanaume Watamani Kukutongoza



Je umekuwa ukijiuliza kwa nini haukuwi approached na wanawaume kama unavyotaka? Mtandao wa huu umeamua kukuandalia mbinu na maujanja ya kutumia ili uonekane mwanamke ambaye anaweza kufukuziwa na mwanaume kwa urahisi.

Owk.... 

Kando na itikadi ambazo umekuwa ukifikiria, kuapproachiwa ama kufukuziwa na mwanaume si gemu ya bahati nasimu ambayo mtu anaingojea ijitokezee. 

Na pia kando na itikadi nyingi za wanawake wanazozifikia, si lazima ufanye kitendo kikubwa ama cha inadi ili mwanaume aweze kukutongoza. 

Ukweli ni kuwa, kama unaielewa akili ya mwanaume na jinsi inavyofanya kazi kabla ya kuapproach mwanamke, unaweza kumfanya mwanaume yeyote kutaka kuongea na wewe dakika tano atakapokuja katika himaya yako. 

So mbinu zenyewe ndizo zipi? 

Zama nami... 

Njia za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukutongoza 

Kwanza jiweke nadhifu 

Hii ni muhimu katika yote kama wataka mwanaume akutambue. Mwanaume kitu cha kwanza anachokiangalia huwa ni mwonekano wa mwanamke. Mwanaume anapoingia katika chumba, inamchukua sekunde ndogo zana kuamua iwapo anataka kuapproach mwanamke mfani au la. 

Kama umevalia vizuri na unapendeza, itarahisisha kazi yako sana. 

Pili usionekane kama una shughli 

Usijishughlishe sana na simu yako, ama kitabu chako, ama kitu kingine. Unaweza kuwa umeboeka na unajaribu kujiweka buzy, lakini fursa iweza kuwa hivi, kufanya hivyo kunaweza kumfanya mwanaume anayetaka kukuapproach kuona ya kuwa uko buzy sana kiasi cha kuwa atashindwa kukufuata kwanu unaweza usiwe interested na maongezi yake. 

Tatu ni kuwa mko ligi moja? 

Hii inakinzana na hatua ya kwanza, lakini inaweza kuwa na tatizo iwapo unaoneka kama uko ligi tofauti na mwanaume. Kama utaoneka amakujiweka mtu wa hadhi ya juu wanawake watapenda kukuangalia lakini hawatakuaproach. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hawapendi kudhalilishwa wakati wanapoamua kukuapproach....kiufupi ni kuwa ukiwa unavutia kupindukia wanaume watakuogopa. 

Lakini tena, kuna wale wanaume ambao wanajiamini kupindukia ambao wanajua thamani ya kukuapproach, nao ni wanaume alfa, wanaume diriki, na pia wale wanaume mapleya. 

Kama wataka kuteka atenshen ya mwanaume mzuri wa kawaida lakini anayeogopa kukuapproach, jaribu kutumia mbinu ya kuwa jamili na watu wanaokuzunguka. Huwa inasaidia. 

Ujanja wa kumfanya mwanaume aweze kukuakuaproach 

1. Jinsi utakavyovalia 

Usivalie kana kwamba huna kitu cha kuficha. Utapata atenshen ya kila mtu lakini wanaume ambao wataamua kukuapproach ni wale ambao wanataka kulala nawe kwa usiku mmoja pekee. Enyewe kuvalia kwa kutamanisha kunasaidia kuteka atenshen ya mwanaume, lakini usivuke mipaka ya kawaida. 

Kumbuka kuwa si lazima uonyeshe viungo vyako vyote vya mwili ili uweze kuteka macho ya mwanaume. Kama unavutia inatosha kumfanya mwanaume akugundue. 



2. Unavyomuangalia 


Mchungulie mara moja na nyingine, halafu mwangalie mara kwa mara. Hakikisha ya kuwa haujisahau ukamwangalia sana kupindukia ama atakuona kama wewe ni rahisi wa kuapproach na anaweza kukupuuza. 

3. Mitindo ya kumwangalia 

Kuna mitindo miwili mikuu ya kumwangalia mwanaume ili kumuonyesha ya kuwa umevutiwa naye. Unaweza kutumia mbinu zote mbili kulingana na vile unataka. 

i) Kumwangalia polepole - wakati ambapo unaangalia pande zote, angalia upande wake na uyaangalie macho yake kwa sekunde kadhaa huku ukiweka tabasamu. Halafu pole pole zungusha kichwa chako uangalie kwingine. Mbinu hii ni ya kijasiri ya kumwonyesha mwanaume umevutiwa kwake. 

ii) Kumwangalia kwa uharaka - hii ni mbinu ya kumwangalia kwa uharaka. Anza kumuangalia, ukiona kama anataka kukuangalia, ghafla angalia kando halafu utoe tabasamu ukiangalia chini. Mbinu hii inampa confidence na kukuona wewe ukipendeza. 

4.Mfanyie kazi iwe rahisi 

Inakuwa vigumu kwa mwanaume kumuapproach mwanamke sehemu ambapo yuko kundini na marafiki zake. Kama mawazo yako ni kufuatwa na mwanaume, hakikisha ya kuwa wakati mwingine unajipa time ukiwa pekeako ama zaidi uwe na rafiki yako wa kike mmoja. 

5. Sehemu zifaazo 

Si kila sehemu ni nzuri kufanya maongezi na mtu. Kama unataka mwanaume akuapproach, chagua sehemu ambayo si kila mtu ataanza kujeuza kichwa chake kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yenu. Sehemu za mkawahawa, supermarket, ama bookshop ni sehemu nzuri zaidi za kukutana na mwanaume kupiga stori. 

6. Mpatie nafasi aongee na wewe 

Hata kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe, unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume huyu kuzungumza na wewe. 

7. Tabasamu 

Onekana jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka macho ya mwanaume yamwone. 

8. Usiboe 

Kuwa mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua. Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo na mwanga. 

9. Usiwe mjeuri 

Kama wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa. 

10. Usitangamane na wanaume 

Hii ni muhimu kwa mwanamke yeyote aelewe. Usiwahi kamwe kutangamana na marafiki zako wa kiume kama unataka kukuwa approached na mwanaume. Haitafanya kazi kamwe. 

11. Mwoneshe kuwa uko intrested 

Mwonyeshe kuwa uko interested kwake kwa kutaka kumjulia hali zaidi. Hata kama uko na marafiki zako mnaongea halafu amekaa karibu na wewe, mwangalie iwapo anakuangalia hata kama unawajibu rafiki zako. 

12. Onyesha uanawake wako 

Mwangalie mara kwa mara, halafu ukishika macho yake, peta nywele zako nyuma ya sikio lako. Inaweza kuonekana kama jambo dogo kwako, lakini kwa mwanaume ni kama kugonga ndipo. 

13. Mtege 

Pita mbele yake halafu mwangalie machoni mwake wakati unapompita. Mtese kihisia, ataipenda kuona atenshen yake. 

14. Usilazimishe 

Utakuwa unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia mara moja na nyingine ama kuwatabamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa. 

Ok hizi ni mbinu ambazo unafaa kuzitumia kama unataka mwanaume yeyote yule akunotice ama akufukuzie.







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2IMHdpc

Thursday, October 10, 2019

JE, KUNA UGONJWA WA KUPENDA KUFANYA MAPENZI AU KUJIENDEKEZA???




Tatizo kubwa la wadada wakisgafikisha miaka 28 kuendelea, ukimtongoza anafikiri kuwa unataka kumuoa, mara ghafla anaanza kukupa mipango ya miaka kumi ijayo mpaka unaanza kuboreka. Mtu hata miezi mitatu hamjamaliza ashaanza kukuuliza “Kwetu unakuja lini?” Dada zangu nije kufanya nini? Kwamba kuna staili ambazo huwezi kunipa mpaka nije kwenu? Hapa ndipo wadada wengi wanaanza kuboa, kwakua ukimuambia kuwa nikama wanalazimishia ukajitambulishe wakati wewe unataka kustarehe.


Maswali yanakua mengi, visirani vinakua vingi mpaka mwanaume unaanza kuwaza “Hivi kama miezi mitatu hivi ananuna mpaka mdomo unanuka kisa tu sijapokea simu yake nitaweza kuishi naye mpaka afe huyu?” Dada zangu mimi nawalewa, lakini unaja wako umekula huko na X wako, mmekaa miaka 7 unampikia na kumpakulia hajaja hata kwenu kuangalia TV, mimi nimejuana na wewe miezi mitatu unataka nikajitambulishe?


Unataka mwanaume akajitambulishe kwenu, mtu hata X wake hajaachana naye vizuri, mwingine alichawa anasubiri akama ataerudiwa au la unataka akajitambulishe kwenu halafu? Najua umri umeenda lakini punguza kasi, tena mwanamke unatakiwa kushtuka umekaa na mwanaume miezi mitatu anataka kuja kwenu kujitambulisha, narudia unatakiwa kushtuka kwani mara nyingi wa namna hiyo naye ni kichomi tu hivyo chunguza kidogo.


Hili swali la “Utakuja lini kwetu kujitambulisha?” Linavunja mahusiano mengi sana, wanawake wanakua na wasiwasi sana wa kuachwa mwanaume akishindwa kulijibu, kibaya Zaidi nikuwa mwanamke anakua na maswali mengi, wasiwasi ambao unageuka na kuwa kisirani, kwa namna hiyo mwanaume anakuchoka, hata kama una mzuka wa kuolewa acha kuuliza kwanza hembu msome mwanaume na si kukimbilia kuuliza wakati unaona matendo yake hayaelekei!









from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2okZfIh

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KIPINDI CHA HEDHI




Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujiusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana..Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili.Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi...Zifuatazo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake{period}..


 MADHARA KWA MWANAUME.
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.


 2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.


 3.Kuziba kwa njia ya mkojo.


 4.Utasa au ugumba.


 5.Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.


 6.Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.
MADHARA KWA MWANAMKE.
1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID( PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.


 2.Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).


 3.Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.


 4.Utasa au Ugumba.


 5.Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.


 6.Athari mbaya ya kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka KU-DO.
NOTE
 Hali hii ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/35jzZTc

JE MPENZI WAKO ANAKUPENDA KWELI AU ANAKUDANGANYA? HEBU SOMA HAPA.


Moja ya dalili kubwa ya mtu uliyenae kuwa anakupenda, ni heshima anayokupa. Heshima ni nguzo ya upendo katika mapenzi yoyote yale, maana huzalisha neno linaloitwa kipaumbele.


Wapenzi wanaoheshimiana, daima hakuna neno ubinafsi bali jambo lao ni lao na si la mtu mmoja mmoja. Maana kila mmoja ulipa kipaumbele jambo la mwenzake.

Upendo huonyeshwa kwa vitendo, na moja ya matendo makubwa ya upendo ni ile heshima unayoipata kutoka kwa mpenzi wako, na ile unayoitoa wewe.

Mpenzi wako anapokuambia ninakuheshimu, ni vinzuri akaonyesha kwa vitendo. Na hiyo ndiyo dalili ya kuwa, mpenzi wako anakupenda kweli na si kwa maneno tu.

Siku zote heshima inapoanza kupungua katika upendo wenu, ni moja ya dalili kubwa ya kuanza kuchokana.

Kumbuka yeyote anayekupenda, basi atakuheshimu. Na mwenye kukuheshimu kila wakati, huyo ndiyo mwenye mapenzi ya dhati kwako. Maana atakujali na kukuthamini kwa jinsi ulivyo.










from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2VsllEw

Wednesday, October 9, 2019

NINI CHA KUANDIKA KWENYE UJUMBE WAKO WA KWANZA WA MESEJI KWA MSICHANA ULIEKUTANA NAE KWA MARA YA KWANZA ?



SOMA STORY FUPI YA MAPENZI YA KUHUZUNISHA YENYE MAFUNZO KWENU HASA HASA WAKINA DADA. NI STORY YA KWELI KABISA


"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile 

nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu 

likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.

Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani 

kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu 

mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.

Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya 

kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga 

lakini aliipinga sana. 

Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani 

nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye 

atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.

Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari 

aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo 

na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo 

baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa 

kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa 

wazazi.

Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta 

kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona 

katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. 

Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na 

tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na 

maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.

Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno 

moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima 

hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.

Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule 

aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha 

yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu 

alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.

Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na 

maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. 

Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini 

uwasimulie wengi baada ya kifo changu.

Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu 

kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie 

vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu. 

Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!

Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku 

moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume 

mwenzako 

AMENITENDA HIVI!!! 








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2AZ7tbq

Mazingira Yasiyoepukika kwa Mwanamke Kutoa Maamuzi



Kuna mambo ambayo wataalamu wengi wamekuwa wakiongelea katika maisha hasa yanayohusiana na hisia, tunapokuja kwenye swala la kutaka kufanya maamuzi tunashauriwa sana kuepuka kufanya maamuzi unapokuwa na hisia fulani, hii inaweza kukuletea matokeo  chanya au hasi lakini mara nyingi unakuwa haujategemea kupata matokeo hayo kulingana na hali uliyokuwa nayo.


Kwa wanawake, hii huwa ngumu kwao kwa sababu kuna hali  ambazo aidha kwa kupenda au kutokupenda anaweza kujikuta tu akifanya maamuzi bila kujali yataleta matokeo gani baadae.


Kwa kumsikiliza pia moja ya wataalamu wa mahusiano kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salam , Chris Mauki anasema kuwa kuna hali ambazo mwanamke hata ufanye nini inakuwa ngumu kwake kuacha kufanya maamuzi pengine apate mtu wa karibu sana kuweza kuzipinga hatua zake.


Baadhi ya hali hizo zinazoweza kumfanya ashindwe kuacha kufanya maamuzi ni pamoja na :-


Akiwa mpweke – akiwa na kiu ya kuliwazwa kwenye upweke wake haangalii huyu ni mume wa mtu, mchumba wa mtu, mzazi wa mtu. Yeye anachotaka upweke wake uishe


 Akiwa desparate (mwenye kiu ya kuolewa) – mwanamke akiwa kwenye hali hii, basi mwanaume yoyote kwake ni potential husband, awe mume wa mtu au la, akifikia hapa hajali mambo ya kupima afya, mambo ya dini au imani, vigezo na masharti vyote vinafukiwa ardhini.


 Akiwa na kiu ya mtoto – Hapa hajaliwi mtu inajaliwa mbegu tu. Kila akiona mwanaume anamwona kama baba mtoto wake, hapa haliangaliwi penzi tena bali mbegu za mtoto. Hapa hata kama ana imani ya kuhamisha milima atakuwa tayari kwenda kwa mganga pale anapoona maombi hayafanyi kazi. Mtoto atatafutwa come what may, come sun come rain


Hali yako na mapito yako yasikufanye ushushe standards zako. Ndio maana taji hata siku moja haitolewi mwanzoni bali mwishoni. Yeye avumiliaye atavikwa taji 







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/310eP9k

Tuesday, October 8, 2019

Kutongoza mwanamke: Siri 15 za kumfanya mwanamke yeyote akupende





Kutongoza mwanamke wakati mwingine inaweza kuwa na tatizo. Hizi hapa ni mbinu na ujanja 15 za jinsi ya kutongoza wanawake na wafall na wewe.Tumeshapitia hapo. Kuna yule mwanamke mrembo ambaye umekufia naye na una hamu ya kutaka kumjua. Lakini kuna lile tatizo linajitokeza ambalo linakufanya ushindwe kuongea na yeye uso kwa uso. Unatamani kuwa na uwezo wa kumuapproach ili umsome akili yake na umwambie yale yote yaliyo moyoni mwako.Hapo hapo, ijapokuwa kutongoza mwanamke huwa inakuja automatic kwa baadhi ya watu, kwa wengine inawafanya wajihisi wako katika hali ngumu. Yale mawazo tu ya kumuapproach mwanamke yakiwajia wanaanza kutokwa na kijasho kwa mikono, midomo inakauka, na unaanza kuongea kama kigugumizi unapotamka maneno – yaani inakuwa mbaya kujieleza na si vizuri itokee kwa mwanaume yeyote. Watu wa aina hii tumezoea kuwaita 'Domo Zege'Habari njema ni kuwa unaweza kujifunza njia za kutongoza, na ufanye mazoezi ya kutongoza hadi ujihisi kuwa umejiamini na tayari kuandama msichana unayempenda. Na kwa hilo, nimekuja na mbinu 15 ambazo unaweza kuzitumia kutongozea wanawake. 

#1 Tabasamu.  
Kutabasamu ni hatua ya kwanza bora ya kuanzia, haswa wakati ambapo umeingiwa na kibaridi. Hakikisha ya kuwa anayaangalia macho yako na unamaintain mtizamo wa macho yenu. Tabasamu huku unajiamini na usiwe wa kwanza wa kuangalia kando. 
Kama atakurushia tabasamu, basi angalia kando kwa dakika chache halafu mwangalie tena huku ukitabasamu. Njia hii itampa ishara ya kumwambia kuwa uko interested na yeye. Lakini usifanye kosa la kurudia rudia kumtabasamia kwa sababu atakuona kama fala. So unachohitajika ni kujiandaa kumuapproach ili uanze mazungumzo. 

#2 Tumia miondoko ya mwili inayofaa.  
Hakikisha unamakinika na miondoko ya mwili wako wakati unapozungumza na yeye. Kama umeingiwa na wasiwasi, usitie shaka muaproach mwanamke huyu kana kwamba hauko interested na yeye. Kuikunja mikono yako, kuangalia miguu, na kuangalia kando hupaswi kufanya kamwe. 
Kuwa wazi na utumie macho yako kuwasiliana naye – mwangalie bila kuona aibu! Tumia mwili wako kumtongoza. Mwonyeshe kuwa umevutiwa na yeye. 

#3 Mguse. 
Njia rahisi ya kumtongoza mwanamke ni kumgusa. Unaweza kumsugua na mkono wako, ama kama umekaa kando yake unaweza kuuachilia mguu wako umguse. Iwapo amependezwa na wewe hatauondoa. 
Kama unamjua zaidi, kumgusagusa hua inafanya kazi vizuri sana. Mkumbatie, weka mkono wako kiunoni mwake wakati unaongea na yeye na hali kadhalika. Fanya haya yote iwapo tu hakatai. Na ukiona kama anarudia kile ambacho unamfanyia basi ujue umefaulu. 

#4 Mfanye acheke.  
Ucheshi ni kitu cha kwanza ambacho wanawake huangalia kwa mwanaume, hivyo basi ni lazima ujifunze tabia ya kuwa mcheshi kama unataka kufaulu katika sanaa ya kutongoza. Kama unaweza kumchekesha basi utamfanya ajifeel amerelax na wewe mara moja hivyo kumvutia. 
Si lazima uwe mcheshi kama Kingwendu ama Churchill ili umfanye acheke, la. Kinachohitajika ni uwe mhalisi. Kila mtu katika huu ulimwengu ana kipawa chake cha ucheshi. Hivyo unaweza kukumbuka jambo lolote ambalo ushawahi kuchekesha mtu. Mwanamke akikupenda anaweza kuchekeshwa na kila neno ambalo utasema. 

#5 Mwache aombe nguo zako.  
Anapenda kuvalia lile vazi lako kubwa, so mpatie avae kama kuna baridi. Hakikisha pia linanukia marashi yako, na kama anakupenda, atatamani akae nalo ili alikumbatie kwa kitanda na akuote katika ndoto zake. 

#6 Msifu. 
Kumsifu mwanamke huwa ni mbinu nzuri ya kutumia wakati unapotongoza mwanamke, so mwonyeshe kuwa anavutia. Kama hutaki kwenda haraka unaweza kuanza na maneno kama ‘leo unapendeza’ ama ‘nimependezwa na kiatu chako’. Hii ni njia ya rahisi kumwambia mwanamke kuwa anavutia bila kusema neno ambalo  litamuudhi. 

#7 Kuwa mzuri mbele ya marafiki zake.  
Hakikisha kuwa unajipa time na marafiki zake. Kama ataona kuwa unajaribu kuwasiliana na marafiki zake, itampa ishara kwake kuwa umependezwa naye na uko tayari kuspend muda naye. Kama bado hajaamua basi atatafuta ushauri kutoka kwa marafiki zake na itakuwa rahisi kwao kukuidhinisha kwake. 

#8 Muulize maswali.  
Kama unataka kujua kutongoza wanawake basi lazima uonyeshe interest kwa kumuuliza maswali mengi. 
Atashukuru ule muda wote ambao umekaa na yeye ukimuuliza maswali kutaka kumjua zaidi. Hakikisha unamakinika na majibu yote ambayo atakwambia ili wakati mwingine mtakapokutana usisahau chochote kile wakati ambapo atakuuliza swali. 

#9 Ijue familia yake. 
Kuijua familia yake ni njia nyingine ya kuonyesha kuwa umevutiwa na yeye na uko tayari kujipa muda kujua zaidi kumhusu. 
#10 Mfanyie favour/fadhila.  
Kutongoza mwanamke huwa kunakuja na njia tofauti tofauti. Kumwonyesha ukarimu mwanamke kwa kumfanyia jambo asilotarajia ni njia murua ya kuhakikisha kuwa utawini penzi lake. 

#11 Mnunulie kinywaji.  
Wakati mwingine vile vitu rahisi huwa ndivyo bora. Kama unataka maongezi yenu yawe rahisi na yaliyotulia basi huna budi kumnunulia kinywaji halafu mazungumzo yaanze na hapo. 

#12 Mnunulie zawadi.  
Zawadi nzuri na yakuvutia ni njia nzuri ya kumtandaza mwanamke katika hali ya kumtongoza. Unaweza kumzawadia zawadi cheshi na yakufurahisha haswa kutokana na mambo ambayo ameyataja kutokana na mazungumzo yenu ya awali. Hii itamvutia. Hakikisha haumnunulii zawadi ambayo ni ya gharama ama iliyo serious coz unaweza kumuogopesha. 

#13 Kuwa interested na mambo anayopenda. 
Pata kujua kile kitu anachopenda na kufanya wakati yuko free, vitu anavyopenda na kila kitu. Hii itakupa nafasi ya kuwa na mambo mengi ya kuongea kuhusu. Ataona kana kwamba mnafanana kimtizamo flani. 

#14 Mtumie SMS. 
Mazungumzo ya SMS ni njia nzuri kwa kutongoza. Kwa mtu mwenye kuona aibu inakuwa rahisi kwake kabla ya kuanza mazungumzo ya moja kwa moja. Mtumie jumbe za kutongoza, cheshi, na kama atajibu inavyostahili unaweza kumtumia jumbe zaidi. 

#15 Mtese.  
Kumtesa kwa upole ni njia nzuri ya kuanza kutongoza mwanamke. Kila mtu anajua kuwa wale wavulana wadogo hupenda kuvuta nywele za wasichana wadogo ambao wamependezwa nao. Hivyo hivyo kumtatiza mwanamke kwa upole, unampa ishara kumwambia kuwa umevutiwa naye. Hii mbinu ina utata lakini ni kweli. 
Mbinu ndizo hizi tushakupa. Usingojee tena. Jiamini uanze kumuapproach yule dada saa hizi! 

NB: Kuna watakaokuja na hoja ya "siku hizi hamna haja ya kutongoza ni Pesa yako tu"....Sijakataa, ila acha wengine wajifunze, najua pesa ina nafasi yake kwenye mahusiano kwani ikipungua na mapenzi vilevile hupungua.... 
Vilevile, kama kuna mbinu nyingine unayo karibu maana najua kuna wale magwiji waliotukuka katika sanaa hii  








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2OwPwJd

Hizi Ndio Mbinu za kumuweza, Mwanamke Aliye Mgumu kutongozeka


Wakati mwingine, vitu huweza kumaanisha zaidi ya tuwezavyo kutamka kwa vinywa vyetu. 
MWANAMUME yeyote anapotaka kumtongoza mwanamke hulazimika kwanza kumwonesha – japo kwa matendo – kuwa anampenda, au kwamba amevutiwa naye, hata kama ni kimwili tu. Hatua hii ndiyo yenye changamoto kubwa zaidi kwa mwanamume, maana ndipo wakati anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe kwa mlengwa huku yeye mwenyewe akijihakikishia kuwa haharibu mambo. 


Mwanamume anapokuwa anajaribu kufikisha ujumbe wa “nakupenda” kwa mwanamke, mapigo ya moyo yanaweza kumwenda mbio, hususan kama mwanamke mwenyewe anaonekana kuwa “maji marefu”. Hata hivyo, ni kazi ambayo kila mwanamume hulazimika kuifanya. 
Kazi hii ya kufikisha ujumbe kwa mara ya kwanza huhitaji umakini. Bahati njema, shughuli yenyewe ina sayansi yake, ambayo ina misingi katika mahusiano ya kijamii. Ukifahamu sayansi hii inaweza kuwa rahisi zaidi kwako kufikisha ujumbe kwa mtarajiwa wako – na kufanikiwa. 

1. KUKUTANISHA MACHO NI MUHIMU 
Kawaida, mambo yote huanzia – na pengine kuishia – katika kukutanisha macho. Mwanamke atakapobaini kuwa hujajaribu kumwangalia japo kwa sekunde mbili mfululizo, ataondoa mawazo na hisia zake kwako hata kabla hujasema neno lolote. 
Macho ndizo zana muhimu zaidi mtu anapokuwa anataka kufikisha ujumbe kwa mwenzake kuwa anampenda, au amevutiwa naye. Hii ni kwa sababu macho ndiyo vipitisho na visambazaji muhimu vya ishara baina ya mtu na mtu, hata kama si katika masuala yanayohusiana na mapenzi. 

Kukutanisha macho na mtu wa jinsia nyingine unayevutiwa naye au anayevutiwa nawe ni jambo lenye nguvu za ajabu katika kuanzisha uhusiano. Kwa sababu hiyo, hata unapofanikiwa kumtazama moja kwa moja machoni mwenzako hutarajiwi kutumia zaidi ya sekunde mbili, kutokana na nguvu iliyomo katika mawasiliano haya. 
Katika hili, wanaume mahiri hufahamu ni wakati gani wa kumwangalia mwanamke na ni wakati gani wa kutomwangalia. Mara nyingi, ni vizuri zaidi kumwangalia zaidi mwanamke wakati anapozungumza, huku ukikwepesha macho kidogo pale unapozungumza wewe. 

2. UNATAKIWA UWIANO, UKWELI KATIKA MAZUNGUMZO 
Ni jambo lisilopingika kwamba wanaume na wanawake wanatofautiana katika maana ya dhana ya mawasiliano. Hata hivyo, bado inawezekana kuendesha mazungumzo shirikishi na yenye kuburudisha ukiwa na mwanamke, bila kuonekana wa bandia. 
Watu wa jinsia zote mbili wanaweza kutuhumiwa kwa kupindisha ukweli na kujaribu kuficha tabia na mienendo yao wanapozungumza na wapenzi watarajiwa. Naam, katika mazungumzo ya kwanza baina ya wapenzi au wachumba watarajiwa uwongo – ukiwemo ule usiotarajiwa – huwa mwingi. 
Katika mazungumzo ya kwanza ni kawaida kwa mwanamume kubadilisha matendo yake na mtindo wake wa kuzungumza kwa maslahi ya kumpata mwanamke, jambo ambalo huifanya hulka yake ya wakati huo kuwa ya bandia. Lakini pia wasichana/wanawake husema “Nakupenda” bila kumaanisha, pengine kwa ajili ya kumfurahisha mwanamume, au kusikia mwanamume atasemaje. 
Jambo la muhimu katika mazungumzo ya awali baina ya mwanamume na mwanamke ni kuepuka michezo ya kudanganyana na kukwepana, badala yake, yafanye mazungumzo kuwa rahisi na halisi. Hapo ndipo mwanamume hujitofautisha na wanaume wengine na kupendwa kwa sababu hiyo. 

3. USIPUUZE NGUVU YA LUGHA YA MATENDO 
Wakati mtu anapokuwa akijaribu kuwasilisha ujumbe wa “Nakupenda” kwa mwenzake, lugha ya matendo yake huzungumza kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno yake. Hili limeweza kuthibitishwa kwa nyakati mbalimbali kutokana na tafiti mbalimbali. 
Katika muktadha wa kujaribu kufikisha ujumbe wa “Nakupenda” kwa mlengwa, lugha ya matendo ndiyo yenye nafasi kubwa zaidi. Kwa hakika, asilimia kubwa ya ujumbe unaowasilishwa kwa mlengwa huwasilishwa kwa njia ya matendo ya mwili na si maneno. Ni asilimia ndogo tu ya ujumbe inayowasilishwa kwa maneno – na wakati mwingine maneno huweza kuleta matatizo maana katika kuzungumza kuna kujikwaa kwingi, kwani ulimi hauna mfupa. 
Ili uweze kufanikiwa katika kueleza nia yako kwa mwanamke, lazima ujue jinsi ya kutumia lugha ya matendo yako. Na pengine hutatumia nguvu, maana watu husema penzi kikohozi – kama unalo litaonekana tu machoni pa mlengwa. 
Ukitafakari kwa makini utabaini kuwa huhitaji kusema sana ndipo uweze kupendwa, kwani maneno huchangia asilimia kidogo tu. La muhimu ni kuhakikisha kuwa mlengwa wako anakusoma na kukuelewa vizuri kwa kuangalia matendo ya mwili wako. 

4. ACHA ASILI ICHUKUE MKONDO WAKE 
Katika nadharia mbalimbali za kijamii na kidini ni jambo la kawaida kusikia kuwa binadamu wote ni sawa. Hata hivyo, katika muktadha wa kimapenzi, kila mtu mmoja mmoja anafahamu kabisa kuwa si kila mwanamume/mwanamke ni sawa na mwenzake. 
Methali yenye asili ya kimagharibi husema “Uzuri wa mtu uko katika macho ya yule anayemtazama.” Hii ina maana pia kwamba, kila mtu anavyo vigezo vyake vya uzuri kwa kuzingatia maumbile yake. Pia jamii zinavyo vigezo vya uzuri, lakini hutangulia kwanza vigezo binafsi. 

Unapokuwa umekaa na mwanamke ambaye anakuvutia kwa mwonekano wake, sauti yake na kadhalika, si rahisi sana kujizuia kuonesha kuwa anakuvutia. Hii ni kwa sababu si wewe, bali ni nafsi yako inayokusukuma. Na yeye mwenyewe atakusoma kwa kuangalia lugha ya matendo yako na kukwelewa, utakaobaki ni uamuzi wake tu. 
Katika jamii kuna vigezo kuhusiana na kiuno, miguu, maziwa, makalio na kadhalika. Wengi wa wanajamii huvizingatia na kuongeza vyao. Huu ni ukweli wa kibiolojia ambao hauwezi kupingika. Mwanamke mwenye vigezo vinavyokubalika zaidi katika jamii yake atawavutia wanaume wengi zaidi. Hapa mwanamume hahitaji kutumia nguvu nyingi – asili ya maumbile itamsaidia humtambulisha mwanamke kuwa amempenda. 

5. TUMIA CHANGAMOTO YA WALAKINI 
Mara nyingi changamoto kubwa katika suala zima la mtu kubainisha nia yake kwa mwanamke hutokana na ukweli kwamba katika mchakato mzima huwa kuna wasiwasi na walakini. Kwa hakika, jambo hili ni la “pengine” au “labda” kutokana na kutoweza kufahamu kirahisi mwenzako anawaza nini. 
Unapoonesha nia yako ya kumpenda mwanamke, ni kama unaamsha hisia zake kwako na ni kama vile unamuuliza: “Ungependa kuwa nami?” Kwa njia hii ni kama utakuwa unafungua mlango wa kupata jibu la “ndiyo” au “hapana” kwani huyo unayemwonesha kuwa unampenda na yeye ana matakwa yake na mapendeleo yake. 
Kimsingi hakuna kanuni wala sheria rasmi unazopaswa kuzingatia wakati wote. La muhimu ni wewe mwenyewe kujiachia na kuingia katika maji usiyofahamu kina wala mwisho wake, bali wewe nenda na mkondo wake huku ukitarajia kuwa lolote linaweza kutokea. Hiyo ndiyo sehemu ya raha yake. 

6. DHIBITI HISIA, MIHEMKO 
Tofauti na mwanamke, mwanamume anayejaribu kuonesha nia yake hatakiwi kujiweka katika mkao wa mwanamitindo. Wanawake ndio hufahamika zaidi kwa mikao yao “ya kula” wanapokuwa katika mawindo (japo wengi hubisha), lakini si mwanamume. Wanawake ndio hutarajiwa kujieleza zaidi kwa njia ya matendo na mikao, lakini wanaume hutarajiwa kudhibiti hisia na mihemko yao . 
Tofauti katika lugha ya matendo baina ya watu wa jinsia mbili hutokana na maumbile ya kujenetiki pamoja na utamaduni wa jamii husika. Yote yakizingatiwa, matakwa ya mwanamke ndiyo hupewa kipaumbele zaidi. Kwa ufupi, matendo ya kutongoza ya mwanamke huwa wazi zaidi, lakini mwanamume hulazimika kuficha hisia na mihemko yake. 
Wajibu wa kufikisha ujumbe kwa mtu wa jinsia tofauti ni wa kila mmoja – mwanamume na mwanamke. Hata hivyo, wanaume ndio wenye jukumu kubwa zaidi la kuanzisha, kwa kuzingatia utamaduni wa jamii nyingi. Unaweza ukaona ugumu, lakini ipo sayansi itakayokusaidia. Kama una wasiwasi na uwezo wako, ni vizuri kuyazingatia yote yaliyobainishwa hapa.







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2AWiaeM

Mbinu Za Kumfanya Mwanamke Akupende bila Kutongoza

Feb 22, 2019




Wanawake wengi huwa hawajui ni kitu gani kinachowafanya wanase kwenye mitego ya wanaume. Hawajui kuwa wanaume wengi hutumia hizi njia kuwafanya wanawake wawapende kila siku. Hizi ndizo njia za kuwanasa.

Wanaume wengi hushangaa na kujiuliza, kwanini wanawake wengi huvutiwa na wanaume wengine, lakini sio wao.

  

Je wanatatizo au mapungufu fulani? Ni kitu gani wanakikosa ambacho hao wengine wanacho/ wanavyo?

Usijali, katika huu mchezo wa kuwavutia wanawake, haikuhitaji uwe na fedha nyingi kwenye account ya benki, au uwe na gari zuri sana kuliko wanaume wote ndo uwavutie wanawake - kinachowavutia ni mwanaume anaye

jua  na anayeweza kuwavutia

Jinsi gani ya kumvutia mwanamke na akupende bila ya wewe kumwambia

#1 Usioneshe unampenda sana. Kwa muda mrefu, kumekuwa na utamaduni wa mwanaume kumwonesha mwanamke anampenda sana ili aweze kukubaliwa, na wanawake ndo wamejijengea utamaduni wa kufatwa. Hii inawapa wanawake uhuru wa kuchagua mwanaume wanayemtaka na kuwatema wasio wataka.

Japo, unaweza ukageuza mambo kwa kuwa karibu na mwanamke na kumfanya yeye ajue kwambw awewe haumuhitaji yeye au hauna lengo la kumtongoza au kumtaka, kwa maana hiyo huna haja ya kumuomba kitu yeye akukubalie. Punguza hisia, zisikuendeshe ssana hatakama unamuhitaji. Hii itamfanya mwanamke akuone wa tofauti kwa sababu wegi wanamsumbua lakini wewe haumsumbui, hivyo atajitahidi afanye kila linalowezekana ili akuvutie(Hivyo umegeuza kibao)

#2 Wakati mwingine KATAA. Usiwe mwepesi wa kukubaliana na kila jambo, wanaume wengi ili wakubaliwe huwa radhi kufanya lolote wanaloambiwa hatakama hana uwezo ili tu amvutie mwanamke. Kama kweli unataka kumvutia mwanamke , hautakiwi kuanguka kwenye huu mtego. Usimvutie kiti ili akae, usimnunulie kinywaji, muda mwingine puuza maombi yake, na ikiezekana kwa baadhi ya mambo useme "HAPANA".

#3 Usiwe rafiki sana. Jijue kuwa wewe ni mtanashati na mwanume halisi. Kama unaingia bar au mgahawani na huyu mwanamke anakuangalia tangu unaingia , nenda kakae kwenye kiti kilichopo karibu na yeye - ikiwezekana umtazame. Hapo mawazo yake yatakuwa yashampeleka kwamba unataka kumuagizia kitu eidha kinywaji au chakula.

Badala yake, achana naye na sura yako bila kujtabatamisha sana agiza kinywaji chako mwenyewe na usimwangalie tena, fata yako. Haya mambo yatampagawisha na itamfanya yeye sasa, afanye jambo lolote ili aweze kukuvutia.

#4 Mfanye awe na wivu. Njia nyingine ya kumfanya mwanamke akupende bila ya kumwambia, ni kuzitumia hisia zake kumuangamiza mwenyewe. Kama unajua anakutamani / kukupenda, mfano, jaribu kuonesha kuwa unatoka na mwanamke mwingine. Kama ni rafiki yako, mwambie kabisa unataka umfanyie vitu vya makusudi vitakavyo mtamanisha mwanamke mwingine. Kwa kumfanya huyo mwanamke awe na wivu, unacheza na hisia zake. Atafanya kila analoweza ili umpende yeye na umuone yule mwanamke uliyenaye siyo kitu.[Soma:Ishara 12 zinazoashiria kabisa anakutaka wewe na anataka umuombe kutoka out!.]

#5 Mchanganyie ishara. Wakati mwingine mwangalie kabisa - macho - masikio - pua vimuelekee yeye. Kama unaongea naye jifanye kama unamsogelea taratibu, kumtamanisha alafu gafla rudi nyuma na uegemee kiti chako. Au, Mwambie yeye ni mwanamke mzuri ana alafu wakati huo umwangalie mwanamke mwingine anayepita pembeni.Haya mmbo yatamchanganya. Hii itamfanya yeye ahisi kuwa anahitaji kufanya vitu vingi zaidi ili aweze kukuteka.

#6 Usitabirike. Kuwa wa tofauti na wanaume wengine ambao alishawahi kuwaona. Fanya kitu kitakaho mfanya asipate picha halisi ya ni nini unamaanisha. Wanawake wengi sana hukerwa na wanaume wanaotumia style moja kuwafata au kufanya mambo kwao. Muahidi utampigia simu muda fulani lakini ukifika ule muda, usimpiigie subiri saa kadhaa zipite ndo umpigie. Utamfanya yeye atamani kusikia neno lolote kutoka kwako lakini hatalipata kwa muda huo. Kwa namna hiyo atakuwa anafikiria sana kuhusu wewe kwa wakati huo.

#7 Uwe mwepesi. Hii ni njia nyingine ya kumfanya mwanamke akupende - kuwa mwepesi wa kufanya mambo ya akili. Jifanye kuwa wewe ni zaidi yake. Vaa vizuri na usiogope kuonesha vitu vizuri ulivyonavyo. Iwe kazini, au mtaani, kama ushajua anachokipenda kuona kutoka kwako - kitumie hicho kitu. Kama kasema anaipenda movie fulani, mwambie jinsi hiyo movie usivoipenda hatakama haumaanishi.

#8 Mfanye ajisikie mpweke. Kuwa mwema na mkarimu na mchangamfu kwa kila mtu - isipokuwa yeye. Hii itamfanya ajistukie - na aone kama vile yeye kuna kitu amepungukiwa au kujiuliza yeye anatatizo gani. Hata penda hivyo. Kwa hiyo atajitahidi kwa namna yeyote anayoweza kufanya mambo yatatamani uwepo wako - au uyaelewe mambo yake anayofanya. 

#9 Mwambie mapungufu yake. Wanawake wengi huwa makini sana katika mambo wanajua ni mapungufu kwao, mfano uzito wao, syle ya maisha, lugha, kwa kuorodhesha vichache. Kama unataka mwanamke akupende muda wote, mfanye ajione hajakamilika.

Mfute kidogo kwenye shavu lake hatakama hana uchafu, mwambie leo hajapendeza - au makeup imemuharibu, au mwambie kuwa unahisi kaongezeka uzito au kanenepa kiasi cha kutisha, hatakama hajanenepa kweli.

#10 Msifie. Njia nyingine ya kumdatisha mwanamke ni kumsifia. Wakati unavoweza kumponda - vivyo hivyo msifie pale anapostahili. Mwambie nanavyonukia vizuri - au nywele zake alivyopendeza, na utamfanya moyo wake uende kasi.

#11 Mfanye ajistukie. Muda mwingine mwambie ni katoto au kituko au wakutamaniwa. Mwambie vyovyote vile vitakavyomfanya abaki na maswali. Hii itamfanya muda wote akuwaze na awe anatilia maanani kila unachomwambia. Mfano, kama utamuuliza aliwaza ini kuhusu njia A ya kukusanya mapato ya biashara, akasema ameshaitumia tayari na ameongeza mapato kwa 19%, mwambie, "Nilijua, utakuwa unatumia mifumo midogo kama hiyo . Sasa, hii ni njia B niliyoiona itakusaidia kuongeza mapato kwa 50%..."

#12 Mkatishe. Muanzishie maongezi, na muulize kitu ambacho unajua anakipenda sana kukiongelea. Na wakati ndo anataka aikoleze story yake, mkatishe na mwambie, "Ohhh.. samahani nilisahau, natakiwa kukutana na mtu muda sio mrefu. Bye!"

Na bila kusita, ondoka na umuache mwenyewe. Hii itamuacha kachanganyikiwa, kwasababu alikua bado hajamalizia story yake. Hapo sasa utakuwa na ujiko wa kumtafuta siku nyingine ya kumuomba mtoke wote ili akakumalizie story.

#13 Mfanye ajione akakimbele mbele sana. Wakati ulimwengu wa mapenzi ukiendelea kubadilika kutokana na utandawazi, sheria za kimapenzi nazo pia zinabadilika - lakini bado wanawake wana udhaifu katika mapenzi. Kwa hiyo muda mwingine mwanamke akikufata - mwambie, "..Unajaribu kunitega au? Kwa sababu kama unalengo hilo, Mimi sipo huko kabisa".

#14 Kuwa mtawala. Simaanishi umuendeshe kwa kila jambo - Hapana. Kuwa muwazi kwa kile unachokitaka katika mahusiano yenu. Kwa lugha nyingine usifiche makucha, hii itamdhihirishia kuwa sio muda wote utakuwa unafata kile anachokitaka. Mfanye ajue mwanzoni kabisa kuwa wewe ni mtu wa aina gani na maisha yako yakoje ukiwa single, jinsi unavyo ishi kwa furaha ukiwa mwenyewe, kwa maanai hiyo hautaki kuingia kwenye mahusiano ambayo yatakuwa yanakupa msongo wa mawazo(stress).Muoneshe ni jinsi gani upo tayari kuwa mwenyewe kuliko kuwa na mtu anayekuendesha. Hii itamsaidia yeye ajue asimame wapi na ni vitu gani inampasa asivifanye.

#15 Jifunze mchezo mchafu wa kutongoza. Mfanyie kitu kimoja kitakachomfanya akupende sana, kisha baada ya hapo muache

#16 Mpe story za uongo. Wanawake hupenda sana maigizo. Huwa na huzuni kwa story zihuzunishazo alafu baadae hufurahi. Kwa hiyo kabla haujamfata mwanamke, fikiria kitu au jambo lililokugusa kimaisha la kuhuzunisha sana. Ongeza vichumvi kidogo ili story iwe tamu utakapoanza kumsilmulia. Kitu cha muhimu hapa ni kuleta furaha na uzuni = = igizo, na hapo atakuwa anakuangalia kwa huruma kama katoto ka mbwa kanachohitaji kupewa chakula.

#17 Kuwa msiri. Ukikutana na mwanamke yeyote yule, usije ukampa taarifa zako zote zinazokuhusu wewe kirahisi hivyo. Kama kakuuliza kuhusu kazi yako na wewe ni fundi ujenzi, mwambie, ninatengeneza tengeneza vitu hapa na pale, na ishia hapo. Kwa kufanya hivyo utamfanya awe anawaza, na kukuwaza wewe zaidi.

#18 Baada ya hapo, tumia silaha yako ya siri(secret weapon). Lile neno "L". Hakuna neno linalowamalizaga wanawake nguvu kama neno "I Love You - Nakupenda". Kama mtakuwa mmeshazoeana na wakati mwingine huwa mnatoka out, usiogope kumwambie kuwa unampenda, na umwambie hili katika hali ya juu kihisia na wakati wote mpo katika hali kubwa ya utulivu. Ukiupatia muda wa kumwambia, hakuna kitakachomfanuya akatae.

#19 Mshike. Hii ni njia nyingine ya kumtamanisha bila hata ya mumwambia neno lolote. We mshike tu. Kama ni rafiki yako sana au kwa kiasi fulani, mshike mkono wake - kama vile haukutarajia, na hapo lazima umdake.

Au kama tayari mmeshazoeana na huwa mnatoka out, unaweza mshika mabega au mashavu. Hii itapeleka signal kwenye mwili wake, na ataanza kujenga hisia na matarajio ya wewe kumwambia kitu - na hicho ndicho ulichokuwa ukikitaka.

#20 Jiamini. Dhihirisha kwamba unaweza kuishi bila yeye. Mvuvi anapokwenda baharini anakuwa anatafuta samaki, akimkosa / akiwakosa sehemu moja haimaanishi ndo mwisho wa maisha yake - hii inampa muda wa kuingia ndani ya bahari zaidi ili kupata samaki wengine. Mfanye ajue kuwa yeye siye mwanamke pekee duniani hatakama unampenda.







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2pVsG3X

Ishara 12 Za Kuonyesha Iwapo Rafiki Yako Amekuzimia







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2pX05eJ

Jinsi Ya Kumtongoza Mwanamke Katika Gari La Abiria

Hello reader wa Nesi Mapenzi! Somo la leo ukimaliza kulisoma nataka ukajaribu angalau mara moja. Najua kuna baadhi ya watu ambao washawahi hujaribu na kufaulu (kawaida unafaulu asilimia 100 kila wakati), so somo lenyewe ni kuapproach mwanamke katika gari la usafiri la abiria. 

Ok, hebu tuanze hivi, ni mara ngapi ushawahi kuingia katika basi ukakutana na mwanamke mrembo ukamtamani? Ama ni mara ngapi ukiwa ndani ya gari ushawahi kumwona mwanamke mrembo ameingia na kukaa mbele yako? Ni mara nyingi. Mambo kama haya hutokezea kila siku. Mwanzo kila siku unapoabiri basi huwa unakutana na wanawake tofauti tofauti na warembo. Na je, unajua mbinu ya kuwaaproach uanze mazungumzo? Somo letu litafafanua kwa upana.


Wanawake wakiwa ndani ya magari ya usafiri huwa rahisi kuwaaproach tofauti na sehemu nyingine unazozijua. Hii ni kwa sababu ya mambo haya:

1. Kinga zake ameziweka chini. Katika gari za usafiri mwanamke huwa hayuko katika hali ya kutangamana, so hatakuwa na mawazo katika akili yake kama vile anavyokuwa katika kilabu. Mfano hafikirii mbinu za kukabiliana na wanaume wanaoudhi ama kuwa na wasiwasi wa kwanini hakuna mtu mpaka sahizi amemuaproach. Nguvu zake zote katika gari la usafiri huwa zimetulia ukilinganisha na wakati ameenda kula bata na marafiki zake usiku. Katika hali hii huwa ni rahisi kumuaproach na anaweza kuungana na wewe kirahisi bila matatizo.

2. Gemu huwa ya juu. Katika magari ya usafiri wanawake ni wengi mno. Kila siku ukisafiri utakutana na wanawake tofauti. Wale ambao utakutana nao leo, si wale ambao utakutana nao kesho. Hii inamaanisha kuwa kadri utakapokuwa ukisafiri ndipo utakapokuwa na nafasi nzuri ya kuchagua mwanamke unayetaka wewe.

3. Una mstari ambao unafanya kazi kila wakati. Kuanza mazungumzo na mwanamke ni rahisi katika magari ya usafiri. Sentensi kama, "Unasafiri ukielekea wapi?" Tayari inaweza kuamsha mazungumzo yasiyokuwa na mwisho.


Ok. Hapo juu tumeonyesha sababu muhimu ambazo zinafanya kuapproach mwanamke katika gari la usafiri kuwa rahisi kuliko zote.

Kuna aina tatu za kumtambua mwanamke abiria. Nazo ni kama zifuatazo:

Hali #1 Mumesimama nje ya gari la usafiri unangojea kuingia ndani ukamwona mwanamke unayempenda. Katika hali hii mara nyingi hutokea katika basi. Abiria wote wako nje wanangojea kuabiri basi, halafu ghafla ukakutana na mwanamke unayevutiwa. Hatua ya kufanya hapa ni rahisi. Unachotakiwa kuanza ni kwenda hadi pale alipo, simama karibu yake halafu umwambie, "Waah, leo abiria ni wengi/wachache. Hivi unaelekea wapi?" Hapa atakujibu bila wasiwasi wowote sababu kinga zake zote ameziweka chini (sababu tumeeleza hapo juu).

Akikujibu usimalizie hapo, mwambie pia wewe unaelekea wapi. Katika mazungumzo yenu hakikisha unaongea mada ambazo zinazungumzia usafiri, usiingize siasa wala michezo. Halafu kuaproach hivi lazima uwe mtu asiyemwoga. Kama unatatizika na uoga wa kutojiamini ingia hapa. 

Sasa mazungumzo yenu hayaishi hapo nje, lazima uingie ndani ya gari. Sasa hapa kuna changamoto kidogo. Kama unaingia ndani ya gari ambalo kiti unajichagulia mwenyewe utakuwa umefaulu kumnasa. Kama tayari mumepewa tiketi ambayo kila mtu ameandikiwa kiti chake itakuwa vigumu kuendelea na appraoch kwa huyu mwanamke kama kiti chako ni nambari 12 na yeye ni 35.

Turudi kwa kujichagulia kiti mwenyewe; Wakati mnapoingia kwa basi, unamwambia maneno kama, "Mi hupenda kuketi katika viti ya katikati, ingekuwa bora tukae katika viti vya nambari 23 na 24." Ukimwambia maneno kama haya hawezi kupinga. Mwanzo ushajitokeza kama mwanaume alpha, jambo ambalo wanawake wanapenda.

Ama unaweza kutumia mbinu nyingine nzuri ya kumwonyesha sehemu ya kuketi kwa kutumia ishara. Mfano wakati mnaingia ndani ya basi, elekeza sehemu unayotaka akae, mwambie, "kaa hapa sehemu ya dirisha." Akishaketi sasa wewe unafuatilia. Hii ni mbinu nyingine rahisi ya kufuatilia.

Kwa kuwa tayari mazungumzo yenu yalianza mkiwa nje ya gari, ni rahisi kuendelea hadi umwombe namba yake ya simu.

Hali #2 Unaingia ndani ya gari la abiria halafu unamwona mwanamke amekaa pembeni akiwa pekeake. Hapa moja kwa moja unaenda kukaa sehemu alipo. Anza na mstari wa, "Unaelekea sehemu gani?" halafu mazungumzo yaanze na hapo.

Hali #3 Umekaa nyuma ya gari, ghafla mwanamke mrembo akaingia na kukaa viti vya mbele pekeake. Hatua kama hii unapaswa kuwa mjanja. Jambo la kufanya ni kuhakikisha kuwa mwanamke aina hii hakukuona. Hakikisha hajaona sura yako. Akishaenda kukaa kwa kiti sasa unaweza kubeba ujasiri wako na kuaproach sehemu alipo. Hapa lazima ufahamu mambo mawili. Kwanza ni kuwa ukienda kukaa sehemu yake lazima atajua kuwa ulikuwa ndani ya gari so lazima uwe na sababu za kwa nini umeenda kukaa na yeye. Pili ni kuwa usipojieleza ukaeleweka unaweza kumfanya mwanamke kama huyu kuziamsha kinga zake hivyo ukakosa kila kitu. So hivi ndivyo unavyopaswa kusema wakati umekaa na yeye, "Kule nyuma kuna joto na unarushwarushwa kila wakati, nimekuja hapa mbele angalau nafeel kibaridi na hewa safi." ama "Nimekuona ukiingia kwa hili gari nikaona si vizuri kumwacha mwanamke nadhifu kama wewe ukae pekeako, waendeleaje lakini?"

So, je kama mimi sina kitu cha kuongea? Kama hujui utasema nini basi hupaswi kuapproach mwanamke aina hii mpaka ujue jinsi ya kuwazoea wanawake.

Mazungumzo ukiwa katika gari la abiria ni rahisi sana. Mwanzo unazungumzia kuhusu gari lenyewe na kampuni inayomiliki, unazungumza kila kitu kuanza mwenendo hadi mwishio, unaongea kuhusu sehemu unayoenda na uliyotoka, vitu mnavyokumbana navyo barabarani nk, yaani mazungumzo hayana mwisho.

NB Wakati mnapowasiliana, hakikisha mazungumzo yenu hayavunjiki. Kuna abiria wengine huongea dakika mbili tu halafu kule kwingine wanaua mazungumzo, haupaswi kufanya hivyo. Hakikisha pia katikati ya mazungumzo yenu unachukua namba yake ya simu. Halafu wale wanaopenda kufanya vituko wakiwa safarini unaweza kutumia ile mbinu yetu ya kuwasisimua wanawake.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2AQYngX

Njia Rahisi Ya Kuchukua Namba Kutoka Kwa Mwanamke Unayemjua


Kuchukua namba kutoka kwa mwanamke ni rahisi zaidi kuliko hata kutamka jina lako. Unachohitajika ni kuenda moja kwa moja kwa mwanamke unayetaka kumuomba namba halafu unamwagiza akupatie. Mara nyingi mwanamke hawezi kukataa kukupatia namba yake unless uwe umemuapproach kwa njia isiyofaa ama hakujui. 


Mara ya mwisho mimi binafsi nilichukua namba kwa mwanamke chini ya dakika moja ya kukutana na yeye. Nilikuwa nimeandamana na marafiki zangu halafu mwanamke mmoja akapita kando yetu halafu muda wa dakika nikaamua kumuaproach na kunipatia namba yake ya simu hapo hapo. 

Kama bado unatatizika ni njia gani za kuchukua namba ya simu kutoka kwa mwanamke basi fuata maagizo haya ya haraka ambayo nitakuelezea. 

#1 Jiamini.  Kujiamini ni kitu muhimu. Wakati unapoamua kuapproach mwanamke lazima uwe unajiamini. Utajiamini vipi? Kujiamini ni rahisi. Kile unachohitajika kufanya ni kuweka nia kuwa wakati ambapo utamwaproach mwanamke lengwa basi lazima namba yake ya simu atakupatia. Huko ndiko nikujiamini. 

#2 Kuwa na mawazo chanya.  Mawazo chanya ni mawazo ambayo yanakubaliana na wewe. Mfano unaweza kuwa unataka kufanya kitu, halafu katika akili yako umeweka dhana ya kuwa kile ambacho unakusudia kufanya basi kitafanikiwa. Haya ndio tunayaita mawazo chanya. Ni dhana ambayo unaamini kuwa itatokezea. Ukiweka mawazo chanya kuwa ukiapproach mwanamke flani na atakupa namba yake ya simu basi bila shaka utafanikiwa. Lakini ukiweka mawazo ya kuwa hautafanikiwa basi kweli hautafanikiwa. 

#3 Kuwa mwigo.  Wakati mwingine inakuwa vigumu kabisa kwa wanaume flani kuongea na mwanamke. Inakuwa vigumu zaidi kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Njia rahisi ya kutatua shida hii haraka ni kuigiza. Kuomba mwanamke namba haichukui zaidi ya dakika mbili, hivyo unaweza kuwa mwigo. Unaweza kuigiza vile rafiki yako anavyoomba namba ya simu ama unaweza kufanya mazoezi kivyako kabla kumuapproach mwanamke kumuomba namba ya simu. 

#4  Relax.  Wakati unapoach mwanamke lazima uwe umetulia. Punguza wasiwasi, toa kijasho chochote ambacho uko nacho, pumua kiutulivu na uondoe ubabaifu wowote ulio nao. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa umerelax utakuwa na nafasi nzuri ya kukumbuka mambo ambayo umeyapanga kumwambia mwanamke flani. Hivyo ni muhimu kurelax kabla ya kuchukua approach yeyote. 

 Njia nzuri ya kumuapproach mwanamke


Njia rahisi ya kuomba namba ya simu kutoka kwa mwanamke ambaye unamjua na anakutambua ni ile ya moja kwa moja. Ukimwona anatembea mtaani halafu wewe umesimama na marafiki zako, mwanzo hakikisha umefuata masharti tuliyoyaeleza hapo juu; jiamini, relax, mawazo chanya na mwigo. Nenda moja kwa moja na umwambie hivi: 

"Mambo Mamito. Niko na ishu flani nataka kukuambia lakini sahizi naona si wakati mzuri wa kukuambia... Nipatie namba yako ya simu nitakupigia simu usiku."

ama

"Mambo Mamito. Napatie namba yako ya simu nataka kukupikia simu jioni nikwambie kitu flani"

Hii ndio njia ya moja kwa moja. Mwanamke wa kawaida, ambaye anakutambua hawezi kukataa kukupatia namba yake ya simu. Mwanzo unaweza kuwa na bahati ya kuwa huyu mwanamke alikuwa inteested na wewe tangu kitambo lakini anashindwa jinsi angeweza kuwasiliana na wewe.

Kama ni mwanamke ambaye humjui na hakujui, basi ni vyema kwanza ujitambulishe ili akufahamu. Si lazima uchukue namba yake ya simu siku io hio bali unaweza kungojea muda mpaka mzoeane.

Wanaume wengi wanatatizwa na tatizo la kutojiamini na woga. Lakini naamini kama unaweza kutatua mambo hayo mawili basi kazi yako itakuwa rahisi.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2LZ9VVX

Monday, October 7, 2019

Jinsi gani ya kuongea na msichana bila kupungukiwa Swaga

Jifunze jinsi ya kuongea na msichana bila kupungukiwa na swaga, bila ya kujali upo wapi. Unachohitaji ni hivi vitu 10 hapa kufanya maajabu na kumteka!.


Mfate alipo


Moja ya vitu ambavyo ni vigumu kwa wanaume wengi kufanya ni kumfata msichana anayemtaka kwa mara ya kwanza. 

Kuchati na mwanamke ni kitu rahisi sana hatakama hamkuwahi kuonana, lakini kumfata ndipo kwenye utata. 

Wakati unapohitaji kumfata msichana ambaye haukuwahi kuongea nae kabla, na ukahitaji kuanzisha maongezi, moyo huanza kwenda kasi kama ngo'ombe anayekwenda machinjoni. 

Fata hizi hatua 10 kwa uda huu mfupi, na kabla haujafika huko, kujua jinsi ya kuongea na mwanamke unayemtaka itakua rahisi kama vile mtu anayetembea kwenye bustani. 
Unapenda sana kuongea na wanawake wa hadhi(high status), si ndiyo? 
Kama vile upendavyo, vivyo hivyo wanawake hupenda kuongea na wanaume wa  
viwango. 
Kwa maana hiyo, hakuna cha kuogopa hapa!. 
Kumbuka, sheria kubwa ya kuijua wakati unataka kujua jinsi ya kuongea na mwanamke unayemtaka - hautakiwi kuvuka hatua. Kama ulivyojifunzaga kutembea kabla haujajua kukimbia, unatakiwa kujua jinsi ya kumtamanisha hata kabla haujaongea nae. 

Sasa Twende.. 

# 1Mfanye ajue kuwa unamtaka . Najua unajua, kuongea na mwanamke kwa mara ya kwanza siyo kama mtu anayemfata mwanamke na kumuomba watoke out. Inatakiwa iende kwa hatua, lakini licha ya hiyo hautafikia lengo. Mwanamke anahitaji kujua unamtamani/ kumpenda hata kabla hamjaongea ili aweze kukuchambua / kukufahamu / kukuchunguza(to evaluate you). 

Kama utamfata mwanamke ambaye kwanza hajawahi hata kukuona ukionesha interest kwake, utaishia kumshtua tu. Na ataishia kukwambia neno ambalo mama yake alimfundisha akiwa mdogo - kwamba akikutana na mwanaume amwambie nini "Niache".  

#2 Fanya mautundu . Baada ya kujua kuna kiumbe kama wewe duniani, anza michezo ya kichokozi. Jitahidi kuwa unamuangalia kila wakati mpaka yeye ajue unamuangalia, hii itamfanya naye awe anafanya hivyo hivyo japo hatapenda kujionesha(ila usimshangae). Sasa unatakiwa kujua, na yeye anakuangalia? je marafiki wake wanakuangalia? je wanatabasamu wakikuona?. Jaribu kujua hayo.  

Hakuna haja ya kutaka kujua jinsi ya kumfata mwanamke ambaye ukimtazama anakuangalia vibaya au kwa hasira, na wakati mwingine hajali kama unamuangalia au la. Kumbuomba mwanamke kutoka nae mda mwingine huwa kama majanga kama haujamvutia, hivyo kuwa mwangalifu. 

#3 Usimchomoe au kumuita kutoka mahali. Kumchomoa mwanamke kutoka sehemu fulani mara nyingine huwa smart na ya kuvutia, lakini mara nyingi siyo njia sahihi. Jitahidi kuangalia mazingira. 
Mfano kama alikua sehemu fulani, kisha akawa anaondoka unaweza mfata na kusimama mbele yake na kumuabia vitu kama " natamani ungejua ni kwa muda gani nimekua nikitamani kuwa na muda kama huu". au kitu kingine cha kawaida. Iwe ofisini, park ya magari au hata bar, jaribu kumuuliza swali ambalo linaendana na mazingira. 

Lakini kumbuka kutumia lugha ambayo itamchanganya ka kutaka wewe uongee zaidi ili akuelewe. 

#4 Usikamie maongezi . Hii hufanikiwa vizuri pale unapomuuliza maswali ya kumchanganya na kuwa anakujibu. Akishakujibu, wote mnakua katika mood ya kuongea lakini bado hamjawa marafiki. Atakuwa anayajibu maswali yako huku akitazama sehemu nyingine. Wakati mwingine anaweza hisi unamtania au unataka kumchanganya, hivyo hatatamani kuendelea na maongezi. 

Unaweza ukafanya hivi, Jitambulishe wewe ni nani au endelea kumuuliza maswali kisha baadae kidogo jitambulishe. Kwa kuangalia muitikio wake wa maongezi, mwambie ni kwa muda gani umekua ukitamani ukutane nae. 

Tayari anajua ni kwa muda gani umekua ukimtazama, kwa hiyo huna haja ya kuigiza kwamba umestukiza. 

#5 Mpe nafasi.  Usimsimamishe maeneo ambayo yatamfanya asiwe anajiamini, mazingira kama vichochoroni au sehemu za kujificha. Kama utaweza, unaweza ukaongea nae hata mbele ya rafiki zake. Kumbuka, ukimsimamisha sehemu ambayo ni salama itamfanya ajisikie kujiamini na kukuamini pia kuwa wewe siyo mtu mbaya.  

Baada ya kumchangamsha, sasa atakuwa anatamani aendelee kuongea na wewe zaidi na utazidi kumvutia kiasi kwamba hataweza kutambua kama unamtega ili uwe nae.







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2AUcMJa

Baada ya penzi moto kwa mpenzi wako mpatie ujumbe huu






kwa yako dozi hakika katika mapenzi wewe ni mkufunzi, wajua bakora kuitumia, mpenzi usije ukawa na mwingine unayempatia, hakika nikijua nitaumia sana, nina wivu na penzi lako tamu my love. Nnakupenda!








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/30SW87h

SMS Nzuri za Mapenzi kwenda kwa mtu umpendae


mtoto unajua kutabasamu maana kila nikiitazama picha yako napatwa na hamu ya ...., natamani kama ningekuwa ufukweni tukila upepepo mtamu huku tukipeana maneno matamu, kisha mzuka ukipanda tukatoane hamu au unasemaje?



1. Wangu kipenzi ninayekuenzi, jua wanitia uchizi na kuninyima usingizi, sijui kama una kizizi au ni mapenzi ndiyo yaninyima huo usingizi, la azizi nimekumiss kichizi, u hali gani mpenzi?

2. Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!

3. Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.

4. Mpenzi najua u-mbali nami, majaribu ni mengi wapaswa kujihami, nituniye zangu zabibu wangu tabibu, jitahidi kuwa mvumilivu nitakuja kukutibu, miss u ma luv.

5. Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kujyatibu, napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu, mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda.

6. Nimeamini wewew ni mtalam wajua kunitoa hamu, unipapasapo huhisi kupoteza fahamu, maneno yako matamu hunizidisha hamu, hakika wajua kunikamua, luv u.

7. Kuwa nawe najivunia, mtoto mapenzi wayajua, kiuno, sauti yako tamu mithili ya chiriki wajua hasa kuitumia, mua wangu wajua kuukamua, ukiniacha jua nitaumia, nakupenda usije niacha nitajiua!

8. Mambo yako adimu ndiyo yanayonipa wazimu, nikuonapo hupatwa hamu, hutamani unipatiye wako utamu, la azizini lini utakuja kunitoa hamu, hakika nimemiss wako utamu na kwa kuupata sifahamu maana ni wewe tu ndiyo mtaalamu. Miss u

9. Dear siku zimekaribia, miaka …… utatimiza katika hii dunia, hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia, hongera kwa wako wazazi kwa kunizalia kipenzi, zawadi yangu toka kwangu ni ahadi ya kulienzi lako penzi. Happy Birthday mpenzi.

10. Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.

11. Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sin thamani katika hii dunia!

12. Namini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi mpenzi, badili yako mavazi, bafuni ingia upate maji kujimwagia, nakupenda la azizi, pole sana na kazi!

13. Huna haja ya kulia kwa yaliyotokea kwani si wakwanza katika hii dunia, mpenzio kumfumania, wengi huwatokea katika hii dunia, tulia na vumilia Mungu atakupatia mpenzi aliyetulia, pole rafiki yangu klpenzi ndiyo mambo ya dunia!

14. Giza limeingia simuoni wakunikumbatia niko kama kinda la njiwa na zaidi ya mshitakiwa mwenye hatiya, sjiui wapi joto kwa kwakulipatia na wajua kipupwe kimewadia, uko wapi my dear?

15. Mpenzi sijui umenipa kizizi maana huishi kunijia kwenye njozi, hakika kwako sijiwezi, nadaka kila nikikuona kwenye lako pozi na usiku ukifika ndipo hutawala zangu njozi, tafadhali mpenzi usiniweke pozi, u hali gani la azizi?

16. Nashukuru kwa yako dozi hakika katika mapenzi wewe ni mkufunzi, wajua bakora kuitumia, mpenzi usije ukawa na mwingine unayempatia, hakika nikijua nitaumia kama sikujiuam. Nnakupenda!

17. Wangu Malkia nashukuru kwa mahaba uliyonipatia, nikikumbuka miguno na viuno ulivyonipatia na raha niliyojisikia, nahisi kuna mwingine unampatia, please dear penzi langu usije wengine kuwapatia! Nakupenda.

18. Ulisema wanipenda na katu kwa mwingine hutokwenda na leo umenitenda! Umeamua kwenda ingawa wajua bado nakupenda, leo ni siku kenda toka umekwenda, amini bado nakupenda na kwa mwingine siwezi kwenda!








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2ANTzJl

Jinsi Ya Kumtongoza Mwanaume Bila Kuonekana Kama Unamtongoza




Kutongoza ni sanaa ambayo baadhi ya wanawake wako nayo na wengine hawana. Je ushawahi kukutana na mwanamke ambaye anaweza kumpata mwanaume yeyote bila tatizo? Tumekuandikia mwongozo wa jinisi ya kumtongoza mwanaume bila kuonekana kama unafanya hivyo.


Kabla haujaijua sanaa hio, lazima ufahamu jinsi ambavyo wanaume wenyewe hutongoza. Kwanza ni kuwa wanaume kwa kawaida hupenda wanawake wanaovutia. Hii inatumika kwa mwanaume yeyote yule. Tabia zao ni moja. So ukitaka kuteka atenshen ya mwanaume, lazima ujue jinsi ya kuvutia.

Pili lazima ujue kuwa wanaume hawawezi kutongoza kila mwanamke. Kutongoza si kitu rahisi. Wanaume wengi huogopa kuanza mazungumzo na mwanamke. Wengi wataweza kukutongoza iwapo tu utatoa ishara ya kuwa unataka kutongozwa. Sababu kuunya wanaume kushindwa kuapproach wanawake hivi hivi ni kuogopa kukataliwa na mbaya zaidi kuwa na sifa za mwanaume zege asiyekuwa na bahati kwa wanawake.

So, utaanzaje kumtongoza mwanaume bila kuonekana kama unamtogoza ili umpatie ile ishara ya kuchangamke?

#1 Onyesha tabasamu na aibu 

Wanaume hupenda mwanamke ambaye anafuraha na hisia chanya. Na zaidi hupenda wanawake wanaotabasamu na kucheka wakati wanapozungumza nao. Usiongee maneno ya kuudhi ama misengenyo ukiwa na mwanaume sababu hawapendi tabia kama hizo. Pia usisahau kutabasamu na kuonyesha aibu.

#2 Msifu na umshukuru

Wanaume pia hupenda kusifiwa. Kumsifia mwanaume ni mbinu ya kwanza kuanzisha mchakato mzima wa kumtongoza. Ukiona kitu kizuri kutoka huyu mwanaume basi usisite kumsifia. Pia mshukuru kwa mambo anayokufanyia. Ukimwonyesha tabia kama hizi, utakua unaanza kumtayarisha kwa mambo ambayo anapaswa kutarijia kutoka kwako hivi karibuni.

#3 Mwangalie machoni

Siri ya kujua jinsi ya kumtongoza mwanaume vizuri ni kwa kujihusisha kwa kila kitu ambacho anapenda kufanya. Si lazima uwe umefall in love na yeye ili uweze kuuteka moyonwake. Kile unachohitaji kufanya ni kumfanya awe na furaha kila wakati anapokuwa na wewe.

So wakati ambapo utakuwa umekutana naye na mnazungumza, mwangalie machoni mwake na umpe tabasamu. Kunaweza kumfanya achanyikiwe lakini mwisho utakuwa umemfanya mnyonge hadi magotini.

#4 Jionyeshe

Mwanamke ni umbo. Hivyo lazima umbo lake lionekane. Hakikisha unamakinika vizuri kwa kioo kabla kutoka kukutana naye. Jipambe vizuri, halia nguo nzuri za kuvutia. Hapa hatumaanishi unavalia nguo za uchi, la. Tunamaanisha unavalia nguo za heshima ambazo zitapendeza mtu yeyote ambaye atakuona.

Wakati mnapoongea na huyu mwanaume hakukusha unajionyesha vizuri. Mfano cheza na macho yako. Cheza na nywele zako wakati mnaongea. Hii ni moja wapo ya njia nzuri ya kumsuka mwanaume.

#5 Usiongee kwa nguvu.

Wanaume hupenda kuona ufemini kwa mwanamke. Hivyo ukiwa unaongea na huyu mwanaume hakikisha ya kuwa unaonyea kistaarabu. Sauti yako unailegeza vile ambavyo inastahili. Pia hakikisha unaongea kwa toni iliyo ya chini.

#6 Mguse mara kwa mara

Hii ndio njia nzuri zaidi ya kuhakikisha kuwa mwanaume anaingiwa na hamu ya kutaka kuongea na wewe. Wanaume hawawezi kujizuia wakati ambapo wanaihisi miguso ya wanawake ikiilisha kwa ngozi zao.

Hivyo kwa upande wako, wakati ambapo unazungumza naye, unaweza kumgusa viganja vyake, kumshika bega ama sehemu yeyote ile ambayo haitazua taharuki.

#7 Kuwa kisichana

Hapa hatumaanishi kuwa lazima ujifanye kama mtoto wa shule ili mwanaume aanze kukutongoza bali tunamaanisha kuwa unajiachilia na kumpa majukumu mwanaume ili achukue usukani. Hapa unamwacha mwanaume anakuwa kama nguzo. Usionyeshe kuwa unajua zaidi kumliko ama una akili nyingi kumliko nk. Mbinu hii utamfanya akuone uko chini yake hivyo itakuwa rahisi kwake kukutongoza haraka.

#8 Mfanye spesho

Kama umejua umuhimu wa jinsi ya kumtongoza mwanaume, basi unajua umuhimu wa kumfanya yule unayemtongoza kujihisi speshio. Hapa huhitajiki kufanya chochote kipya, lakini lazima ukumbuke kuwa ukimfanya mwanaume kujifeel spesho, basi atavutiwa na atatamani kuwa na wewe.

Mfanye ajihisi spesho kwa kumtabasamia na kumuonyesha uso wa furaha. Msifie na uwe unatumia miguso wakati mnaongea. Hapa mwanaume huyu atataka kukutongoza kwa kuwa atakuona mwanamke tofauti kati ya wote.







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/33cUHSV

Mambo Ambayo Wanaume Wanakosea Wakati wa Kutongoza Mwanamke




1.PAPARA 
Wanaume wengi tumekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu.mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake.mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata coz atakufikiria sana juu ya uharaka wako.

2.KUJIFAKE



Wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu.ukiwa unaaproach jaribu kuwa real.huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki afu uko na techno 

3.KUTOSOMA MOOD YA MWANAMKE 
unapomuaproach mwanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke unamtongozaje mwanamke asubuhi?


4.KUMPONDA UR EX LOVER 
Mwanamke anakuuliza kwanini uko single,unaanza kumponda ex wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae.

5.KULALAMIKA 
Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako.

UKITULIA NA KUMTONGOZA MWANAMKE BILA KUYATENDA HAYA MBONA UTAMPATA KILA UMTAKAE







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2LSWC9d