Mungu anasema si vyema mtu (Mwanaume) awe peke yake. (Mwanzo 2:18), na ni kweli Mwanaume hakuumbwa kuwa peke yake eti jeshi la mtu mmoja hata Mungu anajua, upweke unaleta disorder. Lakini wakati unasubiri au ukiwa kwenye mchakato wa kutafuta mwenzi wa maisha usitumie wanawake kama magazine za waiting room Airport ukiwa unasubiri muda wa kupanda ndege. Usijiingize kwenye mahusiano na mtu eti unavuta-vuta muda kupata mtu sahihi. Ni mbaya sana.
Unamtongoza dada wa watu na kumsumbua mpaka anajiaminisha kuwa unampenda kumbe hayuko hata kwenye ndoto zako, unataka tu mtu wa kupotezea mawazo. Yeye (Msichana) anajenga imani kwako na kuanza kukuingiza kwenye mawazo ya hatima (future) yake. Anakubwagia limoyo lake lote, kumbe wewe hata hisia huna. Inaumiza sana.
Bora utumie hiyo nafasi kujikita kwenye michezo au gym au mchakato wa kibiashara, au online courses ili uvute muda ukiwa unajiandaa kupata mtu sahihi wa maisha yako. Kwa nini umwambie mtu unampenda sana na uko tayari kufa kwaajili yake, wakati unajua unamtamani tu na sio kweli kuwa unampenda? Kwanini uumize hisia za mtu kwa makusudi?Kwa nini ujiingize kwenye maisha ya mtu na kumvurugua utaratibu wake kumpotezea muda wake?
Huenda usingakaba hiyo nafasi angekuwa huru kupata mtu wake wa maisha. Lakini we umekaa kwenye maisha yake kama jiwe kwenye mlango wa kaburi la Lazaro, mbele hasogei nyuma harudi, kila siku unamuumiza tu. Umekuwa kitunguu kwenye maisha ya mtu haishi kulia kwa sababu hisia zako haziko kwake.
Hii ni tabia mbaya sana. Kama unasoma post hii na uko kwenye mahusiano na mtu ambaye unampotezea wakati tu huna malengo naye nakusihi umuache mara moja. Kumbuka utapata watoto wa kike najua hautapenda mtu awe kwenye maisha ya mwanao akimpotezea muda.Haya mambo tunafanya wanaume hata Mungu hapendi. Watu wanafeli masomo, watu wanakunywa sumu, wengine wanafia vitandani mahospitalini wakitoa mimba tulizokataa, wengine wamepata magonjwa ya mioyo kwa sababu ya hayo maumivu tumesababisha. Hayana faida hayo maisha, unajiwekea tu laana na mikosi itakayosakama maisha yako. Na ni utoto na upumbavu kutumia uanaume wako, uongo na ujanja ujanja kuchezea hisia za mtu. Amua kubadilika. Huu sio ujanja ni ufala.
TUKUMBUKE MUNGU ANAONA NA UNACHOKIFANYA NI MBEGU UNAPANDA.
#USIJE_KUSEMA_HUKUAMBIWA
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/33aNW4G
No comments:
Post a Comment