Tupa mizigo yako kwa kutumia mbinu hizi.
Inaonekana kwamba watu hawaamini kuwa kuna uwezo wa kuondoa mizigo ya hisia mbaya kwa upesi zaidi. ingawa mazingira yanaonyesha lazima kuwe na badiliko lingine kwanza.
Jaribu mawazo haya.
1.Kuwa mkweli, muwazi, kutokana na chanzo cha aibu
Tuingie kwenye mifano ya kanuni. Unapenda kulala sana usiku, lakini unapenda kuamka mapema . kila siku unajikuta umechelewa kuamka, unajisikia vibaya kwa ajili ya hali hio.
Ukitaka kuamka kwa jambo la muhimu siku hio unaweza, lakini mara nyingi kwenye mambo mengine unachelewa kuamka mpaka marafiki zako wanajua kuwa unalala sana.
Kwa msaada.
Hisia hufuata matendo. kama ukifanya bila aibu kujifunza kuamka mapema unaweza kufanya hivyo bila ya kuwaambia rafiki zako. pia jisikie kuwa hukufanya kosa ila ulijitengenezea tabia hio na kwamba una uwezo wa kutengeneza tabia mpya ya kuamka mapema.
Watu wanaweza kukubaliana na wewe kwa kuwa umekuwa mkweli kuhusu tatizo ulilokuwa nao.
2.Amua Kitu Ambacho hutakiruhusu kikupate
Kati ya asilimia 50 ya mahusianon yanakuwa na hisia tofauti, kwa maana kwamba hayo mahusiano ni chanzo cha kuwaza vizuri au vibaya . Wenza wetu na wanafamilia mara nyingi wanazifahamu hizia zetu, na hufahamu namna ya kuzikataa. Fikiri wakati ambapo mwenza wako anapoleta maumivu yake na kutaka kukuumiza wewe au familia inakusema vibaya kuhusu mwonekano wako, au mwenza wako kukuambia makosa ambayo yalikwisha pita miaka mingi.
Fanya maamuzi ya kutojali, kwa sababu makosa kila mtu anafanya, au kama kuna kitu huwezi kubadilisha achahana nacho. jikubali ulivyo.
3.Chagua malengo ya muhimu .
Kuna watu hutamani kuwa na malengo mengi, mfano, kukimbia, kujifunza lugha mpya, kutaka kuwa na misuli kama wengine, kununua gari nyingine, kujenga nyumba nyingine. vitakuchanganya, chagua kitu cha muhimu kifanye ,vingine vitafuata kidogo kidogo ili usijione kama umeshindwa. Fanya vile vyenye kipaumbele kikubwa.
4.Fahamu kwamba kuna vitu hutaweza
Kama utaangukia kwenye mtego wa kujiona hutimizi majukumu yako kwa mke, wazazi au huwezi kubadilisha ratiba yako ambayo imekuwa na mambo mengi ya kukuzidi lazima utakuwa na wasiwasi.
Usiogope watu, fanya kitu unachokiweza, tena ujisikie vizuri kwa kuwa huna uwezo wa kufanya hicho kwa wakati huo.
5.Jisamehe mwenyewe kwa makosa yaliopita.
Ni makosa gani yanakusumbua, maamuzi gani ulifanya na sasa unajuta? Fikiria maumivu uliyoyapata wakati unajitahidi kutoka kwenye hali hio ili ufike hali nzuri.
Anza kusema kwa sauti ukiwa mwenyewe kuwa umejisamehe kwa kutumia muda vibaya, kutumia pesa vibaya, kwa kutokuwa mwaminifu. Kuongea mwenyewe inasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa woga, wasiwasi uliopo.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2TPXsWE
No comments:
Post a Comment