Thursday, July 4, 2019

ZAWADI 5 ZITAKAZOMFANYA MPENZI WAKO KUKUPENDA ZAIDI











Upendo ni zawadi nzuri zaidi ambayo unaweza kumpa mtu unayemthamini zaidi
Lakini kwa wanawake, je, mnajua baadhi ya mambo unayoweza kumfanyia mpenzio ili aweze kukupenda zaidi?
Unaweza kuzingatia yafuatayo kumvutia zaidi mpenziwe kwani ni wazi kwamba baadhi ya mambo ambayo huwafanya wanawake kujikuna kichwa ni jinsi ya kuwapendeza waume wao.
Ukweli ni kwamba sio eti wanaume hupenda vitu ghali, bali hupenda vitu visivyo na watu wengi, ambavyo vitawafanya kukumbuka kila mara vilikotoka vitu hivyo.
Saa Wanaume wengi hupenda saa nzuri ambazo hazina watu wengi. Ukiweza kununua ghali, basi umefika!
Mpeleke kujivinjari Mpeleke kujivinjari, atafurahi sana. Wanaume ndio huaminika kuwanunulia wapenzi wao zawadi ghali.
Panga kumwandalia sherehe ubwa ya kuadhimisha sikku yake ya kuzaliwa Wanaume wengi hushughulika zaidi kazini na kusahau kuwa wanafaa kusherehekea siku yao ya kuzaliwa. Inafaa kumshtua kwa kualika marafiki wake wote kusherehekea siku hiyo.
Mnunulie nguo Mnunulie shati Unaweza kumnunulia shati, suruali au mshipi. Atafurahia sana ukimpa zawadi ya aina hiyo. Ataithamini zaidi kwa sababu imetoka kwa mtu anayethamini sana katika maisha yake. Picha Tengeneza albamu nzuri ya picha zake kutoka wakati mlipokutana na kuelezea safari yenu katika uchumba wenu. Hii itamfanya mpenziwe kugundua vile ulivyo karibu sana naye.




from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2RR2Ms5

No comments:

Post a Comment