Siku hizi mambo yamebadilika sana. Ukitokea kumpenda mtu fulani kama kweli nia yako ni kuingia naye kwenye ndoa na siyo kukidhi matamanio ya siku moja, zipo mbinu nyingi zinazoweza kukurahishia kazi yako. Kuna simu za mikononi, kuna mitandao ya kijamii na njia chungu nzima hivyo huna haja ya kuendelea kuumia na upweke.
Na lazima ujue kuwa penzi bora ni lile ambalo wawili huanza kwa kuwa marafiki, ni makosa kukurupuka kumtongoza mtu kwenye simu au kwenyemitandao ya kijamii bila kumvuta kwanza karibu yako na kumfanya kuwa rafiki yako.
Unatakiwa kujitahidi kujenga ukaribu naye,
Kama unadhani ni vigumu kwa wewe na yeye kukutana ana kwa ana, unaweza kutafuta namba yake ya simu. Ukishapata namba ya simu ya huyo umpendaye, tafuta muda ambao utakuwa umetulia kisha mpigie na jitambulishe.
Mweleze kwamba umempigia simu kumjulia hali,
Kama akikuuliza mahali ulikoipata namba yake, unaweza kumjibu vyovyote lakini inashauriwa kuwa siyo vizuri kumtajia aliyekupa namba yake kwa sababu unaweza kuwagombanisha.
Usiwe na papara,
Mtakie siku njema na endelea na shughuli zako nyingine. Unaweza pia kuendelea kumtumia meseji za kawaida (siyo za mapenzi),ukimjulia hali, ukimuuliza kama ameshakula au amekula chakula gani, anafanya nini kwa muda huo na vitu anavyovipenda sambamba na vile asivyovipenda.
Tumia sauti ya utulivu yenye hisia ndani yake,
Utazidi kumvuta karibu yako, Usipende kuzungumza kwa sauti ya juu au kupayuka au kupiga simu ukiwa kwenye kelele, akipokea tu simu yako, mjulie hali yake kisha msifie kidogo kuhusu sauti yake na namna anavyozungumza.
Badili mazungumzo,
Muulize kama anajua kwamba yeye ni mzuri sana na hujawahi kukutana na mtu anayevutia kama yeye. Kama wewe ni mwanaume na unayezungumza naye ni mwanamke, utakuwa katika nafasi nzuri ya ‘kum-win’ kwa sababu wanawake wengi wanapenda sana kusifiwa
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2YsBXNi
No comments:
Post a Comment