Tuesday, July 2, 2019

FANYA HIVI KUJITIBU TATIZO LA KUFIKA KILELENI MAPEMA







Kati ya matatizo makubwa kabisa yanayowasumbuwa wanaume katika suala la tendo la ndoa ni tatizo  kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinasema kuwa, wanaume 7 kati ya 10 wanapatwa na tatizo hii.
Malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wanaume yanathibitisha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika mbili kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu wakati wakiandaana na kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa.
Hata hivyo wale wanaoweza kusimama tena mara baada ya tendo la kwanza wanakiri kuchelewa kidogo, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi wa rika zote vijana hata wazee.
Ndoa nyingi zimevunjika chanzo kikiwa ni tatizo hili. Karibu kila pembe ya dunia kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni, ambalo limewafanya waonekane si lolote kwa wenzi wao.
Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humwacha mwanamke na huzuni kwani anakuwa hajapata kile anakihitaji katika tendo hilo.
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.

Hivyo zifuatazo ni njia za kujitibu tatizo la kuwahi kufika kileleni:

1. Acha mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.
Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.
Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.
4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.
Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku.
5.  7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!
Fanya hivi kila siku kila unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4. Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama umepona tatizo lako. Pia unaweza kuamua kutumia siku 1 na siku inayofuata unapumzika na siku ya tatu unaendelea hivyo hivyo kila baada ya siku 1.
6. Kula tikiti maji
Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.
Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara
7. Kula ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.
8. Tumia chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.




from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2LwEWAB

No comments:

Post a Comment