Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili.
Wataalamu wanasema kwamba unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.
- Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani. Kuongeza mwendo wa damu.
- Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili. hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji
- Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.
- Hupunguza maumivu wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu ya viungo [arthritis] maumivu ya shingo [Whiplash] na maumivu ya kichwa
- Ulinzi wa tezi ya kibofu [mwanaume] Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu [prostate] yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini.
- Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa maji maji hayo yenye madhara.
- Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.
- Hupunguza mfadhaiko wa moyo.
- Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini.
- Wale wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.
- Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume [testosterone] na za kike [Oestogen]
- Faida nyingine inayopatikana kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi.
- Hata hivyo baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2Xrttth
No comments:
Post a Comment