Wakati wa kulala si lazima wapenzi wafuate utaratibu ule ule kila mara.Hii inawezekana msimamo wa akili ulivyo kwa wakati huo.Fuatilia mitindo ya ulalaji na maana yake
KUKUMBATIANAMtindo huu hutumika sana kwa miaka 5 ya mwanzo wa ndoa.Mume huweka miguu juu ya mkewe na mikono kumkumbatia eneo la kifuani.Aina hii hupendwa sana na wanawake kwani hujiona yuko salamaNi alama ya mahusiano bora ya kimapenzi.
KUTAZAMANAHukumbatiana lakini baada ya saa 2 au 3 hujibagua na kila mmoja kulala upande wake.Ni alama ya kusaidia kuondoa mkinzano unaoweza kujitokeza.
MALIWAZO YA MUMEHushikana mikono na mke kuweka kichwa chake kwenye mabega au juu ya kifua cha mumewe.Ni alama ya tafsiri ya mapenzi ya dhati ya mume kwa mke.
BARAFU WA MOYOMke hupanda juu ya mume na wanaweza kujadiliana mambo mbalimbali.Ni alama nzuri nyakati za maelewano.
KILA MMOJA UPANDE WAKEIkiwa mmoja kaweka mguu mmoja au mkono kwa mwenzake,mtindo huu hujulikana kama daraja la mahusiano.Si alama ya kutiliwa mashaka
USINGIZI BARIDIPale wanandoa wanapolala kama wasiotambuana bila kugusana pasipo kujielewa ni alama kuwa wako mbali kifikra.Hutokea pale mvuto usipokuwepoHali hii isiruhusiwe ikue.
VISIWA TOFAUTIWanalala bila ushirikiano kwa visingizio vya kuchoka,ni kama visiwa viwili tofauti.Chanzo chaweza kuwa matatizo ya kimwili,kiakili au kiuchumi.Hali hii ikitokea mara kwa mara huweza hata kuachanisha wapenzi
MGONGO KWA MGONGOMtindo huu hujitokeza sana kwa wapenzi.Ingawa wanaweza kupeana migongo lakini wanaweza kuwasiliana.Ni alama ya kawaida na wanasaikolojia wanauita mtindo huu “muda wa kupumzika”
MZIGO USIOHITAJIKAKila mmoja hulala kivyake na mara nyingi ni kama vile wanandoa wanataka kuonyeshana umwamba.Kila mmoja hamjali mwenzake,,hali hii si ya kawaida ni mbaya sana kwani hutengana kuanzia wanapopanda kitandani hadi kunapokucha.Si ajabu hata kununua vitanda viwili au kulala vyumba tofauti.Wanasaikolojia wanaita hali hii kiburi na jeuri.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/319ygxB
No comments:
Post a Comment