Saturday, June 1, 2019
KINA KAKA MUOGOPE WANAWAKE WA NAMNA HII
1.Asiyeridhika na penzi unalompa
Wapo wanawake ambao wewe unaweza kujitahidi kumpatia mapenzi kadri unavyoweza lakini yeye hatosheki,,anakuchukulia wewe ni dhaifu sana na wakati mwingine kuhisi yupo anayeweza kumpa zaidi ya kile unachompa,,huyo ni tatizo.
2.wivu uliopindukia
Hatukatai,wivu ni muhimu katika swala zima la mapenzi lakini kuna ule wivu uliopindukia mpaka hugeuka kuwa kero,,waliopo kwenye ndoa wananielewa.
3.Anaona unamsaliti kila mara
Huku kunatokana na kutokujiamini tu,,,ukioa mwanamke ambae ukiwa na mbali nae tu anahisi unamsaliti,,huyo hakuamini na kamwe hamuwezi kudumu,,mtakuwa watu wa kugombana tu kila siku.
4.Anahisi amekosea kuolewa na wewe
Wapo wanawake ambao wanapoingia kwenye ndoa baada ya muda wanahisi wamekosea kuolewa na mwanaume HUYO,,unamkuta mke wa mtu anahisi fulani ambaye zamani alikuwa nae kwenye mahusiano ndo anafaa kuwa mume wake baada ya kuona upungufu fulani kwa yule aliyemuoa.
5.Yupo kimasilahi zaidi
Kuna wanawake ambao wanakuwa na furaha na wewe ukiwa nazo tu,,ukiishiwa wanaanza kununa na kisirani tu.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2Wi61Ot
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment