Saturday, June 1, 2019
KAMA UNATAKA KUDUMU KATIKA MAHUSIANO EPUKA MANENO HAYA
Endapo umekwisha ingia katika mahusiano au unatarajia kuingia katika mahusiano ya KIMAPENZI,,,,,yapo mambo ambayo yanafaa kumwambia mpenzi wako naye akafurahi lakini pia kuna mambo ambayo kimsingi hupaswi kumwambia mpenzi wako,,kwani endapo utaamua kumwambia utatengeneza njia ambayo itafanya mahusiano yenu yafe mara moja,,
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile
1.Nakuchukia
Chuki ni kitu kikubwa sana,,kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambae unamchukia,hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili,,unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe.
2.Maneno ya matusi
Maneno kama mjinga au mpumbavu,,,yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha linapotoka kwa mwenza.
3.Kumfananisha tabia mbaya mwenzi wako na wazazi wake
Tabia zako kama mama yako au kama baba YAKO,,,maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonda kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.
4.Acha nitafanya mwenyewe
Katika mahusiano jambo la kusaidiana ni la kawaida na muhimu,,maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mwenza wako kutaka kufanya jambo siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.
5.Maneno mabaya ya kukatisha tamaa
Hutaweza hutafanikiwa n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo,,,ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote mwende mbele kwa pamoja,,,umoja ni nguvu.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2Z8pQVJ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment