Akiongea na East Africa Radio kwenye kipindi cha PlanetBongo, amesema iwapo BASATA wataamua kumchukulia hatua waanze kwanza kwa kujihukumu wenyewe, na kisha ndio wamfuate.
“Hao BASATA wenyewe nafikiri wamo umo ndani, umo wataanza kesi yao wenyewe alafu ndo waanze kwa wengine, sitaki kuzungumzia sana hii ngoma lakini naweza nikasema BASATA pia wanahusika kwenye hii ngoma, wamo humo”, alisikika Ney wa Mitego akisisitiza kuhusu kuwepo kwa mstari uliowachana BASATA.
Loading...
Kwenye wimbo huo Ney amesema “Hizi taarifa zangu na ziwafikie BASATA nyie ni kuku au bata, msumeno usiokata, kazi kufungia nyimbo mnajua shida tunazopata? Hamjui wajibu wenu mgekuwa watoto washawachapa”.
Pamoja na hayo Ney amesema ameamua kutoa wimbo huo kwa kuwa aliona game limepoa na watu walikuwa wanahitaji kitu kama hicho.
“Ni wimbo ambao nimeongea vitu vingi sana, wananchi nimewapa kitu ambacho walikuwa wanakihitaji, kwa muda mrefu nimewaletea muziki mzuri ambao watanzania watapenda kuusikia siku zote, kwa sababu wasikia kitu ambacho wanakijua, muda mrefu sana wamemiss muziki wa hivi, muda mrefu game imepoa, muziki umelala this time nimewaletea kitu ambacho wanataka”, alisema Ney wa Mitego a.ka. True Boy
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2l7A0aL
No comments:
Post a Comment