Thursday, June 20, 2019

ZINGATIA HILI KUFANYA MPENZI WAKO AONEKANE MTU MBELE ZA WATU


Mpenzi msomaji, bila kuchelewa niende moja kwa moja kwenye makala yangu ya wiki hii ambapo nazungumzia namna unavyoweza kukitumia kipato chako katika kulinogesha penzi lenu kila siku iendayo kwa Mungu.
Katika hili naomba nitangulize angalizo kuwa, kwenye mapenzi ya dhati si lazima fedha itumike kama chombo cha kuyaboresha lakini inapokuwepo na ikatumika ipasavyo, kuna uwezekano uhusiano wenu ukawa bora zaidi.
Kwa nini nasema hivyo? 
Wapo wanaume ambao wamekuwa wakiwafanyia mambo ya ajabu sana wapenzi wao. Unamkuta mwanamke ameolewa na mume wake anafanya kazi nzuri tu lakini angalia maisha wanayoishi. Mwanamke anavaa ili mradi kavaa, anakula ili mradi siku ipite lakini mume wake ana fedha ambazo zingeweza kumfanya mke wake naye aonekanae mtu mbele za watu.
Wanaume wenzangu, wanawake ndiyo wanaotupa furaha katika maisha yetu ya kila siku, ndiyo maana wanawake wakitufanyia mambo tofauti na yale tusiyotarajia tunajisikia vibaya sana na wakati mwingine kuchanganyikiwa.
Kwa maana hiyo basi pale tunapojaaliwa kuwa na fedha, tusiwe wagumu wa kuzitumia na wapenzi wetu. Itakuwa ni jambo la ajabu kama tutakuwa na uwezo wa kuwanunulia watu bia lakini nyumbani wake zetu wana wakati mgumu.
Ndiyo maana leo nimediriki kuandika makala haya kukueleza wewe mwanaume kuwa, hutakiwi kuwa mbahili kwa mtu uliyetokea kumpenda, unachotakiwa kufanya ni kumuwezesha  katika mahitaji yake muhimu pale ambapo utaona fedha kwenye ‘waleti’ yako inaruhusu.
Lakini na wanawake nao waone wana jukumu la kuwafanyia mambo kadhaa watu wao waliotokea kuwapenda. Hapa nawazungumzia wale ambao nao wana mishemishe zao zinazowaingizia fedha.
Unaweza kuwa mstari wa mbele katika kuchangia mahitaji muhimu ya kifamilia lakini pia usiwe mgumu kumnunulia mume/mpenzi wako chochote ambacho unaamini ataona unamjali kama ambavyo na wewe utafurahi pale atakapokufanyia hivyo.
Kuna wakati wewe mwanamke utapenda mpenzi wako akuwekee vocha kwenye simu yako na wewe wakati mwingine fanya hivyo kwake. Hivyo itawafanya muamini kuwa kila mmoja yupo kwa ajili ya mwenzake.
Utegemezi haukatazwi katika uhusiano lakini iwe hivyo tu pale ambapo mmoja kati yenu atakuwa hana njia yoyote ya kujiingizia kipato. Lakini kama unao uwezo kifedha na bado hujisikii kumfanyia mambo flani mpenzi wako, wewe utakuwa huna mapenzi ya dhati kwake.
Kwa nini nimeandika makala haya?
Juzi wakati niko ofisini nilipata fursa ya kutembelewa na dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Eliza.
Katika mazungumzo yetu alinieleza kuwa, miaka ya hivi karibuni alibahatika kuolewa na mwanaume ambaye anafanya kazi lakini maisha anayoishi ni ya kifukara sana. Anasema:
Huwezi kuamini mume wangu anafanya kazi na anapokea laki tano kwa mwezi achilia mbali marupurupu mengine lakini sijawahi kuionja fedha yake, nikimwambia nina shida flani ananiambia hana fedha wakati anatoa harufu ya pombe mdomoni.
Jamani, nilishawahi kusema kuwa mapenzi na fedha ni vitu viwili tofauti lakini itakuwa haileti picha nzuri kama utakuwa na uwezo kisha mpenzi/mke wako akawa hana tofauti na yule aliyeolewa na fukara. Ifike wakati ujiulize, kama huyo ni wako usipomhudumia unatarajia nani amhudumie?
Hilo ni kwa wale wenye uwezo kidogo kifedha ila kwa wale wenzangu na mimi wasio na uwezo, hawatakiwi kujali wala kujiona kwamba labda kutowapa wapenzi wao fedha ama kuwanunulia zawadi wataonekana
hawawapendi.
Kumbuka mapenzi ya dhati ni yale yanayotoka moyoni. Kumuonesha kwako mapenzi ya dhati itakuwa ni sabuni tosha ya roho yake




from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/31Nu7zE

No comments:

Post a Comment