Wednesday, June 5, 2019

WANAWAKE; EPUKA WANAUME HAWA MAISHANI MWAKO



Kuna wanaume kuwa nao kwenye mahusiano wanaweza kukupotezea sana muda na, hakuna mwanaume mbaya hata siku moja na kwamba hakuna mtu mkamilifu katika mapenzi lakini inapofikia wakati inabidi  kutambua kuwa mwanaume uliyenae ni sahihi kwako au la.
kwa wanawake, sio kila mwanaume anaekufata na kukutongoza anakuwa anataka kuwa na wewe, unaweza kuwa na mwanaume na kudumu  nae katika mahusiano kwa muda mrefu lakini  kichwani  mwake anajua kuwa wewe sio mkewe na muda wake wa kuoa ukifika anakuachilia mbali.
Hivyo basi ebu jaribu kukaa mbali na watu hawa :-
Wanaume wapenda ngono.
Wapo wanaume wanaoamini kwamba hakuna upendo wa kweli bila kufanya mapenzi. Hili ni kundi ambalo kwa mantiki ya haraka hawana lengo la ndoa bali wanalenga kutimiza tamaa za mwili. Japokuwa wapo wanaojihusisha na ngono kabla ya ndoa na kufanikiwa kuoana, hilo halitakiwi kusifiwa au kupendekezwa kwa namna au sababu yoyote ile na jamii yetu.
Wanaume wapenda ngono wana mbinu kali za ushawishi, huanza taratibu kwa mambo madogo madogo, huonesha uaminifu mwanzoni lakini kwa namna ya masihara hujikuta wamekuangusha kwenye uzinzi. Watu wa namna hii wanajua kujali, hawajui kuonya ukikosea, ni wepesi kuitikia hitaji lako, anaweza kuahirisha kazi ili tu achati na wewe anapogundua u mpweke.
Wanaume “watoto
Wanaume ambao wanaanza mahusiano lakini wana akili za kitoto. Si ajabu kumkuta mwanaume ambaye hawezi kufanya maamuzi bila mchango wa wazazi wake. Ukiwa na mwanaume kama huyo ujue dakika yoyote atakapoambiwa we humfai utaachika bila sababu. Kifupi hawapendi kuzungumzia ndoa. Kuna tofauti kati ya wanaochelewa kuoa na wasiopenda ndoa, hapa nazungumzia wasiopenda kujadili kuhusu ndoa. Hukwepa kwa sababu kisaikolojia wao bado ni watoto.
Wanaume “wapenda ukamilifu”
Lugha nzuri tunaweza kuwaita “perfectionists” na sio vibaya ukawajumuisha na “judgementalists” kwenye kundi hili. Hawa ni wanaume ambao wanataka kila kitu kiende sawa sawa na kilivyopangwa.
Judgementalists ni wanaume wanaopenda kujudge kila kitu, yaani hakuna kitu utafanya wasiulize maswali. Hawajui kutia moyo, kusifia au kupongeza. Kuishi na wanaume wa namna hii ni lazima ujipange. Ni wepesi kubadili maamuzi bila kujali muda na rasilimali mlizotumia kwenye mahusiano yenu.
Wanaume wenye mtazamo hasi (Negative minded men).
Mara nyingi wanaume wanapenda wanawake wabadili tabia ili kuwafaa wanaume na sio kinyume chake. Sababu za kuwa na mtazamo hasi ni nyingi kutokana na mtu mmoja na mwingine. Wengine ni kwa sababu ya kutojiamini, wengine ni kutokana na mambo ambayo umewahi kumfanyia kwenye mahusiano yenu, wengine historia za maisha yao ya utotoni na wengine ni kwa sababu ya wivu uliopitiliza kwa hiyo anawaza kuibiwa tu na mengine mengi.
Wanaume wanaoigiza maisha (pretenders)
Hawa ni wanaume ambao hawajakubali hali zao za maisha. Kama ni maskini atataka aonekane tajiri. Akijuana na mtu maarufu basi na yeye anataka aonekane maarufu. Wanaume wa namna hii ukiwagundua hawaoni shida kuvunja mahusiano ili kuficha aibu yao.  Kifupi hawa ni wanaume ambao hawana mikakati thabiti ya maisha yao, hufuata upepo na mara nyingi hawana uwezo wa kweli wa kutunza familia


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2XnXDcO

No comments:

Post a Comment