KUNA wanaume wanaoishi kwa masononeko makubwa kwa kukosa kujimudu wakati wa shughuli chumbani.
Wanavyosimulia vidosho ni kwamba wanaume hao huachilia goli moja na kuishiwa na nguvu huku wakiacha wachumba au wake zao wakitamani ngoma zaidi.
Ukweli mchungu ni kuwa wanaume kama hao huwa na wasiwasi wakunyang’anywa wachumba au wake zao na mafisi wanaojua kuwashaghulikia propa na kukata kiu cha uroda.
Kuachilia goli moja kwa dakika tatu humuacha mwanamke akiwaka na anaweza kukuchukia sana na hata kukunyima asali. Mwanamke hupenda kukolezwa uroda sio kumuamsha hisia na kushindwa kuzizima.
Ukiwasha moto, unafaa kujua kuuzima na kama hajui kuuzima, la busara ni kutouwasha. Hofu ya wanaoshindwa kuwarithisha wapenzi wao kupokonywa na wanaume wengine ni ya kweli.
Mwanamke kama huyo akiangukia mwanamume anayejua kulima shamba kikamilifu ni rahisi kumtema mtu wake.
Ajabu ni kwamba akifikia uamuzi huo, mwanamke huwa hakumbuki mazuri mengine ambayo mwanamume huwa amemtendea.
Anamdharau hadharani. Utasikia mwanamke akimwambia mumewe hafai kutajwa wanaume wanapotajwa. Lugha kama hiyo huwa ya wanawake wanaochepuka yaani wale ambao wameonja asali nje na wanakolezwa utamu wake.
Wanaume wasiotamba chumbani mara nyingi huwa na hasira wanawake wao wakiwadharau na baadhi yao huchukua hatua zinazowaletea majuto.
Kuna wanaojitia kitanzi, kuwaua au kuwajeruhi wake zao. Hizi ni hatua ambazo hazisaidii chochote. Wanachofaa kufahamu ni kwamba kuna njia nyingi za kumfanya mwanamume kunguruma chumbani katika tendo la ndoa na kukata kiu cha mpenzi au mke wake.
Ili kufanya hivi hatua ya kwanza na muhimu kabisa ni kuelewa kinachokufanya kuwa bwege wakati wa shughuli au kutotamani ngoma au kutoimudu.
Uking’amua tatizo, ni rahisi kupata dawa yake. Na simaanishi ni lazima mtu apate dawa. Amini usiamini, tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume mara nyingi halihiitaji dawa mbali huwa ni la kisaikolojia.
Tafiti zimeonyesha kuwa wengi wanaoshindwa kuwika kitandani huwa na mfadhaiko, yaani wale wanaume wanaojibebesha mzigo wa mamilioni ya tani katika mawazo yao. Kama stress ni ya kazi, iwache ofisini au kiwandani, usiipeleke nyumbani.
Tenganisha kazi na mapenzi, tenganisha masuala yote na uwe na wakati wa uroda. Inasemekana kuwa mwanamume akikose kupata shibe la uroda au asiyejiweza chumbani hawezi kufanikisha lolote.
Pengine ni kweli. Hili ni suala ambalo tutaendelea kuangazia katika meza ya mapenzi lakini kwa sasa, wanaume, wacheni stress, zinazima jogoo. Wacheni ulevi wa kupindukia, sigara na mihadharati.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2WdTDKp
No comments:
Post a Comment