Friday, June 21, 2019

SHOGA KAMA WAMPENDA MPE MASHAMSHAM MUMEO ATULIE NYUMBANI


Leo shoga yangu nataka kuzungumza nawe kuhusu mada yenye kichwa hicho hapo juu, naamini nitakapofika mwisho utakuwa umepata darasa la kutosha.
Nimeamua kutiririka na mada hiyo baada ya baadhi ya wenzetu kuwalalamikia waume zao kwamba hakuna siku wanayotulia nyumba wao wapo bize tu!Shoga yetu mmoja mkazi wa Ubungo Maziwa aliniambia kwamba anamshangaa mumewe, hata akiwahi kutoka kazini akishakula tu anamuaga kwamba anatoka kidogo.
“Yaani mume wangu namshangaa sana, hakai nyumbani kabisa, ikitokea kawahi kurudi akila tu anaondoka, anasema anakwenda kwa rafiki zake au kuangalia mpira, kurudi saa saba usiku,” alilalamika shoga yetu huyo.Kwa maelezo ya shoga yetu huyo nimebaini sababu kubwa ya baadhi ya wanaume kutopenda kukaa nyumbani ni wake zao kutokuwa na mashamsham ya malovee.
Nasema hivyo kwa sababu wapo wenzetu hawajui hata namna ya kuwapokea vifurushi na kuwakaribisha waume zao walirudipo nyumbani kutoka kazini.
Hawana kauli za mahaba kwa waume zao, sasa wanategemea nini kama siyo kuwakimbiza waume zao ‘home’ na kwenda kwenye baa kuangalia mpira na kupata kilevi na marafiki zao?
Wapo wenzetu ambao hawajui kama mahaba ni muda wowote na kwa wanaojua hilo wanainjoi sana wanapokutana na waume zao asubuhi, mchana na usiku.
Shoga ambaye huna utamaduni wa kufinyana na mumeo mchana au jioni, hebu anza utamaduni huo bila kusingizia kwamba unashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya watoto.
Kumbuka bila ya huyo mumeo watoto wasingepatikana, kwa kuwa mumeo ni namba moja unapomhitaji au yeye kukuhitaji mchana, msinyimane jamani.Ili muwe huru, wapatie fedha wanao na kuwaambia waende sehemu yoyote kupata chipsi, kinywaji huku nyuma mpe raha mumeo uone kama hatatulia nyumbani.



from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2xb5ij6

No comments:

Post a Comment