Sunday, June 2, 2019
MWANAUME WA KWELI HAWEZI RUHUSU HAYA KWA MWANAMKE
Mwanaume wa kweli kwako hatakuacha ujisikie mpweke,,,hata kama hayupo karibu na wewe atajitahidi kufanya mambo ambayo yatakufanya ujisikie faraja na uwepo wake kwako
Mwanaume wa kweli kwako atakupigia simu kutaka kujua unaendeleaje,,,,atakutumia ujumbe kukwambia AME miss uwepo wako.
Mwanaume wa kweli kwako hatakudanganya wala kukuficha mambo yake kwako.
Mwanaume wa kweli kwako atakufanya wewe kipaumbele kwake,,atakuonyesha kuwa uwepo wako anafaidi kitu.
Mwanaume wa kweli kwako hatakudanganya na wala hatajaribu kukubadilisha,,atakufanya siku zote mwenye furaha na tabasamu usoni mwako.
Mwanaume wa kweli kwako atakuvumilia katika mapungufu,, atakurekebisha panapostahili.
Mwanaume wa kweli kwako hatajaribu kukusema vibaya wala kukutukana,,kiufupi atakuonyesha heshima ukiwa pekee yako au mbele ya watu wengine.
Mwanaume wa kweli kwako utamtambua tangu siku ya kwanza mnaanza mahusiano,,usipuuze tabia ambazo anazo ambazo unahisi hutaweza kuzivumilia kwasababu kuingia kwenye mahusiano na asiye aina yako ni mzigo.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2WbwNDg
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment