Mahusiano Baina Ya Mwanamme Na Mwanamke
Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi. Jee, unapata raha na una amani katika mahusiano yako na mpenzi wako? Huna wasiwasi wo wote na mahusiano yenu kwamba labda mkeo ana mahusiano na mwanamme mwingine? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza.
Kama mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.
Kama kuna mambo yanasababisha tendo la ndoa lisifanyike kwa urahisi, ufanisi na kufurahia, hamu ya kufanya tendo hilo inaweza kupungua. Kwa mfano, kama mwanamme unawahi kufika kileleni au una matatizo ya jongoo wako kupanda mtungi, tendo zima la ndoa halitakuwa la kukufurahisha sana hivyo unaweza kupoteza hamu ya kulifanya. Hebu fikiria tunda linalokufurahisha sana ukilila, ukilikosa kwa siku kadhaa, utalikumbuka na kulitafuta lakini ambalo halikufurahishi sana ukilila hutalikumbuka na kulitafuta.
Mawazo Mengi Na Uchovu
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia. Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani. Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.
Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi. Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.
Matumizi Ya Madawa Na Pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na:
– madawa ya high blood pressure
– madawa ya kuondoa msongo wa mawazo
– madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone
– na mengineyo
Umri Kuwa Mkubwa
Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanammme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. Kama thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.
Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.
Matatizo Ya Kiafya
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2Ih1JNu
No comments:
Post a Comment