Watafiti wameonyesha kuwa wale wanaosikiliza kwa makini wamekuwa na mafanikio makubwa katika mahusiano yao.
Katika sehemu nyingi ambazo nimegundua katika mahusiano kuna mtu mmoja anayeongea sana na mwingine huwa anasikiliza . Lakini… Msikilizaji anasikiliza kweli? watu wengi hufikiria kuwa wao ni wasikilizaji wazuri.
Lengo la usikilizaji wa kina ni kupata taarifa, kumuelewa mtu au mazingira. na kuwa radhi. Usikilizaji mzuri ni kuhusu kuweka ufahamu wako kuamua kusikiliza kitu kinachosemwa. ni kuwajibika kabisa kwa wengine. maneno yao na ujumbe wao. bila ya kuingilia .
Inaonekana kwamba sababu zilizo nyingi ambazo watu hutafuta tatibu ni kutaka historia zao zisikilizwe. Ili uweze kusikilizwa historia yako , unahitaji kupata mtu wa kukusikiliza . Msikilizaji mzuri. Ukiwa ni msikilizaji mzuri, na ni mtu wa kuelewa na kutambua mbinu za ujuzi wa kujifunza, kuwa kiongozi, na unaweza kuwa tatibu mzuri. Ujuzi wa kusikiliza unaweza kujifunza. Lakini ukweli ni kwamba, kuna watu huwa ni wasikiliza wazuri kuliko wengine.
Umuhimu wa kuwa na usikivu katika mahusiano ya watu wawili huenda hayatiliwi mkazo kama inavyotakiwa. Kuna aina mbili za usikilizaji. Kusikiliza kwa ajili ya kuelewa . Na kusikiliza kwa ajili ya Kujibu. Kwa wale ambao wanasikiliza kwa ajili ya kuelewa wana utoshelevu mkubwa katika mahusiano yao kuliko wengine. Ingawa kuna watu wanaweza kuwa wanataka kusikiliza ili kuelewa lakini kumbe wanasikiliza ili wajibu.
Mtu anayetaka kumbadilisha mwenzake, mara nyingi ni yule mwenye kusikiliza kwa kutaka kujibu. Utafiti unaonyesha kuwa , Wanandoa ambao wanaenda kwa mshauri wa ndoa mara nyingi kwa pamoja huwa ni watu wanaosikilizana na kuelewana kuliko wengine kwa sababu wanakuwa wamepata mbinu muhimu za kuwasaidia.
Inasemekana kuwa Wanawake wanahitaji kusikilizwa. Ni kweli. Na wanaume wao ni kutaka kurekebisha na kutengeneza au kutaka kujibu.
Utendaji au usikilizaji wa kina upo ndani ya kila mahusiano yaliyo na afya. Pia kuna matokeo mazuri ya kukua na kuleta mabadiliko. wale ambao husikilizwa wanakuwa wazi zaidi, wanakuwa na uhuru wa kuamua katika njia zao, sio watu wa kujihami.Wasikilizaji wazuri hawana hali ya kuhukumu mtu, hutengeneza mazingira salama na kuweka akili, mwili na roho ya mzungumzaji kuwa salama.
Kwa kusikiliza kwa makini wakati mtu anaongea, utakuwa unamwambia kuwa unamjali kwa kile anachokisema. ikumbukwe pia kuwa kumsikiliza mtu ni kumponya. tunaposikiliza wengine, tunaweka nafasi ya kusikilizwa.
Habari nzuri ni kwamba tunaweza kujifunza jinsi ya kuwa wasikilizaji wazuri; Ingawa itahitaji zoezi la kutosha. tunapozidi kufanya hivyo. ndivyo tunapoweza zaidi. na kadri tunavyokuwa positive, mahusiano yatakuwa mazuri.
Hapa kuna mbinu za kukuwezesha kuwa msikilizaji mzuri.
-Jiweke mwenyewe ndani ya akili ya mzungumzaji. vaa kiatu chake.
-Sikiliza kwa kumaanisha
-Kuwa makini kwenye lugha ya mwili wako
-Jitihada ya Uelewa
-Epuka kuhukumu
-Tazama macho ya mtu anayezungumza
-Kuwa makini na hisia za mwili
-Tambua hofu ya mwongeaji
-Rudia kwa maneno yako kwa kuonyesha uelewa kwa yale anayoongea.
-Onyesha kuwa kweli unasikiliza kwa kuitika kwa kichwa au kusema mh, uh-huh…
Hapo utakuwa umemweka katika hali ya ulinzi mkubwa mtu anayekueleza jambo lake.
Shirikisha wengi kama umefaidika na makala hii.
from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2WNOJIx
No comments:
Post a Comment