Sunday, June 2, 2019

MAMBO HAYA YATAFANYA MWANAMKE ASIKUCHOKE NA ASIKUACHE




Upendo ni kitu ambacho hakizuiliki. Napale patakaposhikilia ule upendo ipasavyo ndo husikii wala huoni utakaloambiwa juu ya akupendaye. Matendo mbalimbali yanayofanywa na wale wapenzi moja kwa moja huchochea upendo wa moyoni ambao hudumu milele, ndio hapo utasikia keshapewa madawa, mara mke wake kamkalia kila atakachoomba lazima apewe na mengine mengi ambayo umekumbana nayo au kuyashuhudia kwa watu wengine.
Moja kwa moja niende kwenye hivo vichochezi kama ifuatavyo:
Kusikiliza na kua mshauri mwema kwa mwenzako. Iwe ni kuhusu familia yake au mipango yake ya baadae au kimasomo, kikazi na hata kibiashara. Ikumbukwe kuwa mafanikio ya mmoja ni chachu ya maendeleo mazuri hata mtakapokua katika familia.
Kujishusha panapotokea kutokuelewana (yaani kuwa mwepesi wa kuomba msamaha). Majibizano siku zote hayajengi hasa mnapokua mna hasira au mmoja kati yenu ana hasira.
Neno ahsante ni dogo sana ila lina couragement kubwa saana, Ukipongezwa na hata unapopewa pole shukuru. Unapopewa chochote na mwenzako iwe ni ushauri, maoni, mawazo mapya juu ya miradi mbalimbali au kazi huna budi kushukuru.
Mwepesi wa kusamehe na kusahau. Vilevile mwelekeze mwenzako pale alipokosea ili siku nyingine kitendo hicho kisitokee. Usiwe mwombaji mzuri wa msamaha huku wewe hautoi.
Msifie mwenzako anapopiga hatua ya maisha anapokua katika muonekano mzuri n.k Usisubiri jirani amwambie. Tena hapa muwe makini sana maana ni rahisi kwa mwingine kuvutika upande wa pili kwa ajili yakusifiwa(Kusifia kunajenga picha ya kujali) japokua sio wote wanamaanisha.
Kuwa mkweli na mwaminifu katika mahusiano yenu
Usisubiri matukio maalum ndo utoe zawadi kama vile birthday, valentine day n.k, Mpe wakati wowote unapokua na uwezo wakumpa.
Usimuulize mpenzio anataka zawadi gani. Siku zote zawadi ni kitu ambacho mpokeaji hakijui na wala hatakiwi kukijua kabla hujampelekea. Kuna zawadi nyiingi sana ambazo unaweza mpa mwenza. Na kupitia muda wa urafiki wenu naamini utaweza kujua walau nusu kama si robo tatu ya vitu anavyovipenda. Ila jitahidi uwe ni muibuaji wa vitu vipya sio vilivyozoeleka.
Natumaini kwa kiasi fulani vitu kama hivyo kutoka kwa mwenza wako vimekufanya au vinakufanya umpende zaidi. Au ukosaji wa vitu hivi kwa mwenzako vimekufanya mshindwe kuendelea kua katika mahusiano au kuvunjika moyo. Jiheshimu na pia muheshimu mwenzako pamoja na hisia zake, mjali, mthamini, mtie moyo, mrekebishe anapofanya ndivyo sivyo na lingine ni kuombeana Baraka za mwenyezi Mungu zikae nanyi nakuwaongoza katika kila jambo.


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2MoZpcz

No comments:

Post a Comment